Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Mimi kwa uzoefu nilio nayo na account za ESCROW ni kuwa ile Fedha zilizomo katika ile account bado hazikuwa za IPTL japo kuwa zinatakiwa kulipwa IPTL. Ingelikuwa ni za IPTL zingekuwemo katika account yake ila kwavile kuna mgogoro, Escrow Account (third party holder) ikafunguliwa. Kwahiyo zile Fedha ni bado za Tanesco. Na tusisahau kuwa Mule ndani kuna fedha za TRA.
Sasa Suali linakuja je fedha za tanesco na TRA ni za Umma au sio za Umma?
Sasa ikiwa tanesco na TRA ni Private companies basi fedha sio za Umma ila ikiwa ni Public companies tusidanganyane zile fedha ni za Umma tu.

Sasa kutokana na Taarifa za CAG na PCCB kuwa PAP sio wamiliki halali wa IPTL. Na waziri na timu yake pamoja na Mwanasheria mkuu wamehusika na ruhusa za kutoka zile fedha kwa tapeli ambae anajulikana Duniani kuwa ni mtu wa Fraud.
Kwahiyo PAC hawakutoa uongo ndani ya bunge wao wametoa Report ya uchunguzi uliofanyika kutoka report ya CAG na uchunguzi wa PCCB na TRA.
 
Si kwamba hoyo Pasco hatambui kuwa hizo pesa ni za umma laa...! Bali apenda kuwatweza zenyu akili maana yu kazini.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi, with due respect, tubishane kwa hoja tuu na sio kwa emotions, hata uthibitisho ukithibitisha PAP ni mwizi, ameinunua IPTL kwa utapeli, then hizo fedha zilizoibiwa ni fedha za IPTL!, sio fedha za umma!.
  1. Tanesco ni shirika la umma, litatumia fedha za umma kulipia huduma, zile fedha zikiisha change hands na kumfikia service provider, zina change form, from fedha za umma to fedha binafsi.
  2. Escrow ni account iliyofunguliwa katakana na mgogoro wa kiwango cha capacity charges mlalamikaji ni Tanesco na sio IPTL!, hivyo determinant ya fedha kutoka ni Tanesco na sio IPTL!.
  3. jumla ya deni la IPTL kwa Tanesco ni bilioni zaidi ya 300!, ndani ya escrow kulikuwa na bilioni 128!. Hivyo bado Tanesco inadaiwa zaidi ya bilioni 180!.
  4. Tanesco na IPTL walikaa na kukubaliana kwa maandishi, kuwa wamekubali kuwa fedha zote ni za IPTL walioridhia IPTL walipwe!. Hivyo hata kama zingekuwa ni fedha za umma, baada ya fedha hizo kulipia huduma, wajemeni sio fedha za umma tena!.
  5. Kuna swali nimeuliza na sijabahatika kupata jibu lolote la maana kuwa kama account ya escrow ni ya Tanesco na IPTL, na fedha zilikuwa za IPTL, ilikuwaje BOT ikailipa PAP ambaye ni third party?. Sakata la Escrow: Did "BOT Had a Role to Play?, or Just An Innocent Victim?
  6. Alichofanya Singasinga ni kula dili ya kuuibia IPTL na sio serikali, kwa sababu hata ingekuwa kama IPTL na Tanesco wangekubaliana kuipunguza capacity charge to 50%, bado fedha zote zilizomo ndani ya account ya escrow, bado zingekuwa ni za IPTL.
  7. Kwa vile invoices ni za IPTL ambayo inalipa VAT, na hata kama PAP alidai ameinunua IPTL, BOT ilibidi kuzilipa hizo fedha IPTL, kisha IPTL ilipe kodi ya serikali, ndipo imlipe PAP ambaye sio VAT registered!, ilikuwaje invoice za IPTL zenye kodi, akalipwa PAP ambaye hana VAT?!.
  8. Huu mjadala umefika hapa kwa sababu wengi wetu tunajadili kwa kutumia emotions na sio reasoning, tuwewke emotioms pembeni, tendwe kwenye facts tupu, tutakubaliana!.
  9. Hata kama fedha za escrow sio za serikali, haina maana Tanzania hatuibiwi, bali sioni yoyote anayezungumzia hili jinamizi la IPTL lilitokea wapi na majinamizi mengine kibao yaliyopo, watu wameshupalia tuu escrow, huku tunaibiwa mara mia kuliko escrow na watu mmenyamaza!.
  10. Mjadala wa escrow umenifumbua macho how ignorants we are!.Escrow: Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.Tuache Cherry Picking !.
Pasco
 
Pasco unaonaje ukaeleza hio maana ya "fedha za Umma"
Mzee wa Conspiracy, nikieleza itafika mara 100 sasa, ila kwa faida yako na wengine ambao hawakuliona jibu la awali, nitarudia.
 
prof mark mwandosya kaeleza vizuri sana pesa zimeibiwa kutoka ac ya escrow iliyokuwa chini bot na ndiyo maana gavana alikuwa anachukuwa tahadhari kubwa sana kuzitoa lakini pia kaongeza kuwa mabenki yote yako chini ya bot yakiibiwa au kufilisika bot inalipa kama yameshindwa kulipa kwa msingi huo hata hizo pia ni fedha za umma twende kwenye pesa ambazo tanesco walikuwa wanadai kutozwa zaidi kutokana iptl kutotimiza baadhi ya masharti ya mkataba kwa hiyo kwenye ac escrow kwa miaka 12 tanesco kuna pesa yao na wameshinda kesi na kinachotakiwa ni kupiga hesabu upya kwa mujibu wa madai ya tanesco tatizo hauwezi kupiga hesabu wakati pesa zimeshaliwa.
na cheyo kalieleza vizuri aliyelipwa siyo iptl bali pap aliyedai kauziwa shares na piperlink kwa nyaraka za kugushi harakaharaka kalipwa pesa za iptl inatakiwa kama ingelikuwa kweli angebeba na madeni ya iptl iliyokopa benki ya standard chatered ya hongkong lakini tunavyosema pesa zimeshabebwa zote account ya pap imefungwa sasa madeni yote ya iptl tutayalipa sisi kwa kuwa iptl walikopa wakiwa na government guarantee sasa kuna watu wanadhani hatujaibiwa akili nzito kiasi gani cheyo kidogo alie machozi na bora angelilia kabisa nchi hii inaumwa nini?
 
Sawa sio zetu...Na kodi?
Kampuni zinapouziana hisa lazima zilipe Huyo aliegawa kalipa kodi ila huyo mwenye hisa nyingi kaondoka na kodi zetu tafsiri Sahihi ni Mwizi.
 
Mara nyingine watu hutaka kuonyesha usugu wa akili zao na kujifanya kila kitu wanajua,ndio maana Mama Makinda akasema ikiwa wewe si mwanasheria ila unatoa ushauri wa kisheria then wewe ni bush Lawyer.

Hiyo Escrow imeelezwa na wataalam kuzidi Pasco ambaye si mchumi,si muhasibu.......lakini hpa unataka kutuaminisha na tuchukue kile unachosema wewe wakati unajua kabisa si sahihi.Hakuna watu ninawakubali kama Wasira,Zitto Kabwe,na Luhaga Mpina,ninawakubali kwasababu wako fresh sana upstairs,mwanzo sikuilewa kabisa hii ishu ila niliamua kujifunza kutokana na hoja zilizoletwa na nimegundua kuwa humu ndani ya Jukwaa kuna watu kwa makusudi kabisa wanataka kutupotosha.

Labda ni kwa makusudi au vyovyote vile lakini ukweli mioyoni mwao wanaujua.

Tupeni ukweli hata kama unauma.
 
Unajua nyinyi watu. Kuna majamaa wasio viongozi wa serikali pia wamepokea huo mgao. Escrow imegusa sehemu kubwa ya jamii kuanzia dini,serikali na hata tasisi binafsi.

Mpumbavu atajitetea na isitoshe wengi wanakuja hapa kutetea hoja kwamba sio maili ya umma maana wamefaidika nazo kwa namna moja au nyingine.
Kwanza hujui historia ya IPTL mpaka baada ya escrow watu ndio wanajua.
Pili,ni wapi duniani watu wanapeana fedha binafsi kwa mabilioni na serikali isiulize?
Je serikali ya kikwete iliuliza ? Kwanini askofu apewe hela binafsi? Kwanini mawaziri wapewe mabilioni? Kwa lipi hasa? Mana wao wamefanya kazi zaidi ya wengine?
In a simple logic tu,this non sense doesnt add up.
Na ndio maana tumekuwa kizazi cha kishenzi, maana ndio culture tunajeng hii; nipate changu kwanza.

Hii ni laana ya mwafrica toka enzi zile za mababu. Selling out another brother or sister ndio zetu.

We pasco unajifanya hujui waa hutaki kujua na unajua wazi hizo hela sio za watu binafsi.
Hawa watu wote waliopokea hiI fedha wengi na wafaham binafsi.
Wengi walikuwa kwenye uratibu wa deal la IPTL toka huko nyuma 1995.
Kwahiyo usionge ushenzi hapa.
 
Niwapongeze sana wasomi nyie kwani mnatuweka bayana kuhusu sakata hili...Hakika nawachukia wansiasa wanatumia bunge vibaya kwa malengo maovu...naomba sana tuwahukumu ifikapo 2015 kwa kuwanyima kura ili tupate wawakilishi wanaoteta maslahi yetu na siyo yao binafsi..
 
Kwa ugawaji huu wa pesa kwa kiongizi makini lazima ushtuke maana hii nisawa na kupindua nchi
 
Pasco unaweza kuwa sahihi kuwa hizi si fedha za umma lakini uchukuaji wake bank unadhirisha kuwa hizi ni fedha haramu. Uharamu wake unatokana na maelezo waliyotoa wanaotetea hoja kuwa hizi ni fedha za umma. Unachonitisha mimi ni kutuhumu PAC badala ya kutuhumu vyanzo vya PAC.
Na nashawishika kudhani Pasco ni hardcore member wa CCM maslahi. CCM maslahi hampendi mifumo ifanye kazi mnapenda mkubwa ndoo aamue.
 
Mkuu Ngozi Mbili, asante kwa hoja zako hizi, nimeziweka kwenye makundi manne.
  1. Kama zilikuwa ni fedha za umma, BOT ilizilipaje kwa PAP wakati mwenye pesa ni IPTL?!, siku zote fedha ni ama za aliyeweka, Tanesco, ama anayepokea IPTL, mwenye pesa za umma Tanesco, ndie aliyeikubalia BOT imlipe PAP, custodian wa fedha za umma hapa ni BOT, aliwezaje kulipa PAP ambao were not part to the contract?!. Ukijikuta umeingiziwa fedha kwenye simu yako ni jukumu la aliyeingiza na sio mpokeaji!.
  2. Nikweli ndani ya escrow kulikuwa na fedha ambayo Tanesco ingepaswa kurudishiwa kutokana na kuibiwa kwa miaka 12. Madai ya Tanesco ni very genuine, wakitaka wapunguziwe capacity charge. Japo mazungumzo ya kupunguziana bado hayafanyika, ila tuseme labda Tanesco wangepunguziwa capacity charge hadi 50 %, bado pesa yote iliyokuwemo ndani ya escrow ni bilioni 128 tuu, jumla ya fedha ambayo Tanesco inadaiwa hadi leo hadi kesho ni zaidi ya bilioni 300!, hivyo hata Tanesco wangepunguziwa vipi, hilo punguzo lisingerudisha hata senti moja back to Tanesco, hivyo ni Tanesco wenyewe kwa ridhaa yao, ndio walioruhusu fedha yote itumike ku ofset hilo deni la bilioni 300!.
  3. Kama ilivyo aliyelipwa ni PAP na sio IPTL, aliyekopeshwa na Standard Charted ni IPTL na sio PAP, PAP kauziwa kampuni bila kuuziwa madeni!. Mkopo wa ujenzi wa IPTL dola milioni 150 ulikopwa na benki ya Sime na Bumuputra za Maleysia, ili fedha zilizofika huku ni dola milioni 80 tuu!. Mechimal ikafilisika huko kwao, deni lake likanunuliwa na benki nyingine ya Maleysia iliyoliuza kwa Stan Chart Bank ya Hong Hong. Hivyo by the time Mechima anaiuza IPTL kwa Piper Link, IPTL original iliisha uzwa kwa Stan Chart, huku IPTL imeuzwa, huku Mechimar inaiuza IPTL kwa bei ya bure kwa Pieper link, wakati PAP ananunua IPTL toka Pieper Link, hakuuziwa deni lolote!, hivyo PAP hajui deni, wala hamjui Stan Chart, yeye kauziwa mitambo, Stan Chart wameuziwa makaratasi!. Hata mahakama yetu imeitambua PAP bila kulitambua deni la IPTL.
  4. Ni kweli mkpo ulikopwa kwa government guarantee, pesa zilizoliwa ni pesa za VAT, na zinalipika!, hata account ya PAP ikifungwa, mitambo ya IPTL bado ipo, na umeme bado unazalishwa!, hivyo kila kitu kinalipika!.
Pasco
 
Pasco unaweza kuwa sahihi kuwa hizi si fedha za umma lakini uchukuaji wake bank unadhirisha kuwa hizi ni fedha haramu. Uharamu wake unatokana na maelezo waliyotoa wanaotetea hoja kuwa hizi ni fedha za umma.
Mkuu Mpitwaga, kwanza asante, pili nakubaliana kuwa hizo fedha zimepigwa!, zimeibiwa!, mwizi ni PAP, ameiba fedha za IPTL zilizokuwa na VAT ndani yake!.

Unachonitisha mimi ni kutuhumu PAC badala ya kutuhumu vyanzo vya PAC.
Na nashawishika kudhani Pasco ni hardcore member wa CCM maslahi. CCM maslahi hampendi mifumo ifanye kazi mnapenda mkubwa ndoo aamue.
Hili la mimi kuwa CCM sina tatizo nalo kabisa!, Pasco wa JF ni Mwana CCM damu ila anajifanya hana chama!.

Hizi ni baadhi ya Threads zangu kutetea chama changu CCM na kumfagilia Mwenyekiti wangu wa chama!.

Mapungufu ya JK: Ni Rais Dhaifu! -

CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!
Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015 ...
Mtazamo: Kanda ya kaskazini, ccm imechokwa mpaka basi!
Katiba: Nashauri Bunge Batili Lililopo Livunjwe!, Liundwe Bunge Halali la Katiba!.
Mchakato Huu wa Katiba, ni Umasikini Wetu!, Tujikubali
Ikithibitika ZNZ Haikushirikishwa, P'se JK Simamisha Huu Mchakato Batili!.
Chonde Chonde Rais JK: Msimamo wa Serikali ...
Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha
Kama Kweli Nia ya Dhati ni Kuimarisha Muungano, Then

Kidumu cha Mapinduzi!.

CCM Oye!.

Pasco
 
Sawa sio zetu...Na kodi?
Kampuni zinapouziana hisa lazima zilipe Huyo aliegawa kalipa kodi ila huyo mwenye hisa nyingi kaondoka na kodi zetu tafsiri Sahihi ni Mwizi.

Kutokua imara kwenye kudai kodi ni uzembe wa TRA angalia nyendo zako usikurupuke kuita watu wezi
 

Thibitisha
 
Nafanya mapitio, kwa ku compare na ku contrast maoni yangu na ya JK!.

Pasco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…