Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

NB. Kuna vitu vitatu hapa msije kuchanganya
1. IPTL NI LIDUDU LILILONGIA NCHINI KWA RUSHWA MWANZO MWISHO.
2. ESCROW NI ACCOUNT YA UBIA WA TANESCO NA IPTL ILIYONUNULIWA KITAPELI NA PAP
3. FEDHA RUGEMALILA ALIZOGAWA NI FEDHA HALALI, FEDHA SAFI ZA MAUZO YA HISA ZAKE NDANI YA IPTL NA HAKUNA KOSA LOLOTE KUZIGAWA POPOTE KWA YEYETE, KWA SABABU YOYOTE AU BILA SABABU YOYOTE.
Kama PAP ametumia utapeli kuuibia serikali, this is none of JR business, kauza kihalali na kalipwa kihalali na kagawa kihalali, hakuna kosa lolote hapa.
Paskali
Hapo kwenye PAP. Je PAP ilianzishwa kutapeli hela za Escrow? Maana wenye mitambo ni benki waliokuwa na hati zake...Kwanini PAP kajifanya ndio mwenye kampuni na mmiliki wa hiyo mitambo?
 
Mkuu huko si unajua kuna walioambiwa wapumzike ssa wakifukua makaburi si itabidi na wenyewe wahusishwe!!!! Hta simba trust tu haitajwi sembuse waliochukua za stanbic !! Anyway muda ndio utaamua ila akimulika na huko serikali itakuwa imefanya jambo la kishujaa sana
Ila sawa Tumpongezee kwa hata hicho kidogo anachotufanyia kuhusu hili sakata kwa kuwapeleka mahakamani
 
si ndio kaanza!! yaani from no where unaanza kuondoa kila mtu serikalini kwa tuhuma ambazo lazima zithbitishwe na mahakama!!!!

hao wawili wataaibua chain nzima na utaona mashahidi kibao wakifika tu mahakamani....akitoka getini anadakwa
 
Kwenye kuvutisha mpunga, wako waandishi 4 wa habari, walivutishwa M.40 kila mmoja, ila hakuna kosa lolotekumpa zawadi mtu yoyote kwa appreciation ya kazi yake nzuri, kwenye media kosa ni kutoa pesa ku influence reporting.
Hili la waandishi kulipwa, nimelizungumza sana hapa
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco ...
P.
Ila kaka Pascal, kila mtu na fani yake, ma traffic wameonekana hawana kosa kupokea hela za ku brush viatu na kununua omo/bleach, nyinyi sio ndio hivyo pia au?! Yaani hela za kununua pencils/pens na notebooks!🙂😉
 
Hiyo attitude ya 'hicho kidogo' ndio ilitufanya tuamini sisi ni watu wa bora mkono uende kinywani, kwa nini tusipate kikubwa!?
Na hicho kidogo cha mahakamani kingelingana na 320/=bln, basi raia tungeelewa, yaani kufilisi makampuni yao utajiri wao mpaka zitimie, zuridishwe zifanye yale yanayotakiwa vijijini na mjini...siamini mbunge toka Bukoba au Bariadi akiomba hela za miundo mbinu wakati yeye anashiriki kuzitafuna?! Ni kichekesho kabisa, halafu anapigiwa makofi au kushangiliwa! Hawa viongozi wenye hila za kifisadi sidhani kama wana akili sawa kabisa...!
 
Ila sawa Tumpongezee kwa hata hicho kidogo anachotufanyia kuhusu hili sakata kwa kuwapeleka mahakamani
Yeah nampongeza ila natamani aendelee mpaka tujue kivp tulipigwa pesa na kodi kukwepwa hadi na viongozi wakubwa waliopewa mgao!!!! Ilikuwaje stanbic watu wakabeba lumbesa bila kukatwa kodi na bado wakaachwa!!! Yaani simba trust ni kina nani?? Katibu wa rais anapigaje pesa zote zile za MADILI afu hachukuliwi hatua kwa ufupi kuna mengi hatuyajui ila akifanikiwa kuwanyoosha hawa wezi wote mpaka kina chenge na werema atakuwa amefanya jambo la maana na atapewa pongezi zaidi hata na wapinzani kma walivylfanya lisu kafulila na zitto tayari
 
si ndio kaanza!! yaani from no where unaanza kuondoa kila mtu serikalini kwa tuhuma ambazo lazima zithbitishwe na mahakama!!!!

hao wawili wataaibua chain nzima na utaona mashahidi kibao wakifika tu mahakamani....akitoka getini anadakwa
Dah basi atafanya la maana sana nasubiri nione wamiliki wa simba trust wakiburuzwa kortini na wale waliopokea mabilion bila kulipa kodi hadi lumbesa stanbic...... naamini hta huko filikunjombe alipo atafurahi sana kuona alichokisimamia kimefanikiwa
 
Tangu lini CAG akakagua fedha/mahesabu binafsi?
Mkuu Nkese, BOT ni benki ya umma, fedha za escrow wakati zinahifadhiwa BOT zilikuwa ni fedha za umma, hivyo ni halali kwa CAG kukagua account ya escrow. Mgogoro ulipomalizika, zile fedha ndani ya account ya escrow zika change hands, toka kuwa fedha za umma na kugeuka fedha binafsi, zikatolewa BOT na kupewa wenye fedha zao!.

Tena Mkombozi Bank walifanya kosa kubwa kutoa siri za miamala ya wateja wao!, Stanbic waligoma!.
Paskali
 
Mkuu Nkese, BOT ni benki ya umma, fedha za escrow wakati zinahifadhiwa BOT zilikuwa ni fedha za umma, hivyo ni halali kwa CAG kukagua account ya escrow. Mgogoro ulipomalizika, zile fedha ndani ya account ya escrow zika change hands, toka kuwa fedha za umma na kugeuka fedha binafsi, zikatolewa BOT na kupewa wenye fedha zao!...Tena Mkombozi Bank walifanya kosa kubwa kutoa siri za miamala ya wateja wao!, Stanbic waligoma!.
Paskali
Kwenye Banking practice yaitwa "Confidentiality Clause", ila wajuzi waweza kutueleza kama yaweza kutenguliwa kwenye kesi kama hii, maana hili SAGA lilipoteza heshima ya TZ na watu wake duniani kabisa, mpaka ikafananishwa as a "Banana Republic"! Ndiyo haiwezekani zile Phd na Masters serikalini ziliweza kuruhusu uchafu ule...!
 
Confidentially of the recipients inaweza kuwa lifted kwa kutumia ombi kutoka FIU ya BOT only kama kuna mashaka kuwa fedha hizo ni dirty money na zimelipwa ili kuzi laundry. Au kama kuna mashaka fedha hizo zitatumika kufadhili ugaidi. Lakini fedha za JR ni fedha safi halali, zimetokana na biashara halali, kazigawa kihalali kwa watu aliowachagua.

Stanbic kamwe haiwezi kufanya ujinga kama wa Mkombozi Bank, recipients wote wa fedha za JR hawana makosa yoyote, wao wamepewa tuu kama sadaka.

Paskali
 
Kwenye Banking practice yaitwa "Confidentiality Clause", ila wajuzi waweza kutueleza kama yaweza kutenguliwa kwenye kesi kama hii, maana hili SAGA lilipoteza heshima ya TZ na watu wake duniani kabisa, mpaka ikafananishwa as a "Banana Republic"! Ndiyo haiwezekani zile Phd na Masters serikalini ziliweza kuruhusu uchafu ule...!
Confidentially of the recipients inaweza kuwa lifted kwa kutumia ombi kutoka FIU ya BOT only kama kuna mashaka kuwa fedha hizo ni dirty money na zimelipwa ili kuzi laundry. Au kama kuna mashaka fedha hizo zitatumika kufadhili ugaidi. Lakini fedha za JR ni fedha safi halali, zimetokana na biashara halali, kazigawa kihalali kwa watu aliowachagua.

Stanbic kamwe haiwezi kufanya ujinga kama wa Mkombozi Bank, recipients wote wa fedha za JR hawana makosa yoyote hata kama itotokea fedha za Escrow ni fedha za wizi, wala JR hana makosa kwa sababu amefanya biashara halali. Ilitokea kuna mwizi, then mwizi ni PAP. Kama PAP aliiba atatakiwa kuzirudisha na hapa ndipo mahakama ita lift the corporate veil ya PAP kuwajua Simba ni kina nani, then wamiliki hao watatakiwa kulipa fedha hizo.

Paskali.
 
Escrow ilianzishwa kwa madhumuni gani ?
Inavo tajwa ni kuwa Tanesco kwa mujibu wa mkataba na IPTL wanapaswa kulipa capacity charges za 7 billion kila mwezi.
Sasa kukawa na mgogoro hivyo wahusika wakaenda mahakamani.
Ila kwa sababu pesa inayo daiwa kila mwezi ni nyingi ikaamuliwa Tanesco walipe hizo pesa kuziweka account maalum. Ndio hilo dude Escrow account.
Hivyo hela ilowekwa mule ni capacity charges tu. Hakuna pesa ingine yoyote ile....
Kesi ikaisha ikaamriwa IPtl walipwe...wakalipwa. Lakini ikawa Iptl imeuzwa hivyo wakalipwa PAP...
Hivyo hapa hakuna hela ya umma .
Ni wenyewe tunajipiga kwenye mikataba.
Wa kukamata sio huyu singa wala tuge bali waloingia hii mikataba mibovu.
Tatizo letu tanzania huwa tunapenda sana kuwona wafanya biashara kuwa ndio matatizo kumbe chanzo ni wenyewe .
Sioni nafasi ya kushinda hii kesi ....unless kila aliehusika hata kwa kiduchu aingizwe mbivu mbichi ijulikane.
Kwa hiyo papa alitoa shi ngap kununua iptl maana naona hela ya escrow , ndo iliyotumika kununua Iptl , hii inawezakanaji kibiashara
 
Kwenye kuvutisha mpunga, wako waandishi 4 wa habari, walivutishwa M.40 kila mmoja, ila hakuna kosa lolotekumpa zawadi mtu yoyote kwa appreciation ya kazi yake nzuri, kwenye media kosa ni kutoa pesa ku influence reporting.
Hili la waandishi kulipwa, nimelizungumza sana hapa
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco ...
P.
si kwa wana habari tu. Hata wanamuziki wanafaa kupewe zawadi wanapofanya vizuri. Mfano mimi binafsi nilifanya jitihada kumtafuta mwanamuziki wa Morogoro aitwaye jina la kisanii Twenti Pasenti ili nimpe zawadi ya shilingi elfu kumi. Zawadi hiyo ilikuwa ni kwa ajiri kibao chake cha kuwaasa vijana kuacha kuibiana na kurudishana nyuma kimaendeleo. Kibao hicho kilikuwa na maneno ya busara na hekima kwa ajili ya vijana. Nilinunu albam iliyokuwa na wimbo huo, lakini nilitaka nihakikishe mwenyewe Twenti pasenti anafaidi jasho lake kwa kibao kile kutoka kwangu, Maana sikuamini wale wauzaji wa sidii zenye kibao hicho kama wanamfikishia mgao wake.

Wapi sikumpata Twenti Percent mpaka wa leo....kila ninayemuuliza anasema hajui halipo msanii huyu. Rongers S. anakazi kubwa sana.
====
Paskali mwazoni nilikuwa sielewi kabisa baadhi ya posts zako. Siku hizi nakusoma haswa.
 
Mkuu Nkese, BOT ni benki ya umma, fedha za escrow wakati zinahifadhiwa BOT zilikuwa ni fedha za umma, hivyo ni halali kwa CAG kukagua account ya escrow. Mgogoro ulipomalizika, zile fedha ndani ya account ya escrow zika change hands, toka kuwa fedha za umma na kugeuka fedha binafsi, zikatolewa BOT na kupewa wenye fedha zao!.

Tena Mkombozi Bank walifanya kosa kubwa kutoa siri za miamala ya wateja wao!, Stanbic waligoma!.
Paskali
Na ktk ripoti yake alisemaje-fedha ilikuwa/haikuwa ya umma?

Pia hata kama fedha iliwekwa kusubiri "wenyewe", kila aliyestahili alipata mgawo wake? E.g.kodi ya serikali.

Na vile vile kwa nini nguvu kubwa itumike kuzima " sakata hili?"

Na kuwa kwa kuangalia suala zima kwa jicho LA " mashaka" iweje watu waliopata mgawo ni wenye nafasi zenye maamuzi?
 
Back
Top Bottom