Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!


Kafanye uchunguzi mkuu,hicho kikao hakikuwa conclusive,hivyo hakiwezi kutumika kama authority ya kutoa pesa ya escrow.
And by the way,hata tukikifanya conclusive,hicho kikao kilifuata taratibu zinazotakiwa ili kutambulika kama kikao chenye status ya kuidhinisha jambo kubwa hivi?
Mnajitoa ufahamu bure lakini ukweli mnaujua,uko wazi tu.
Anyway,time will tell my friend.
 
Halafu una tabia ya kulike kila post,sitaki ulike post zangu hizi kuanzia leo,wewe mnafiki tu.
 

Pasco wewe si umesoma sheria? Nini maana ya "false pretendence"? Na je kampuni au mtu akifanya jambo under false pretendence linakuwa halali ati tu kwa sababu jambo hilo ni tangible? Inakuwaje raisi wa umma atoe maamuzi kuhusu pesa zisizokuwa za umma?
 

Nashukuru kwa pumba zako ila kama kawa nasoma kama hadithi ambazo ni za kupotezea muda.

Mungu analipa yote tunayotendewa watoto wake
 
Mkuu Tety, asante kwa hoja zako zamsingi sana!.

  1. VAT ambayo hajalipwa, inalipika!.
  2. Kwa mujibu wa mkataba wa Richmond, jukumu lakulipa kodi zote za serikali ni jukumu la Tanesco, walipaswa wafanye tax remitance kabla ya kudeposit fedha kwenye escrow!.
  3. Walikaa IPTL ikashusha viwango Tanesco bado wakagoma, hivyo kwa status quo ya wakati wa malipo yale yanafanyika Tanesco ilikuwa inadaiwa fedha nyingi kuliko hata zilizomo ndani ya escrow!.
  4. Mkataba wa mwanzo ulikuwa ni wa miaka 15!, baadae ukageuzwa 20!, baada ya miaka 10 ukaongezwa 20 tena!.
Kisheria kama makubaliano ya mwanzo yalikuwa mtambo wa aina fulani, wakatapeliwa kwa kuletewa mwingine, hapo ndipo mkataba ungepaswa kuvunjwa!.

Pasco
 

Mngese
 

Muhimu pia, iwapo fedha hizi sio za umma, kwanini role ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ilikuwa muhimu Katika kuidhinisha malipo yake? Kama sio fedha za umma, ni Kwanini ofisi ya rais wa jamhuri wa muungano imejihusisha na malipo ya fedha binafsi?
 
Halafu una tabia ya kulike kila post,sitaki ulike post zangu hizi kuanzia leo,wewe mnafiki tu.
Mkuu Juve, like zangu ni appreciation, kwa kuchangia thread yangu, kuna mada kibao humu, na majukwaa kibao, hivyo kitendo tuu cha kufungua thread yangu kusoma na kujibu, unastahili like yangu, the only way ya kufanya nisi like post zako, ni ukikutana na thread yoyote niliyoianzisha mimi, ipitie mbali!.

Tena utakuwa umenisaidia sana, kwa sababu its my wish nijibu kila post, sometimes nashindwa, hivyo zinapotokea chances za baadhi ya mijitu mijinga mijinga kupita mbali na threads zangu, hiyo kwangu ni fursa, za kuvuja kwa pakacha!,

Natanguliza shukrani!

Bye bye Juve!
:A S 103::A S 103:

Pasco.
 
Na sio hao tu, mshauri mkuu wa Rais kisheria (AG)amehusika sana.

Mtendaji mkuu katika wizara (katibu mkuu)ambaye ni mteule wa Rais ameshiriki.
Masaidizi mkuu wa Rais katika wizara anayeingia baraza la mawaziri(waziri) ameshiriki
Waziri wa fedha ameidhinisha malipo ya 'pesa binafsi''

CAG ameshirki kuchunguza pesa za 'watu binafsi''
Mkurugenzi PCCB ameshiriki uchunguzi wa pesa' binafsi''

Waziri mkuu ameelekeza uchunguzi ufanywe kwa ''pesa binafsi''

Mwanasheria mkuu alimkosa Kafulila kwa ngumi akitetea 'pesa binafsi''

Wote hao wanashiriki vipi kwa pesa za watu binafsi?
 
kuna mdau mmoja anaitwa Nkwesa Makambo, kazungumza vizuri sana, ni kama alikuwa na mawazo kama yangu, hata ningekuwa bungeni ningeuliza swali hili, wanaposema zile fedha hazikuwa za umma walimaanisha nini, maana zile fedha zilikuwa zina "hang" kwenye account ya escrow zilikuwa bado hazijalipwa kwa mtu yoyote, si IPTL wala Tanesco alikuwa anazimiliki kwa wakati huo, lakini TANESCO alikuwa ananafasi kubwa ya kuwa na right kwenye hizo fedha maana IPTL alikuwa bado hajatimiza obligation ya kwenye contract yao hivyo hakuwa entitled na hizo fedha mpaka pale atakapo fulfil obligation.

mfano IPTL ange breach contract asingeweza kuzidai, so hizo fedha zilikuwa ni subject to..., na kama zilikuwa ni za IPTL kwanini hazikulipwa kwenda kupitia kwenye account ya IPTL moja kwa mmoja?. naomba usiseme kuwa walikuwa hawaaminiani maana tayari walikwisha kuwa na dispute, kimsingi zile fedha ni mali ya umma, na hata kama zingekuwa ni za IPTL kwanini zigawiwe kiholela hivyo?, kama siyo kuwa kulikuwa na mchezo mchafu?,

kingine ni kuwa, issue ya IPTL siyo kuhusu fedha za kwenye acc ya escrow, maana kuna kukiukwa kwa kanuni za mikataba tokea 1994 kuwa hiyo kampuni haikuwa na sifa ya kushinda zabuni ya kusambaza umeme Tz, hapo napo kuna mchezo mchafu ulifanyika na bado watu wote waliohusika walitakiwa wawajibishwe, sijui kwanini hili halikutiliwa maanani na PAC, Kwahiyo mkuu Pasco jaribu kuliangalia hili jambo kwa jicho la tatu, usiwe biased kiasi hicho, kama una hoja thabiti kuwa zile fedha siyo za umma jaribu kuiwasilisha hapa.

mtazamo wangu kwa sasa, sisi wananchi tuchukue hatua, hizo drama za bungeni tuachane nazo, sisi wananchi ndo tuwe waamuzi wa mwisho, nadhani muafaka tutaupata na siyo kuwategemea hawa wanasiasa ambao wanakila aina ya ila kuweza kuchakachua.

Chagga King from Umbwe Klm.
 
angalia unaweza kujikuta unatumika kama karatasi ya chooni. Ahaa samahani!
 
Nimeogopa hapo kwenye rangi nyekundu. Kama sikosei waziri wa nishati wakati huo alikuwa Kikwete! sina uhakika naomba nisahihishwe!
 
Mkuu Mchambuzi, hakuna mahali popote Rais wa JMT, ametakiwa kuidhinisha malipo, bali hiyo ni initiative ya Gavana wa BOT, kujiridhisha jee awareness ya Mkuu wa Nchi kuhusu jambo hili!.

Pasco
 
...Pasco issue iliyokuwa raised na Zitto wakati anatoa taarifa bungeni, kuhusu kuwepo na "Government Guarantee" kwenye mkataba wa IPTL una maanisha nini, na what are the implications pia unaizungumziaje in connection with the statement kuwa TANESCO is an independent entity kama wao walivyosema (binafsi kisheria ninajua na nina uhakika kuwa TANESCO is a public company) and all undertakings zinakuwa financed na fedha za walipa kodi, pamoja na mapato inayopata kwenye mauzo ya umeme,

kwanini unatetea hizo siyo fedha zetu, why and why? Pasco kama kweli unazungumza kizalendo embu have a mercy on us aisee, ili uthibitishe ur not one of them.
 
Pasco yuko sahihi bila hayo masikitiko wala machozi ya mamba. Tulipoibiwa ni pale tulipochekea mkataba huo wa kiwizi (PPA) ukasainiwa kwa kisingizio cha kutuokoa na "giza refu". Pale ndipo wajanja walipotengeneza namna "halali" ya kuhamishia pesa ndefu ya umma kwenye mikoba yao "kihalali". ESCROW ndiye mjukuu wa "ujinga" wetu katika adha hii na wala sio tulipojikwaa. Hivyo, tusipoteze muda kulia na matokeo. Ndo tumeshaliwa hivyo. Tusome mambo na kudhibiti mapema kuanzia leo. Aidha, kuwapa watu "gerentii" ya kuwa madarakani milele na mtindo tuliouendekeza wa kushabikia "mtu kula mezani kwake" ndio matokeo yake haya.
 

Hata mgawo wa Ruge. alipendekeza waziri kwa kumwambia aseme anataka ngapi atapewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…