Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Mkuu Nkwesa Makambo, mpaka hapa uko right 100%, kwa feddha zilipokuwa ndani ya escrow ni "no mans land", "no ones money!". Si mali ya yeyote!, zikiisha kuwa sii mali ya yoyote maana yake sii mali ya IPTL wala sii mali ya serikali! mpaka muafaka upatikane!. Fedha hizo zilikuwa ni fedha za umma zikiwa Tanesco, baada ya kuwa deposited kwenye escrow, sio fedha za Tanesco tena!. Ripoti ya CAG ya ukaguzi wa kawaida wa hesabu za Tanesco, ulionyesha Tanesco wanaihesabu escrow account kama current asset yao, CAG akawaambia no!, kwa sababu hizo fedha wameisha zi expense!. Sasa hapa kwanza tukubaliane fedha za escrow sio fedha chafu!, hazikuibiwa kuingizwa escrow bali zimelipwa !. Jee unakijua ni nini kilichofanyika hadi hizo fedha to change hands from "no mans money to IPTL Money?!). Tanesco walikaa chini na IPTL, waka work out viwango vipya, japo bado vilikuwa juu na Tanesco kuendelea kuvilalamika, lakini walikubali pesa zitoke na bado wana deni kubwa kwa IPTL na kuandaa schedule ya namna ya kulipa. Hivyo fedha zote zilizokuwemo ndani ya escrow hazikutosha kumaliza deni inalodaiwa na mpaka leo, na mpka kesho Tanesco bado inadaiwa!. Hali hiyo ikapelekea fedha zote kwenye escrow kuwa ni mali ya IPTL!. Fedha za shares transfer sio sehemu ya fedha za escrow!, hizi ni fedha zilizopaswa kulipwa na singa singa from his own sorces na sio kosa la jinai, ni kosa la madai, deni lililokwepa linakuwa established linalipwa!.Pasco

Kafanye uchunguzi mkuu,hicho kikao hakikuwa conclusive,hivyo hakiwezi kutumika kama authority ya kutoa pesa ya escrow.
And by the way,hata tukikifanya conclusive,hicho kikao kilifuata taratibu zinazotakiwa ili kutambulika kama kikao chenye status ya kuidhinisha jambo kubwa hivi?
Mnajitoa ufahamu bure lakini ukweli mnaujua,uko wazi tu.
Anyway,time will tell my friend.
 
Halafu una tabia ya kulike kila post,sitaki ulike post zangu hizi kuanzia leo,wewe mnafiki tu.
 
Wanabodi,

Kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "An Enemy of the People" by Henrik Ibsen mnaweza kuniita mimi Pasco wa JF, kuwa ni "an enemy of the people!", Fedha za Escrow, Sio Fedha za Umma!, hizo Bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya Escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme!.

Inawezekana PAP amenunua kampuni hewa, amefanya utapeli kuinunua IPTL toka kwa wamiliki halali, hayo hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme kweli unaokuwa genereted na mitambo ya IPTL, ni umeme kweli na sio umeme hewa!, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!.

Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!.

Niko tayari to pay the price of expresing my opinion kuwa Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma!.

Pasco.

Pasco wewe si umesoma sheria? Nini maana ya "false pretendence"? Na je kampuni au mtu akifanya jambo under false pretendence linakuwa halali ati tu kwa sababu jambo hilo ni tangible? Inakuwaje raisi wa umma atoe maamuzi kuhusu pesa zisizokuwa za umma?
 
Wanabodi,

Kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "An Enemy of the People" by Henrik Ibsen mnaweza kuniita mimi Pasco wa JF, kuwa ni "an enemy of the people!", Fedha za Escrow, Sio Fedha za Umma!, hizo Bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya Escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme!.

Inawezekana PAP amenunua kampuni hewa, amefanya utapeli kuinunua IPTL toka kwa wamiliki halali, hayo hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme kweli unaokuwa genereted na mitambo ya IPTL, ni umeme kweli na sio umeme hewa!, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!.

Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!.

Niko tayari to pay the price of expresing my opinion kuwa Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma!.

Pasco.

Nashukuru kwa pumba zako ila kama kawa nasoma kama hadithi ambazo ni za kupotezea muda.

Mungu analipa yote tunayotendewa watoto wake
 
Pasco ninapenda namna unavyoweka hoja zako.Kiuchokozi kujua watanzania tumaufahamu wa kiasi gani au ni ushabiki tu.

Nitaweka kwa point kama ifuayavyo:

1.VAT inalipwa pale malipo halisi yanapolipwa kwa mteja aliyekidhi matakwa ya kukatwa VAT.

2.VAT ingekatwa na kuwa submitted TRA baada ya malipo halali kulipwa IPTL na TANESCO.Malipo ya IPTL yangekuwa pungufu ya VAT.Na hii VAT ndiyo malipo halali ya serikali kama yalivyolalamikiwa na TRA.

3.Malipo ya pili yangekuwa kuwa ya TANESCO baada ya kukokotoa malipo waliyokuwa wanapaswa kuwalipa IPTL baada ,na kubaki na tofauti kati ya kilichokuwapa kwenye ESCROW ACC na kiasi kilichotakiwa kulipwa IPTL toka miaka hiyo.

4.Yawezekana kwenye mkataba wa kwanza kabisa unaonyesha mitambo ya IPTL ingetakiwa kumilikiwa na TANESCO baada ya miaka hiyo 20 na hivyo kufanya TANESCO kuwa mmilikiki halali wa IPTL ambayo nadhani ndivuo ilivyokuwa leo tujiulize ni kwa nini Mitambo hii imeuzwa miaka miwili tu wakati TANESCO ikijiandaa kuipokea mitambo hii.je ilikuwa hoja ua nani kuiuza mitambo hii miala miwili tu kabla ua TANESCO kuirithi, na kama hili ni la kwemi basi pesa yote iliyokuwa kwenye account ya ESCROW ilikuwa mali halali ya TANESCO.
Mkuu Tety, asante kwa hoja zako zamsingi sana!.

  1. VAT ambayo hajalipwa, inalipika!.
  2. Kwa mujibu wa mkataba wa Richmond, jukumu lakulipa kodi zote za serikali ni jukumu la Tanesco, walipaswa wafanye tax remitance kabla ya kudeposit fedha kwenye escrow!.
  3. Walikaa IPTL ikashusha viwango Tanesco bado wakagoma, hivyo kwa status quo ya wakati wa malipo yale yanafanyika Tanesco ilikuwa inadaiwa fedha nyingi kuliko hata zilizomo ndani ya escrow!.
  4. Mkataba wa mwanzo ulikuwa ni wa miaka 15!, baadae ukageuzwa 20!, baada ya miaka 10 ukaongezwa 20 tena!.
Kisheria kama makubaliano ya mwanzo yalikuwa mtambo wa aina fulani, wakatapeliwa kwa kuletewa mwingine, hapo ndipo mkataba ungepaswa kuvunjwa!.

Pasco
 
Mkuu Mchambuzi, with due respect, tafsiri rasmi ya fedha za umma ni "public monies!"

Suala la umiliki wa account escrow ni kitu kimoja, na fedha zilizomo humo ndani ni jambo jingine!.
Namna ya kujua kama ni fedha za umma au sio za umma ni the time hizo fedha zinapochange hands toka umma kuwa private money?!.

Account ya escrow ni account ya ubia kati ya Tanesco na IPTL, hivyo wakati wote wa uhifadhi wa fedha hizo ndani ya account hiyo ya escrow, zilikuwa joint finances, na ile siku Tanesco aliporidhia fedha zilipwe IPTL, then fedha zile zili change hands from public money to private money!. Nahisi CAG, TRA na PCCB hawakuangalia mkataba wa IPTL, kodi zote zilipaswa kulipwa na Tanesco na sio IPTL!, kama Tanesco, ilitumbukiza hadi kodi humo kwenye escrow, then ni tatizo la Tanesco!, na kwa vile Tanesco ilikuwa na bado inadaiwa deni kubwa na IPTL, then, hiyo kodi iliyo achwa na Tanesco kwenye escrow, itakuwa dected kwenye next payments!. Kodi inaweza kulipwa wakati wowote!.

Mtu mwingine aliyepaswa kulipa kodi ni Singa singa wa PAP kwenye transfer kutoka Mechmar kwenda Pieper Link na kutoka Pieper Link kwenda PAP na hizi hazihusiani kabisa na pesa za Escrow!.

Pasco

Mngese
 
Hili swali nimemuuliza uzi mwingine, hakuwahi kulijibu.

Na kwa kuongezea, wapi AG Werema amepata uwezo wa kuwa mshauri wa kodi?

Tatu, ina maana pasco haamini CAG ? Sasa kama PAC wamefanya uhuni, uhuni huo si wameutoa katika taarifa ya CAG

Nne, pesa za binafsi zinatumikaje kwa viongozi wa umma, hadi hapo haoni tatizo

Tano, taarifa imeeleza mitambo ya low speed ndiyo ilihitajika, walileta isiyo katika kiwango hicho, hilo pasco hahisi =kuna tatizo kweli

Sita, kama ni pesa za binafasi, CAG, waziri, katibu mkuu wizara wanaingiliaje masuala binafsi?

Saba, jitihada za serikali kuzuia mjadala zililenga nini iwapo ilikuwa ni pesa binafasi.

Muhimu pia, iwapo fedha hizi sio za umma, kwanini role ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ilikuwa muhimu Katika kuidhinisha malipo yake? Kama sio fedha za umma, ni Kwanini ofisi ya rais wa jamhuri wa muungano imejihusisha na malipo ya fedha binafsi?
 
Halafu una tabia ya kulike kila post,sitaki ulike post zangu hizi kuanzia leo,wewe mnafiki tu.
Mkuu Juve, like zangu ni appreciation, kwa kuchangia thread yangu, kuna mada kibao humu, na majukwaa kibao, hivyo kitendo tuu cha kufungua thread yangu kusoma na kujibu, unastahili like yangu, the only way ya kufanya nisi like post zako, ni ukikutana na thread yoyote niliyoianzisha mimi, ipitie mbali!.

Tena utakuwa umenisaidia sana, kwa sababu its my wish nijibu kila post, sometimes nashindwa, hivyo zinapotokea chances za baadhi ya mijitu mijinga mijinga kupita mbali na threads zangu, hiyo kwangu ni fursa, za kuvuja kwa pakacha!,

Natanguliza shukrani!

Bye bye Juve!
:A S 103::A S 103:

Pasco.
 
Muhimu pia, iwapo fedha hizi sio za umma, kwanini role ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ilikuwa muhimu Katika kuidhinisha malipo yake? Kama sio fedha za umma, ni Kwanini ofisi ya rais wa jamhuri wa muungano imejihusisha na malipo ya fedha binafsi?
Na sio hao tu, mshauri mkuu wa Rais kisheria (AG)amehusika sana.

Mtendaji mkuu katika wizara (katibu mkuu)ambaye ni mteule wa Rais ameshiriki.
Masaidizi mkuu wa Rais katika wizara anayeingia baraza la mawaziri(waziri) ameshiriki
Waziri wa fedha ameidhinisha malipo ya 'pesa binafsi''

CAG ameshirki kuchunguza pesa za 'watu binafsi''
Mkurugenzi PCCB ameshiriki uchunguzi wa pesa' binafsi''

Waziri mkuu ameelekeza uchunguzi ufanywe kwa ''pesa binafsi''

Mwanasheria mkuu alimkosa Kafulila kwa ngumi akitetea 'pesa binafsi''

Wote hao wanashiriki vipi kwa pesa za watu binafsi?
 
kuna mdau mmoja anaitwa Nkwesa Makambo, kazungumza vizuri sana, ni kama alikuwa na mawazo kama yangu, hata ningekuwa bungeni ningeuliza swali hili, wanaposema zile fedha hazikuwa za umma walimaanisha nini, maana zile fedha zilikuwa zina "hang" kwenye account ya escrow zilikuwa bado hazijalipwa kwa mtu yoyote, si IPTL wala Tanesco alikuwa anazimiliki kwa wakati huo, lakini TANESCO alikuwa ananafasi kubwa ya kuwa na right kwenye hizo fedha maana IPTL alikuwa bado hajatimiza obligation ya kwenye contract yao hivyo hakuwa entitled na hizo fedha mpaka pale atakapo fulfil obligation.

mfano IPTL ange breach contract asingeweza kuzidai, so hizo fedha zilikuwa ni subject to..., na kama zilikuwa ni za IPTL kwanini hazikulipwa kwenda kupitia kwenye account ya IPTL moja kwa mmoja?. naomba usiseme kuwa walikuwa hawaaminiani maana tayari walikwisha kuwa na dispute, kimsingi zile fedha ni mali ya umma, na hata kama zingekuwa ni za IPTL kwanini zigawiwe kiholela hivyo?, kama siyo kuwa kulikuwa na mchezo mchafu?,

kingine ni kuwa, issue ya IPTL siyo kuhusu fedha za kwenye acc ya escrow, maana kuna kukiukwa kwa kanuni za mikataba tokea 1994 kuwa hiyo kampuni haikuwa na sifa ya kushinda zabuni ya kusambaza umeme Tz, hapo napo kuna mchezo mchafu ulifanyika na bado watu wote waliohusika walitakiwa wawajibishwe, sijui kwanini hili halikutiliwa maanani na PAC, Kwahiyo mkuu Pasco jaribu kuliangalia hili jambo kwa jicho la tatu, usiwe biased kiasi hicho, kama una hoja thabiti kuwa zile fedha siyo za umma jaribu kuiwasilisha hapa.

mtazamo wangu kwa sasa, sisi wananchi tuchukue hatua, hizo drama za bungeni tuachane nazo, sisi wananchi ndo tuwe waamuzi wa mwisho, nadhani muafaka tutaupata na siyo kuwategemea hawa wanasiasa ambao wanakila aina ya ila kuweza kuchakachua.

Chagga King from Umbwe Klm.
 
wanabodi,

kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "an enemy of the people" by henrik ibsen mnaweza kuniita mimi pasco wa jf, kuwa ni "an enemy of the people!", fedha za escrow, sio fedha za umma!, hizo bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme!.

Inawezekana pap amenunua kampuni hewa, amefanya utapeli kuinunua iptl toka kwa wamiliki halali, hayo hayatuhusu, bali malipo ya tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya iptl ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme kweli unaokuwa genereted na mitambo ya iptl, ni umeme kweli na sio umeme hewa!, na imeelezwa kuwa tanesco bado inadaiwa!.

Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!.

Niko tayari to pay the price of expresing my opinion kuwa nimesikitishwa!, huzunishwa!, na kufadhaishwa na uongo wa kamati ya pac!-escrow sio fedha za umma!.

Pasco.
angalia unaweza kujikuta unatumika kama karatasi ya chooni. Ahaa samahani!
 
kuna mdau mmoja anaitwa Nkwesa Makambo, kazungumza vizuri sana, ni kama alikuwa na mawazo kama yangu, hata ningekuwa bungeni ningeuliza swali hili, wanaposema zile fedha hazikuwa za umma walimaanisha nini, maana zile fedha zilikuwa zina "hang" kwenye account ya escrow zilikuwa bado hazijalipwa kwa mtu yoyote, si IPTL wala Tanesco alikuwa anazimiliki kwa wakati huo, lakini TANESCO alikuwa ananafasi kubwa ya kuwa na right kwenye hizo fedha maana IPTL alikuwa bado hajatimiza obligation ya kwenye contract yao hivyo hakuwa entitled na hizo fedha mpaka pale atakapo fulfil obligation.

mfano IPTL ange breach contract asingeweza kuzidai, so hizo fedha zilikuwa ni subject to..., na kama zilikuwa ni za IPTL kwanini hazikulipwa kwenda kupitia kwenye account ya IPTL moja kwa mmoja?. naomba usiseme kuwa walikuwa hawaaminiani maana tayari walikwisha kuwa na dispute, kimsingi zile fedha ni mali ya umma, na hata kama zingekuwa ni za IPTL kwanini zigawiwe kiholela hivyo?, kama siyo kuwa kulikuwa na mchezo mchafu?,

kingine ni kuwa, issue ya IPTL siyo kuhusu fedha za kwenye acc ya escrow, maana kuna kukiukwa kwa kanuni za mikataba tokea 1994 kuwa hiyo kampuni haikuwa na sifa ya kushinda zabuni ya kusambaza umeme Tz, hapo napo kuna mchezo mchafu ulifanyika na bado watu wote waliohusika walitakiwa wawajibishwe, sijui kwanini hili halikutiliwa maanani na PAC, Kwahiyo mkuu Pasco jaribu kuliangalia hili jambo kwa jicho la tatu, usiwe biased kiasi hicho, kama una hoja thabiti kuwa zile fedha siyo za umma jaribu kuiwasilisha hapa.

mtazamo wangu kwa sasa, sisi wananchi tuchukue hatua, hizo drama za bungeni tuachane nazo, sisi wananchi ndo tuwe waamuzi wa mwisho, nadhani muafaka tutaupata na siyo kuwategemea hawa wanasiasa ambao wanakila aina ya ila kuweza kuchakachua.

Chagga King from Umbwe Klm.
Nimeogopa hapo kwenye rangi nyekundu. Kama sikosei waziri wa nishati wakati huo alikuwa Kikwete! sina uhakika naomba nisahihishwe!
 
Muhimu pia, iwapo fedha hizi sio za umma, kwanini role ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ilikuwa muhimu Katika kuidhinisha malipo yake? Kama sio fedha za umma, ni Kwanini ofisi ya rais wa jamhuri wa muungano imejihusisha na malipo ya fedha binafsi?
Mkuu Mchambuzi, hakuna mahali popote Rais wa JMT, ametakiwa kuidhinisha malipo, bali hiyo ni initiative ya Gavana wa BOT, kujiridhisha jee awareness ya Mkuu wa Nchi kuhusu jambo hili!.

Pasco
 
...Pasco issue iliyokuwa raised na Zitto wakati anatoa taarifa bungeni, kuhusu kuwepo na "Government Guarantee" kwenye mkataba wa IPTL una maanisha nini, na what are the implications pia unaizungumziaje in connection with the statement kuwa TANESCO is an independent entity kama wao walivyosema (binafsi kisheria ninajua na nina uhakika kuwa TANESCO is a public company) and all undertakings zinakuwa financed na fedha za walipa kodi, pamoja na mapato inayopata kwenye mauzo ya umeme,

kwanini unatetea hizo siyo fedha zetu, why and why? Pasco kama kweli unazungumza kizalendo embu have a mercy on us aisee, ili uthibitishe ur not one of them.
 
Pasco yuko sahihi bila hayo masikitiko wala machozi ya mamba. Tulipoibiwa ni pale tulipochekea mkataba huo wa kiwizi (PPA) ukasainiwa kwa kisingizio cha kutuokoa na "giza refu". Pale ndipo wajanja walipotengeneza namna "halali" ya kuhamishia pesa ndefu ya umma kwenye mikoba yao "kihalali". ESCROW ndiye mjukuu wa "ujinga" wetu katika adha hii na wala sio tulipojikwaa. Hivyo, tusipoteze muda kulia na matokeo. Ndo tumeshaliwa hivyo. Tusome mambo na kudhibiti mapema kuanzia leo. Aidha, kuwapa watu "gerentii" ya kuwa madarakani milele na mtindo tuliouendekeza wa kushabikia "mtu kula mezani kwake" ndio matokeo yake haya.
 
Na sio hao tu, mshauri mkuu wa Rais kisheria (AG)amehusika sana.

Mtendaji mkuu katika wizara (katibu mkuu)ambaye ni mteule wa Rais ameshiriki.
Masaidizi mkuu wa Rais katika wizara anayeingia baraza la mawaziri(waziri) ameshiriki
Waziri wa fedha ameidhinisha malipo ya 'pesa binafsi''

CAG ameshirki kuchunguza pesa za 'watu binafsi''
Mkurugenzi PCCB ameshiriki uchunguzi wa pesa' binafsi''

Waziri mkuu ameelekeza uchunguzi ufanywe kwa ''pesa binafsi''

Mwanasheria mkuu alimkosa Kafulila kwa ngumi akitetea 'pesa binafsi''

Wote hao wanashiriki vipi kwa pesa za watu binafsi?

Hata mgawo wa Ruge. alipendekeza waziri kwa kumwambia aseme anataka ngapi atapewa!
 
Back
Top Bottom