Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Kama pesa ni hao akina seth kwann wakuu wa serikali walihusika??! Pesa kwa mfano za Rostam au Menngi au hata zako wewe Pasco huwa zinakaguliwa na Mkaguzi wa CAG???! Jamani suala hili msilichukulie poa...hizi hela ni zetu hata kama sio zote..lakini kwann huu mdudu unaitwa IPTL umedumu hivi kuna nini nyuma yake??
 
CCM Wanatuharibia nchi yetu kikundi kidogo kwa kutumia wajinga wengi wanatuangamiza wenye IQ na tamaa za mafanikio pesa ile mgao wake ni kila MTZ angepata 8,000 hoja kama hii c ya kutetewa Fedha za escrow mgao hadi Askofu Kilaini Jaji Waziri Tibaijuka Ngeleja Chenge nk.wanapataje mgao huu wa escrow bora mgao ungewapitia PAP VIP TANESCO na IPTL Waliopata mgao ndo waliocheza mchezo huu kwahiyo wamerudishiwa faida yao ya wizi Nashukuru nchi wahisani kwa kusimamisha misaada na waendelee hivyohivyo cc tuendelee na wizi wetu. Serikali ihukumiwe kwa uzembe kuanzia Rais na Serikali yake yote na ikaribisha Burkinafaso.
 
Pasco, unaomba tuelewashane wakati tayari umeshatoa hitimisho!! Tangu mwanzo hata kabla ya PAC kuwasilisha kamati msimamo wa Kafulila umekuwa kwamba ndani ya akaunti ya ESCROW kuna fedha ya TANESCO (umma). Hakuna aliyewahi kusema kwamba pesa yote ni ya umma. Kumbuka kwamba hela yote imetokana na shauri mahakamani. Badala ya kuilipa IPTL pesa ilikuwa inakwenda kwenye hii akaunti hadi shauri lingeamuliwa ili kujua kiasi halisi ambacho IPTL walistahili. Mahakama ikaamua kwamba ni kweli kwamba TANESCO walikuwa wanalipa pesa nyingi zaidi kuliko uhalisia. Sisi tukapewa nafasi ya kukokotoa mahesabu ili tuchukue cha kwetu na kinachobaki kiende IPTL. Tumeshindwa au tusema tumekaa kufanya hivyo kwa sababu hiyo pesa tulishaipiga, haipo. Ndio hizo akina Ruge wamezigawa kama njugu. Sasa utasemaje kwamba hakuna pesa yetu pale?

Hata kitendo tu cha akina Ruge kugawa hela ovyo kinakwambia kwamba ile haikuwa pesa yao. Katika hali ya kawaida kama ile ingekuwa pesa yao walioipata kihalali ingewezekanaje waigawe ovyo namna hiyo? Matarajiri wa Tanzania ni Rostam, Bakhresa na Mengi, mbona hatujasikia wakigawana fedha bararani namni ile? Na kwa nini waliogawiwa wote ni wanasiasa, viongozi na watu wenye mamlaka fulani? Kwa nini Ruge hakwenda kugawa hizi fedha kwa wanafunzi wetu waliokosa mikopo kama kweli ana roho nzuri kiasi hicho?

Haya, wewe unaona ni sawa watu kugawana pesa kama maembe kama walivyofanya? Nchi za wenzetu hata kuingia na dola 10,0000 wanakuzuia lazima utoe maelezo ya kutosha na vielelezo kibao. Hapa kwetu watu wanagawana pesa kwenye rambo wewe unaona ni sawa hiyo? Pasco please!!

Sawa kabisa;
mimi suala langu ambalo linaniumiza kichwa ni hili la kuwa pesa ya umma au pesa ya IPTL, kwa sababu ilikuwa siyo ya umma ati haina haja ya kuuliza. Pasco anasahahu kuwa Professor Muhongo hakanushi kuwa alipata pesa, ila tu anadai zile pesa siyo za umma. Mimi suala hapa ni kuwa hivi Tanzania imepoteza ethics kiasi hiki? If we steal this way is ok but that way not!!!! Where is the logic then, ethics. Infact sioni kuwa na imani na kuongozwa na mtu ambaye hakili wizi. Muhongo has to come clean and explain if he really got this money. Tibaijuka at least said, she got.

Kama unakubali kuwa hawa watu waligawana pesa basi ilikuwa ni rushwa!!! What kind of a thinking we need!!
 
Pasco twende taratibu.Ulikuwepo ubishani wa capacity charges,Baraza la Usuluhishi la kimataifa likakubaliana na Tanesco kuwa ni kweli walikuwa wanakuwa charged zaidi.Bahati mbaya wewe ni mwanasheria,Escrow account hufunguliwa pale tu panapokuwa na kukinzana kwa maslahi ya pande mbili.Mpaka sasa,suala la fedha hizi zilizoko kwenye Escrow akaunti ufumbuzi wake ulikuwa haujapatikana.Ni dhahiri kuwa,kwa mujibu wa Tanesco wenyewe,fisadi RUGEMALIRA,na baraza la usuluhishi wa kimataifa Taneso ulikuwa inaibiwa.Sasa swali linakuja,pesa zipi Tanesco ilikuwa inaibiwa,si ndo hizi hizi ambazo ziko kwenye Escrow account na bahati mbaya viongozi wa nchi hii wametumika kuziruhusu?

Pengine kwa mujibu wa report you are trying to swim in academic reservoir to interpret the PAC report kwa mujibu wa vionjo vyako,ila ukweli utabaki kuwa Ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tety, asante kwa hoja zako zamsingi sana!.

  1. VAT ambayo hajalipwa, inalipika!.
  2. Kwa mujibu wa mkataba wa Richmond, jukumu lakulipa kodi zote za serikali ni jukumu la Tanesco, walipaswa wafanye tax remitance kabla ya kudeposit fedha kwenye escrow!.
  3. Walikaa IPTL ikashusha viwango Tanesco bado wakagoma, hivyo kwa status quo ya wakati wa malipo yale yanafanyika Tanesco ilikuwa inadaiwa fedha nyingi kuliko hata zilizomo ndani ya escrow!.
  4. Mkataba wa mwanzo ulikuwa ni wa miaka 15!, baadae ukageuzwa 20!, baada ya miaka 10 ukaongezwa 20 tena!.
Kisheria kama makubaliano ya mwanzo yalikuwa mtambo wa aina fulani, wakatapeliwa kwa kuletewa mwingine, hapo ndipo mkataba ungepaswa kuvunjwa!.

Pasco

Basi mpaka hapo Pasco tukubaliane kabisa kwamba hatuna viongozi tunamatapeli ambao wanatumia matatizo ya nchi kujipatia fedha bila kutumia jasho.

Hawa ndiyo wanahitajika kujinyonga wenyewe.Shida ni moja tuanze na yupi?Tembo Mkubwa,Tembo wakati au watoto wa Tembo?Hapo ndipo tulipo kwa sasa,ila kupigwa tumepigwa sana tu hilo halina mjadala.
 
Mkuu Tety, asante kwa hoja zako zamsingi sana!.

  1. VAT ambayo hajalipwa, inalipika!.
  2. Kwa mujibu wa mkataba wa Richmond, jukumu lakulipa kodi zote za serikali ni jukumu la Tanesco, walipaswa wafanye tax remitance kabla ya kudeposit fedha kwenye escrow!.
  3. Walikaa IPTL ikashusha viwango Tanesco bado wakagoma, hivyo kwa status quo ya wakati wa malipo yale yanafanyika Tanesco ilikuwa inadaiwa fedha nyingi kuliko hata zilizomo ndani ya escrow!.
  4. Mkataba wa mwanzo ulikuwa ni wa miaka 15!, baadae ukageuzwa 20!, baada ya miaka 10 ukaongezwa 20 tena!.
Kisheria kama makubaliano ya mwanzo yalikuwa mtambo wa aina fulani, wakatapeliwa kwa kuletewa mwingine, hapo ndipo mkataba ungepaswa kuvunjwa!.

Pasco

Hata JR ni tapeli na amejua alichokuwa anakifanya,yawezekana kabisa hata SInga Singa ambaye ni tapeli la dunia alijua anatakiwa kufanya nini ili pesa za wajinga zitoke.Na kwa vile Tembo mkubwa hajali kwa sasa sababu anamaliza muda wake na ndiyo maana uamuzi wa Tembo Mkubwa unatia ukakaksi.
 
Pimbi wewe ile report co ya PAC.na wala cpaswi kukuelimisha maana ukweli unaujua ila kwa kuwa wewe ni boyaacha ufate mawimbi
 
Pasco wa JF
Hata Pilato alimuuliza YESU "Ukweli ni Kitu Gani"..Yesu alikaa kimya. Maana yake ni kuwa,Ukweli na Uongo its a subjective. Hivyo Wewe Pasco endelea kuamini Ukweli wako.
Hongera.
julius kaisari acha kumchezea ama kumtumia Yesu kujustify unachokitaka!
Tuambie kwenye kitabu gani cha biblia, sura gani na mstari wa ngapi haya uliyoyanukuu hapa kat ya Yesu na Pilato walipata kuulizana?????? Swali hilo kama Yesu angeulizwa angeshindwa kumjibu mtoto mdogo sana huyo Pilato kwa Yesu
 
Last edited by a moderator:
Tanesco waliwahi kuwa na mgogoro na IPTL kuhusu overcharged?suluhisho lilipatikana lini?Kabla au baada ya fedha kuchotwa escrow account?kwa nini?Nini Suluhu iliyotolewa kuhusu mgogoro wa overcharge ya capacity charge?Pasco naomba mimi na wewe tuanzie hapa,tutaendelea baada ya majibu yako!
 
Nashukuru kwa pumba zako ila kama kawa nasoma kama hadithi ambazo ni za kupotezea muda.

Mungu analipa yote tunayotendewa watoto wake

Raia na wewe pia ni mtoto wa Mungu wenu kama ilivokuwa kwa YEssu? Kwa hiyo wewe ni pacha ama kaka yake na Yessu?
 
NCHII HII SIJUI TUMEKUWAJE JAMANI, YAANI PESA ZA TANESCO ZINAZOTOKANANA NA MAKUSANYO YA KODI ZETU SIYO ZETU TENA??

PESA ZA MTU BINAFSI WAZIRI MKUU, RAISI, WAZIRI WA FEDHA et al ANAJULISHWA ILI IWEJE??

FEDHA ZA TANESCO ZINAZOTOKANA NA MAKUSANYO NA KODI ZENU????
damn.. mnatozwa umeme ambao ----------- toka IPTL, mbona hilo la energy charges and capacity charges HAMLISEMI??? katika kipindi choote cha DISPUTE, tanesco ilikuwa inaendelea kuchukua umeme toka IPTL na watanzania walikuwa wanautumia. badala ya kulipa moja kwa moja kwa IPTL, fedha hizo zilikuwa zinapelekwa benk kuu kuhifadhiwa katika account ya ESCROW. how come fedha hizo zirudi tena na kuwa ni za tanesco!!!!!????
KUHUSU SWALA LA MWANASHERIA MKUU KUSHUGHULIKA NA FEDHA HIZO, hizo i taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria. kumbuka tu kuwa fedha hizo zilikuwa zimehifadhiwa BOT ambayo ni benki kuu ya serikali. ulitegemea mchakato wake uendeje bila kuhusika taasisi za kisheria na kifedha za serikali???
tusubiri tuone
 
Kweli wewe sasa unajifedhehesha sasa, kama haikuwa ya kwetu kwanini Ikulu ilihusika? CAG anahusikaje kwenda kukagua account ya mtu binafsi?? Mmmgh
Dah et pesa si ya uma na ripoti ya CAG wanaikubali sasa CAG akaguaje pesa ambazo si za uma? kwa hili wanajichanganya, Lusinde anawatuhumu Mwanasheria mkuu kwa sababu anazitambua kuwa ni pesa za uma kasema mwenyewe jana japo katukana sana ndo point niliyoipata kutoka kwake ila anaogopa kuwawajibisha akidai kuwajibika si jambo dogo
 
Kama si za umma kwanini mwanasheria mkuu wa serikali-werema ndiye alikuwa akitoa maelekezo hadi kwa gaavana nduru na zaidi ya yote alihitaji hata maamuzi ya rais ili hizo pesa zitoke,

hizo pesa za tanesco zilipowekwa katika account zilikuwa za nani? Tanesco wanatengeneza pesa?

Pesa binafsi raisi anaingiaje, au pinda anaingiaje mkuu? hadi ahusike kukopiwa barua??

Kujiridhisha kusijekuwa Na liability kwa serikali in the future sababu ac yenyewe imetokana Na dispute pia
 
  1. unaomba tuelewashane wakati tayari umeshatoa hitimisho!!
  2. Tangu mwanzo hata kabla ya PAC kuwasilisha kamati msimamo wa Kafulila umekuwa kwamba ndani ya akaunti ya ESCROW kuna fedha ya TANESCO (umma). Hakuna aliyewahi kusema kwamba pesa yote ni ya umma. Kumbuka kwamba hela yote imetokana na shauri mahakamani. Badala ya kuilipa IPTL pesa ilikuwa inakwenda kwenye hii akaunti hadi shauri lingeamuliwa ili kujua kiasi halisi ambacho IPTL walistahili.
  3. Mahakama ikaamua kwamba ni kweli kwamba TANESCO walikuwa wanalipa pesa nyingi zaidi kuliko uhalisia.
  4. Sisi tukapewa nafasi ya kukokotoa mahesabu ili tuchukue cha kwetu na kinachobaki kiende IPTL.
  5. Tumeshindwa au tusema tumekaa kufanya hivyo kwa sababu hiyo pesa tulishaipiga, haipo. Ndio hizo akina Ruge wamezigawa kama njugu. Sasa utasemaje kwamba hakuna pesa yetu pale?.
  6. Hata kitendo tu cha akina Ruge kugawa hela ovyo kinakwambia kwamba ile haikuwa pesa yao.
  7. Katika hali ya kawaida kama ile ingekuwa pesa yao walioipata kihalali ingewezekanaje waigawe ovyo namna hiyo?
  8. Matarajiri wa Tanzania ni Rostam, Bakhresa na Mengi, mbona hatujasikia wakigawana fedha bararani namni ile?.
  9. Na kwa nini waliogawiwa wote ni wanasiasa, viongozi na watu wenye mamlaka fulani?
  10. Kwa nini Ruge hakwenda kugawa hizi fedha kwa wanafunzi wetu waliokosa mikopo kama kweli ana roho nzuri kiasi hicho?.
  11. Haya, wewe unaona ni sawa watu kugawana pesa kama maembe kama walivyofanya?
  12. Nchi za wenzetu hata kuingia na dola 10,0000 wanakuzuia lazima utoe maelezo ya kutosha na vielelezo kibao. Hapa kwetu watu wanagawana pesa kwenye rambo wewe unaona ni sawa hiyo? Pasco please!!
Mkuu Mwalimu, Prof. Kitila, kwanza hongera kupata uprofesa, maana hatujakutana humu jukwaani kwenye thread yangu yoyote tangu umekuwa prof, bado nimekuzoea zaidi kama Dr. Pili nimefarijika sana, kunitembelea kwenye uzi huu, its an honour to me and to my thread, kama nilivyofarijika nilipo tembelewa na Mchambuzi na Nguruvi 3.

Kwenye posti yako ume raise hoja 12 za msingi, mwanafunzi unapoulizwa maswali na mwalimu, unaamini kabisa mwalimu anajua, ila anakuuliza tuu ili kuujua ufahamu wako, inapotokea mwalimu anaomba kueleweshwa na mwanafunzi, then mwanafunzi huyo anakuwa more than gladi kumuelewesha mwalimu, na hapa mwanafunzi atajisikia sasa yeye ndio mwalimu, na mwalimu ndio mwanafunzi wake, hivyo Mwalimu Kitila, karibu katika darasa langu.

  1. Mimi ni mkweli daima hivyo mara kadhaa huanzia kwa kuweka "the end" na kisha ndipo na "justify the means". The end product hapa "pesa ni za nani?!", naanza kwenye kumtaja mwenye pesa ndipo tuje kuhalalisha kwa nini sio pesa za umma!. Kuna hoja za mijadala, na kuna hoja sio za mijadala ni straight conclusive!. Ingekuwa hoja yangu ni mjadala, ningeiliza Jee Fedha za Escrow ni za Umma?, ili watu walete michango, mwisho tufikie hitimisho!. Hapa kuna ukweli na uongo!, kuna kumaninishana kwa kudanganyana kuwa fedha za umma zimeibiwa!, zimechotwa, zimekapuliwa, hivyo wananchi wamehaminika, wakati ukweli ni kuwa fedha hazikuibiwa zimelipwa!. Mtindo wangu wa kutoa conclusiwe sikuanza leo, tulupoanza tuu huu mchakato wa katiba, nilisema tutapata "bora katiba". Kabla kura hazijapigwa kuipitisha nilisema humu "kura zisipotosha, zitatosheshwa!". Sasa watu wanapigia chapuo kura za hapana, nikasema wazi huko ni kujifurahisha kwa sababu kura za ndio "zitatosheshwa!", na kwenye siasa pia mara kibao nimeweka conclusive humu hata "2015 ni CCM tena!" kwa sababu hatuna any serious opposition, Ukawa mimi nauita ni just a "married of convenience!", conveniences zikiisha kila mtu atashika njia yake!. Escrow sio fedha za umma!.
  2. Hapa tuko wote, ndani pesa za account ya escrow zimechange formas mara tatu, au zime change hands mara tatu, kuna mtu anaitwa depositor, ambaye yeye ni Tanesco, fedha zilipokuwa mikononi mwa Tanesco, ni fedha za umma, kitendo cha kuzitoa ndani ya account ya Tanesco kuzi deposit kwenye escrow, kitendo cha depositing, kumezichange form hizi fedha from kuwa pesa za umma, into pesa za depository, na zimechange hands from mikono ya Tanesco to mikono ya depositor ambaye yeye ni custodian tuu wa fedha hizo hadi mgogoro utakapokwisha!, hivyo wakati fedha zikiwa kwenye safe custody ya custodian, fedha zile sii za umma wala sii za binafsi, some zingeweza kuwa za umma na kurudishwa Tanesco, some zingeweza kuwa za IPTL with a unique options ya possibility with "uncertainty" that "only some" "could" be Tanesco's, but with definite that some are IPTL's with possibility ya all kuwa ni za IPTL!. Unakijua ni nini kilichotokea kuhusu madai ya Tanesco na ni nini kilikubalika?!. Tanesco wali give in, na kukubali wanadaiwa more than that na wakaweka schedule of repayment na ndipo Tanesco waka authorise pesa zote zilipwe kwa IPTL!, and that is when all the money zili change form kutoka kuwa fedha za wote na kugeuka fedha za binafsi, and during withdrawer by the time fedha zinalipwa IPTL zilikuwa sio fedha za umma!.
  3. Ni kweli Tanesco ilikuwa overcharged hugely hivyo tulikuwa tunaibiwa!, ila wizi wenyewe ni kwa mujibu wa mkataba na tulikubali, kama tulivyokubali kununua radar, ndege ya rais, vifaa vya kijeshi na sasa bomba la gesi na mikataba ya gesi, nenda kanisome hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ...Tetesi: Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ni Kiini Macho!. Hivyo kama ni kuwa overcharged, kila siku tunakuwa overcharged, overpriced, na huge kick backs!.
  4. Nashukuru kuwa kumbe unajua tulipewa hii nafasi jee unajua tuliitumiaje?!. Hii ndio conversion process ya kuachia fedha za umma zilizoibiwa na kugeuka fedha binafsi!.
  5. Hatukushindwa!, this is where the deal is!, PCCB ni nothing!, Hosea is nothing!, kitu kinachoitwa usalama wa Taifa is nothing!, tangu mwanzo IPTL ni rushwa mwanzo mwisho, what did we do?!. Bodi ya Tanesco ilipata "ganzi!" ya ajabu!, wakaridhia kwa maandishi pesa zote ni za IPTL!. Ruge na Singasinga ni wapiga dili, kama pesa zilikuwa zetu, then kikulacho kii nguoni mwetu!, tusitafute mchawi!, wala tusimbebeshe msalaba mtoto wa Mkulima, wezi wetu tunawajua na ni wale wale toka Richmond, Dowans hadi Simbioni!. Tungekuwa na akili laiti mgelijua huyo Simba mwenye 50% ya PAP ndipo angalau mngenielewa!.
  6. "Mwenye kisu kikali ndiye anaekula nyama!", "fimbo iliyoko mkononi ndiyo uiwayo nyoka!", "the end justify the means!", "Aliyeshika usukani wa gari ndiye dereva" regardless gari ni la nani!, hivyo as long as pesa iko mikononi mwa JR as private money, what he does with his monies!, is non of our businesses!.
  7. Private money is none of our business!.
  8. Kumbe sasa tatizo ni kugawa?!, Ukimuondoa Bakhresa, please don't talk of Mengi and Rostam, kwao this is "missed opportunity!", masking JR akajivutia na kujinyamazia, haya yote yasinge fumka!. Siku zote wahindi wanapiga dili hizi na kujituliza tuli!, lakini masikini wakipata.... Kuna DCP walipiga wahindi watupu wakatulia haikubumburuka!, EPA wahindi walikuwa wanaipiga long time, huku wametulia, Waswahili walipoingia tuu, wanasafiri 1st class, wananunua Vogue custom made kutoka UK, wanasafirisha kwa air cargo, gari zinafika zina kuwa cleared by cash on the spot!, mtaani mbona tulikomaje?!, si ndio dili ikabumbuluka!, wangejinyamazia tuu kama walivyo wahindi yote haya yasingetokea!.
  9. As long as sio hela ya umma, haijalishi nani amegaiwa na kwa huduma gani, ndio maana nikasema PCCB is nothing!, mnaangalia waliogaiwa pesa, haya ni matokeo tuu!, mnaacha kuangalia chanzo cha jinamizi hili la IPTL na kila kitu kiko wazi!, Rutabanzibwa alikataa hongo ya dola 200 na akahamishwa!, unamjua waziri wake alikuwa nani?, kama KM alimegewa dola laki mbili, jee aliyekuwa waziri alipewa ngapi?, unamjua ni nani?. Pesa zikiisha kuwa zako, you are free kuzigawa utakavyo bila kuvunja sheria yoyote!. Hakuna sheria inayokataza kugawa pesa wala jinai yoyote kupokea pesa yoyote kwa kazi yoyote au hata bila kazi yoyote!. Hata mimi kuna wakati "huwapitia wale" na kukubaliana bei, then nikifika huko, ninachange mind, lakini bado nalipa mtu bila kufanya chochote, its my money!.
  10. When the money is yours, you are free to use it as you please!, kwa winging umasikini ni laana, hivyo badala ya kuwagawia masking unamuomba Mungu, masking wore bora wajifie tuu na umasikini wao, na kumfutilishia Mungu kuwa mwenye nacho, ataongezewa!, asiye nacho atanyang'anywa hata kidogo alichonacho!, mzee wa vijisenti, kapewa katiba, ndiye mwenyekiti wa kamati ya bajeji na ndie mshauri wa JR wa mambo ya kisheria na umeona consultancy fee yake!.
  11. Yes ni saws kabisa na amini usiamini, hata mimi Pasco wa jf, nikiwa nazo, huwa nagawa!, tofauti ni kiwango, kwa uwezo wangu huwa nagawa ten ten, jelo jelo hadi buku buku!, kila nikienda bush, nahakikisha nina kama just 1.M tangu bank naiomba in small denominations, nikitua bush!, kijiji kizima kinajua leo mtoto wa mama fulani ameingia kijijini, kuanzia pombe hadi hizo ten ten, jeero jero na buku buku, its my money, I do with it what it pleases me!. Kwenye ule mgao kuna kick backs, kuna asante, kuna just sadakalawe kuwa "ninazo" kuna genuine charity na kuna sadaka!.
  12. Sio nchi za wenzetu hata sisi tunayo FIU pale BOT, miala yote ya more than 10.m lazima taarifa ziende FIU ndio maana siku hizi hakuna kutoa malipo more than that bila kupitia BOT, the only exception ni same bank transactions ndio maana recipients wote walilazimishwa lazima wafungue account the same bank!. Nawaombeni sana msibabaishwe na huto tujisenti kwenye account za Mkombozi, the real transactions zimefanywa kwenye account yake iliyoko nchi Uholanzi, naamini "wanene" wamepewa asante zao zimehifadhiwa kule "Credit Sussie" transactions zinafanywa kwa "codes" only!, hata bank manageger, hawezi kujua jina la account holders!.
Natumaini mwalimu utakuwa umenielewa!.

Ni wako mwanafunzi mtiifu
Pasco wa jf!.
 
Basi mpaka hapo Pasco tukubaliane kabisa kwamba hatuna viongozi tunamatapeli ambao wanatumia matatizo ya nchi kujipatia fedha bila kutumia jasho.

Hawa ndiyo wanahitajika kujinyonga wenyewe.Shida ni moja tuanze na yupi?Tembo Mkubwa,Tembo wakati au watoto wa Tembo?Hapo ndipo tulipo kwa sasa,ila kupigwa tumepigwa sana tu hilo halina mjadala.
Mkuu Tetty, hili wewe ndio unalijua leo?!. Unamjua mtu aliyeileta IPTL?!, escrow ni matokeo tuu, lets get back to the basics tutibu chanzo!.

Pasco
 
Mkuu Tetty, hili wewe ndio unalijua leo?!. Unamjua mtu aliyeileta IPTL?!, escrow ni matokeo tuu, lets get back to the basics tutibu chanzo!.

Pasco

Pasco,hivi wajua nyie mliosomea SHERIA ni wabaya sana?Je,walijua hilo?AG na PM hawa wote wananyazifa kubwa sana ni washauri AZIZI wa Mkulu,je inamaana wanasheria hawa wawili walishindwa kumshauri Mkulu wa Kaya?

Je,ni kwanini hawa wanasheria wawili wanajua masharti ya kuwajibika lakini hawakutaka kuajibika mapema mpaka wameamua kumwaga mboga sababu CAG na TAKUKURU wameamua kumwaga UGALI!

Sababu kubwa wametaka kuuelezea ulimwengu tatizo siyo 'SISI"tatizo ni SUPERVISOR wetu.

Na mwisho hatuwezi kutibu tatizo kama WATANZANIA aka WADANGANYIKA hatujaamua kuwa wamoja!Ona WABUNGE tuliowachagua wako busy wanatetea ujinga/wizi wengine wameshindwa hata kukumbuka phrases walizopewa na mafisadi.Unadhani tutaweza kulimaliza hili?

Kwa sasa hata wafanyakazi wa SERIKALINI walitakiwa kupewa ajira za MIKATABA ili kuwe na funzo .
 
Wanaomshangaa Pasco mimi inabidi niwashangae wao, ni afadhali kumshangaa Mzee Mwanakijiji angalau ameshiriki harakati nyingi kabla na yeye hajanunuliwa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom