Pasco, unaomba tuelewashane wakati tayari umeshatoa hitimisho!! Tangu mwanzo hata kabla ya PAC kuwasilisha kamati msimamo wa Kafulila umekuwa kwamba ndani ya akaunti ya ESCROW kuna fedha ya TANESCO (umma). Hakuna aliyewahi kusema kwamba pesa yote ni ya umma. Kumbuka kwamba hela yote imetokana na shauri mahakamani. Badala ya kuilipa IPTL pesa ilikuwa inakwenda kwenye hii akaunti hadi shauri lingeamuliwa ili kujua kiasi halisi ambacho IPTL walistahili. Mahakama ikaamua kwamba ni kweli kwamba TANESCO walikuwa wanalipa pesa nyingi zaidi kuliko uhalisia. Sisi tukapewa nafasi ya kukokotoa mahesabu ili tuchukue cha kwetu na kinachobaki kiende IPTL. Tumeshindwa au tusema tumekaa kufanya hivyo kwa sababu hiyo pesa tulishaipiga, haipo. Ndio hizo akina Ruge wamezigawa kama njugu. Sasa utasemaje kwamba hakuna pesa yetu pale?
Hata kitendo tu cha akina Ruge kugawa hela ovyo kinakwambia kwamba ile haikuwa pesa yao. Katika hali ya kawaida kama ile ingekuwa pesa yao walioipata kihalali ingewezekanaje waigawe ovyo namna hiyo? Matarajiri wa Tanzania ni Rostam, Bakhresa na Mengi, mbona hatujasikia wakigawana fedha bararani namni ile? Na kwa nini waliogawiwa wote ni wanasiasa, viongozi na watu wenye mamlaka fulani? Kwa nini Ruge hakwenda kugawa hizi fedha kwa wanafunzi wetu waliokosa mikopo kama kweli ana roho nzuri kiasi hicho?
Haya, wewe unaona ni sawa watu kugawana pesa kama maembe kama walivyofanya? Nchi za wenzetu hata kuingia na dola 10,0000 wanakuzuia lazima utoe maelezo ya kutosha na vielelezo kibao. Hapa kwetu watu wanagawana pesa kwenye rambo wewe unaona ni sawa hiyo? Pasco please!!