Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Wanabodi,

Kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "An Enemy of the People" by Henrik Ibsen mnaweza kuniita mimi Paskali kuwa ni "an enemy of the people!", Fedha za Escrow, Sio Fedha za Umma!, hizo Bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya Escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme!.

Inawezekana PAP amenunua kampuni hewa, amefanya utapeli kuinunua IPTL toka kwa wamiliki halali, hayo hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme kweli unaokuwa genereted na mitambo ya IPTL, ni umeme kweli na sio umeme hewa!, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!.

Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!.

Niko tayari to pay the price of expresing my opinion kuwa Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma!.

Paskali

Ufafanuzi unapatikana hapa kwa Mkuu Ng'wamapalala.
Hoja za Kamati ya PAC zinavyokinzana kuhusu Escrow akaunti kama ni fedha ya umma



Mkuu Mwalimu, Prof. Kitila, kwanza hongera kupata uprofesa, maana hatujakutana humu jukwaani kwenye thread yangu yoyote tangu umekuwa prof, bado nimekuzoea zaidi kama Dr. Pili nimefarijika sana, kunitembelea kwenye uzi huu, its an honour to me and to my thread, kama nilivyofarijika nilipo tembelewa na Mchambuzi na Nguruvi 3.

Kwenye posti yako ume raise hoja 12 za msingi, mwanafunzi unapoulizwa maswali na mwalimu, unaamini kabisa mwalimu anajua, ila anakuuliza tuu ili kuujua ufahamu wako, inapotokea mwalimu anaomba kueleweshwa na mwanafunzi, then mwanafunzi huyo anakuwa more than gladi kumuelewesha mwalimu, na hapa mwanafunzi atajisikia sasa yeye ndio mwalimu, na mwalimu ndio mwanafunzi wake, hivyo Mwalimu Kitila, karibu katika darasa langu.

  1. Mimi ni mkweli daima hivyo mara kadhaa huanzia kwa kuweka "the end" na kisha ndipo na "justify the means". The end product hapa "pesa ni za nani?!", naanza kwenye kumtaja mwenye pesa ndipo tuje kuhalalisha kwa nini sio pesa za umma!. Kuna hoja za mijadala, na kuna hoja sio za mijadala ni straight conclusive!. Ingekuwa hoja yangu ni mjadala, ningeiliza Jee Fedha za Escrow ni za Umma?, ili watu walete michango, mwisho tufikie hitimisho!. Hapa kuna ukweli na uongo!, kuna kumaninishana kwa kudanganyana kuwa fedha za umma zimeibiwa!, zimechotwa, zimekapuliwa, hivyo wananchi wamehaminika, wakati ukweli ni kuwa fedha hazikuibiwa zimelipwa!. Mtindo wangu wa kutoa conclusiwe sikuanza leo, tulupoanza tuu huu mchakato wa katiba, nilisema tutapata "bora katiba". Kabla kura hazijapigwa kuipitisha nilisema humu "kura zisipotosha, zitatosheshwa!". Sasa watu wanapigia chapuo kura za hapana, nikasema wazi huko ni kujifurahisha kwa sababu kura za ndio "zitatosheshwa!", na kwenye siasa pia mara kibao nimeweka conclusive humu hata "2015 ni CCM tena!" kwa sababu hatuna any serious opposition, Ukawa mimi nauita ni just a "married of convenience!", conveniences zikiisha kila mtu atashika njia yake!. Escrow sio fedha za umma!.
  2. Hapa tuko wote, ndani pesa za account ya escrow zimechange formas mara tatu, au zime change hands mara tatu, kuna mtu anaitwa depositor, ambaye yeye ni Tanesco, fedha zilipokuwa mikononi mwa Tanesco, ni fedha za umma, kitendo cha kuzitoa ndani ya account ya Tanesco kuzi deposit kwenye escrow, kitendo cha depositing, kumezichange form hizi fedha from kuwa pesa za umma, into pesa za depository, na zimechange hands from mikono ya Tanesco to mikono ya depositor ambaye yeye ni custodian tuu wa fedha hizo hadi mgogoro utakapokwisha!, hivyo wakati fedha zikiwa kwenye safe custody ya custodian, fedha zile sii za umma wala sii za binafsi, some zingeweza kuwa za umma na kurudishwa Tanesco, some zingeweza kuwa za IPTL with a unique options ya possibility with "uncertainty" that "only some" "could" be Tanesco's, but with definite that some are IPTL's with possibility ya all kuwa ni za IPTL!. Unakijua ni nini kilichotokea kuhusu madai ya Tanesco na ni nini kilikubalika?!. Tanesco wali give in, na kukubali wanadaiwa more than that na wakaweka schedule of repayment na ndipo Tanesco waka authorise pesa zote zilipwe kwa IPTL!, and that is when all the money zili change form kutoka kuwa fedha za wote na kugeuka fedha za binafsi, and during withdrawer by the time fedha zinalipwa IPTL zilikuwa sio fedha za umma!.
  3. Ni kweli Tanesco ilikuwa overcharged hugely hivyo tulikuwa tunaibiwa!, ila wizi wenyewe ni kwa mujibu wa mkataba na tulikubali, kama tulivyokubali kununua radar, ndege ya rais, vifaa vya kijeshi na sasa bomba la gesi na mikataba ya gesi, nenda kanisome hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ...Tetesi: Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ni Kiini Macho!. Hivyo kama ni kuwa overcharged, kila siku tunakuwa overcharged, overpriced, na huge kick backs!.
  4. Nashukuru kuwa kumbe unajua tulipewa hii nafasi jee unajua tuliitumiaje?!. Hii ndio conversion process ya kuachia fedha za umma zilizoibiwa na kugeuka fedha binafsi!.
  5. Hatukushindwa!, this is where the deal is!, PCCB ni nothing!, Hosea is nothing!, kitu kinachoitwa usalama wa Taifa is nothing!, tangu mwanzo IPTL ni rushwa mwanzo mwisho, what did we do?!. Bodi ya Tanesco ilipata "ganzi!" ya ajabu!, wakaridhia kwa maandishi pesa zote ni za IPTL!. Ruge na Singasinga ni wapiga dili, kama pesa zilikuwa zetu, then kikulacho kii nguoni mwetu!, tusitafute mchawi!, wala tusimbebeshe msalaba mtoto wa Mkulima, wezi wetu tunawajua na ni wale wale toka Richmond, Dowans hadi Simbioni!. Tungekuwa na akili laiti mgelijua huyo Simba mwenye 50% ya PAP ndipo angalau mngenielewa!.
  6. "Mwenye kisu kikali ndiye anaekula nyama!", "fimbo iliyoko mkononi ndiyo uiwayo nyoka!", "the end justify the means!", "Aliyeshika usukani wa gari ndiye dereva" regardless gari ni la nani!, hivyo as long as pesa iko mikononi mwa JR as private money, what he does with his monies!, is non of our businesses!.
  7. Private money is none of our business!.
  8. Kumbe sasa tatizo ni kugawa?!, Ukimuondoa Bakhresa, please don't talk of Mengi and Rostam, kwao this is "missed opportunity!", masking JR akajivutia na kujinyamazia, haya yote yasinge fumka!. Siku zote wahindi wanapiga dili hizi na kujituliza tuli!, lakini masikini wakipata.... Kuna DCP walipiga wahindi watupu wakatulia haikubumburuka!, EPA wahindi walikuwa wanaipiga long time, huku wametulia, Waswahili walipoingia tuu, wanasafiri 1st class, wananunua Vogue custom made kutoka UK, wanasafirisha kwa air cargo, gari zinafika zina kuwa cleared by cash on the spot!, mtaani mbona tulikomaje?!, si ndio dili ikabumbuluka!, wangejinyamazia tuu kama walivyo wahindi yote haya yasingetokea!.
  9. As long as sio hela ya umma, haijalishi nani amegaiwa na kwa huduma gani, ndio maana nikasema PCCB is nothing!, mnaangalia waliogaiwa pesa, haya ni matokeo tuu!, mnaacha kuangalia chanzo cha jinamizi hili la IPTL na kila kitu kiko wazi!, Rutabanzibwa alikataa hongo ya dola 200 na akahamishwa!, unamjua waziri wake alikuwa nani?, kama KM alimegewa dola laki mbili, jee aliyekuwa waziri alipewa ngapi?, unamjua ni nani?. Pesa zikiisha kuwa zako, you are free kuzigawa utakavyo bila kuvunja sheria yoyote!. Hakuna sheria inayokataza kugawa pesa wala jinai yoyote kupokea pesa yoyote kwa kazi yoyote au hata bila kazi yoyote!. Hata mimi kuna wakati "huwapitia wale" na kukubaliana bei, then nikifika huko, ninachange mind, lakini bado nalipa mtu bila kufanya chochote, its my money!.
  10. When the money is yours, you are free to use it as you please!, kwa winging umasikini ni laana, hivyo badala ya kuwagawia masking unamuomba Mungu, masking wore bora wajifie tuu na umasikini wao, na kumfutilishia Mungu kuwa mwenye nacho, ataongezewa!, asiye nacho atanyang'anywa hata kidogo alichonacho!, mzee wa vijisenti, kapewa katiba, ndiye mwenyekiti wa kamati ya bajeji na ndie mshauri wa JR wa mambo ya kisheria na umeona consultancy fee yake!.
  11. Yes ni saws kabisa na amini usiamini, hata mimi Paskali nikiwa nazo, huwa nagawa!, tofauti ni kiwango, kwa uwezo wangu huwa nagawa ten ten, jelo jelo hadi buku buku!, kila nikienda bush, nahakikisha nina kama just 1.M tangu bank naiomba in small denominations, nikitua bush!, kijiji kizima kinajua leo mtoto wa mama fulani ameingia kijijini, kuanzia pombe hadi hizo ten ten, jeero jero na buku buku, its my money, I do with it what it pleases me!. Kwenye ule mgao kuna kick backs, kuna asante, kuna just sadakalawe kuwa "ninazo" kuna genuine charity na kuna sadaka!.
  12. Sio nchi za wenzetu hata sisi tunayo FIU pale BOT, miala yote ya more than 10.m lazima taarifa ziende FIU ndio maana siku hizi hakuna kutoa malipo more than that bila kupitia BOT, the only exception ni same bank transactions ndio maana recipients wote walilazimishwa lazima wafungue account the same bank!. Nawaombeni sana msibabaishwe na huto tujisenti kwenye account za Mkombozi, the real transactions zimefanywa kwenye account yake iliyoko nchi Uholanzi, naamini "wanene" wamepewa asante zao zimehifadhiwa kule "Credit Sussie" transactions zinafanywa kwa "codes" only!, hata bank manageger, hawezi kujua jina la account holders!.
Natumaini mwalimu utakuwa umenielewa!.

Ni wako mwanafunzi mtiifu
Paskali
Hawa ndiyo waandishi wetu wa habari jamani. Magufuli naona fungia magazeti na vyombo vyote vya habari vyenye makanjanja halafu waambie waombe leseni upya ili wachujwe.
 
Wanabodi,

Kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "An Enemy of the People" by Henrik Ibsen mnaweza kuniita mimi Paskali kuwa ni "an enemy of the people!", Fedha za Escrow, Sio Fedha za Umma!, hizo Bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya Escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme! kwa kumlipa mfua umeme, IPTL, hivyo sio fedha za umma!.

Inawezekana PAP ni matapeli, na amenunua IPTL kitapeli, hivyo IPTL chini ya PAP ni kampuni hewa, amefanya utapeli kuinunua IPTL kitapeli, toka kwa wamiliki halali, hayo hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme ambao sio umeme hewa, bali ni umeme kweli unaokuwa generated na mitambo ya IPTL, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!.Kwa lugha rahisi, hata baada ya PAP kulipwa fedha zilizoko ndani ya escrow account, bado Tanesco inadaiwa!.

Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!. Mimi ni mkweli wa kihivi, niko tayari to pay the price of expressing my opinion kuwa Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma!.

Paskali

Ufafanuzi unapatikana hapa kwa Mkuu Ng'wamapalala.

Hoja za Kamati ya PAC zinavyokinzana kuhusu Escrow akaunti kama ni fedha ya umma


Mkuu Mwalimu, Prof. Kitila, kwanza hongera kupata uprofesa, maana hatujakutana humu jukwaani kwenye thread yangu yoyote tangu umekuwa prof, bado nimekuzoea zaidi kama Dr. Pili nimefarijika sana, kunitembelea kwenye uzi huu, its an honor to me and to my thread, kama nilivyofarijika nilipo tembelewa na Mchambuzi na Nguruvi 3.

Kwenye posti yako ume raise hoja 12 za msingi, mwanafunzi unapoulizwa maswali na mwalimu, unaamini kabisa mwalimu anajua, ila anakuuliza tuu ili kuujua ufahamu wako, inapotokea mwalimu anaomba kueleweshwa na mwanafunzi, then mwanafunzi huyo anakuwa more than glad kumuelewesha mwalimu wake, na hapa mwanafunzi atajisikia sasa yeye ndio mwalimu, na mwalimu ndio mwanafunzi wake, hivyo Mwalimu Kitila, karibu katika darasa langu utulie kama mwanafunzi wangu!.

  1. Mimi ni mkweli daima hivyo mara kadhaa huanzia kwa kuweka "the end" na kisha ndipo na "justify the means". The end product hapa "pesa ni za nani?!", naanza kwenye kumtaja mwenye pesa ndipo tuje kuhalalisha kwa nini sio pesa za umma!. Kuna hoja za mijadala, na kuna hoja sio za mijadala ni straight forward, final na conclusive!. Ingekuwa hoja yangu ni mjadala, ningeuliza "Jee Fedha za Escrow ni za Umma?", ili watu walete michango, mwisho tufikie hitimisho kama niza umma au laa!. Hapa kuna ukweli na uongo!, kuna kuaminishana uongo kwa kudanganyana kuwa fedha za umma zimeibiwa!, zimechotwa, zimekapuliwa, hivyo wananchi wamehamanika, kuwa wanaibiwa, wakati ukweli ni kuwa fedha hazikuibiwa bali zimelipwa!. Mtindo wangu wa kutoa conclusive sikuanza leo, tulupoanza tuu huu mchakato wa katiba, nilisema tutapata "bora katiba". Kabla kura hazijapigwa kuipitisha nilisema humu "kura zisipotosha, zitatosheshwa!". Sasa watu wanapigia chapuo kura za hapana, nikasema wazi huko ni kujifurahisha kwa sababu kura za ndio "zitatosheshwa!", na kwenye siasa pia mara kibao nimeweka conclusive humu hata "2015 ni CCM tena!" kwa sababu hatuna any serious opposition, Ukawa mimi nauita ni just a "married of convenience!", conveniences zikiisha kila mtu atashika njia yake!. Escrow sio fedha za umma!.
  2. Hapa tuko wote, ndani pesa za account ya escrow zimechange forms mara tatu, au zime change hands mara tatu, kuna mtu anaitwa depositor, ambaye yeye ni Tanesco, fedha zilipokuwa mikononi mwa Tanesco, ndio zilikuwa fedha za umma, kitendo cha Tanesco kuzitoa ndani ya account ya Tanesco kuzi deposit kwenye escrow account, kumezichange form hizi fedha from kuwa pesa za umma, into pesa za depository, ambaye yeye ni custodian tuu wa fedha hizo hadi mgogoro utakapokwisha!, hivyo wakati fedha zikiwa kwenye safe custody ya custodian, escrow account chini ya BOT, fedha zile sii za umma wala sii za binafsi, some zingeweza kuwa za umma na kurudishwa Tanesco, some zingeweza kuwa za IPTL with a unique options ya possibility with "uncertainty" that "only some" "could" be fedha za umma, za Tanesco's, kutokana na overcharging, but with definite that some are IPTL's with possibility ya all the money ni za IPTL!. Ukijua ni nini kilichotokea kuhusu madai ya Tanesco na ni nini kilikubalika?!. Tanesco wali give in, na kukubali wanadaiwa more than kiwango kilichopo ndani ya escrow account, that na wakaweka schedule of repayment na ndipo Tanesco waka authorize pesa zote zilipwe kwa IPTL!, and that is when all the money zili change form kutoka kuwa fedha za wote na kugeuka fedha za binafsi, and during with drawer by the time fedha zinalipwa IPTL zilikuwa sio fedha za umma!.
  3. Ni kweli Tanesco ilikuwa overcharged hugely hivyo tulikuwa tunaibiwa!, ila wizi wenyewe ni kwa mujibu wa mkataba na tulikubali, kama tulivyokubali kununua radar, ndege ya rais, vifaa vya kijeshi na sasa bomba la gesi na mikataba ya gesi, nenda kanisome hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ...Tetesi: Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ni Kiini Macho!. Hivyo kama ni kuwa overcharged, kila siku tunakuwa overcharged, overpriced, na huge kick backs!.
  4. Nashukuru kuwa kumbe unajua tulipewa hii nafasi jee unajua tuliitumiaje?!. Hii ndio conversion process ya kuachia fedha za umma zilizoibiwa na kugeuka fedha binafsi!.
  5. Hatukushindwa!, this is where the deal is!, PCCB ni nothing!, Hosea is nothing!, kitu kinachoitwa usalama wa Taifa is nothing!, tangu mwanzo IPTL ni rushwa mwanzo mwisho, what did we do?!. Bodi ya Tanesco ilipata "ganzi!" ya ajabu!, wakaridhia kwa maandishi pesa zote ni za IPTL!. Ruge na Singasinga ni wapiga dili, kama pesa zilikuwa zetu, then kikulacho kii nguoni mwetu!, tusitafute mchawi!, wala tusimbebeshe msalaba mtoto wa Mkulima, wezi wetu tunawajua na ni wale wale toka Richmond, Dowans hadi Simbioni!. Tungekuwa na akili laiti mgelijua huyo Simba mwenye 50% ya PAP ndipo angalau mngenielewa!.
  6. "Mwenye kisu kikali ndiye anaekula nyama!", "fimbo iliyoko mkononi ndiyo uiwayo nyoka!", "the end justify the means!", "Aliyeshika usukani wa gari ndiye dereva" regardless gari ni la nani!, hivyo as long as pesa iko mikononi mwa JR as private money, what he does with his monies!, is non of our businesses!.
  7. Private money is none of our business!.
  8. Kumbe sasa tatizo ni kugawa?!, Ukimuondoa Bakhresa, please don't talk of Mengi and Rostam, kwao this is "missed opportunity!", masking JR angejivutia na kujinyamazia, haya yote yasinge fumka!. Siku zote wahindi wanapiga dili hizi na kujituliza tuli!, lakini masikini wakipata.... Kuna DCP walipiga wahindi watupu wakatulia haikubumburuka!, EPA wahindi walikuwa wanaipiga long time, huku wametulia, Waswahili walipoingia tuu, wanasafiri 1st class, wananunua Vogue custom made kutoka UK, wanasafirisha kwa air cargo, gari zinafika zina kuwa cleared by cash on the spot!, mtaani mbona tulikomaje?!, si ndio dili ikabumbuluka!, wangejinyamazia tuu kama walivyo wahindi yote haya yasingetokea!.
  9. As long as sio hela ya umma, haijalishi nani amegaiwa na kwa huduma gani, ndio maana nikasema PCCB is nothing!, mnaangalia waliogaiwa pesa, haya ni matokeo tuu!, mnaacha kuangalia chanzo cha jinamizi hili la IPTL na kila kitu kiko wazi!, Rutabanzibwa alikataa hongo ya dola 200 na akahamishwa!, unamjua waziri wake alikuwa nani?, kama KM alimegewa dola laki mbili, jee aliyekuwa waziri alipewa ngapi?, unamjua ni nani?. Pesa zikiisha kuwa zako, you are free kuzigawa utakavyo bila kuvunja sheria yoyote!. Hakuna sheria inayokataza kugawa pesa wala jinai yoyote kupokea pesa yoyote kwa kazi yoyote au hata bila kazi yoyote!. Hata mimi kuna wakati "huwapitia wale" na kukubaliana bei, then nikifika huko, ninachange mind, lakini bado nalipa mtu bila kufanya chochote, its my money!.
  10. When the money is yours, you are free to use it as you please!, kwa wingine, umasikini ni laana, hivyo badala ya kuwagawia maskini unamuomba Mungu, maskini wote bora wajifie tuu na umasikini wao, na kumfuatilishia Mungu kuwa mwenye nacho, ataongezewa!, asiye nacho atanyang'anywa hata kidogo alichonacho!, mzee wa vijisenti, kapewa katiba, ndiye mwenyekiti wa kamati ya bajeji na ndie mshauri wa JR wa mambo ya kisheria na umeona consultancy fee yake!.
  11. Yes ni sawa kabisa na amini usiamini, hata mimi Paskali nikiwa nazo, huwa nagawa!, tofauti ni kiwango, kwa uwezo wangu huwa nagawa ten ten, jelo jelo hadi buku buku!, kila nikienda bush, nahakikisha nina kama just 1.M tangu bank naiomba in small denominations, nikitua bush!, kijiji kizima kinajua leo mtoto wa mama fulani ameingia kijijini, kuanzia pombe hadi hizo ten ten, jero jero na buku buku, its my money, I do with whatever I wish that will please me!. Kwenye ule mgao kuna kick backs, kuna asante, kuna just sadakalawe kuwa "ninazo" kuna genuine charity na kuna sadaka!.
  12. Sio nchi za wenzetu hata sisi tunayo FIU pale BOT, miamala yote ya more than 10.m lazima taarifa ziende FIU ndio maana siku hizi hakuna kutoa malipo more than that bila kupitia BOT, the only exception ni same bank transactions ndio maana recipients wote walilazimishwa lazima wafungue account the same bank!. Nawaombeni sana msibabaishwe na huto tujisenti kwenye account za Mkombozi, the real transactions zimefanywa kwenye account yake iliyoko nchi Uholanzi, naamini "wanene" wamepewa asante zao zimehifadhiwa kule "Credit Sussie" transactions zinafanywa kwa "codes" only!, hata bank manageger, hawezi kujua jina la account holders!.
Natumaini mwalimu utakuwa umenielewa!.

Ni wako mwanafunzi mtiifu
Paskali
Huu ni ukweli japo unacheleweshwa,zile hela si Mali ya umma

Tuache kutesa watu rumande
 
Mkuu Kinkongu, humu jf tunabishana kwa hoja, mtu akipotosha, unauleta ukweli ambao ni tofauti na upotoshaji.
Kipi nilichopotosha, kama ni kuhusu fedha za escrow, msimamomo ni ule ule, fedha hizo sio fedha za umma!.

P.
Kwa Mujibu wa Zitto,Inasemekana SInga Singa alitembeza Umate Umate(Mrungula) kwa baadhi ya waandishi na baadhi ya wabunge ambao waliokuwa wanasema kwamba fedha za Tegeta Escrow sio za umma.

Kitendo cha PCCB kuwakamata na kuwafungulia mashtaka ya uhujumu uchumi hapo inamaanisha ndani ya zile fedha zilizochotwa ndani yake kuna fedha za umma.

Sipingi Msimamo wako wa kuwa Zile fedha si za umma lakini ukweli umejulikana baada ya Wakurugenzi wa PAP na VIP Engineering kufukishwa mbele ya pilato.
 
Mkuu Kinkongu, humu jf tunabishana kwa hoja, mtu akipotosha, unauleta ukweli ambao ni tofauti na upotoshaji.
Kipi nilichopotosha, kama ni kuhusu fedha za escrow, msimamomo ni ule ule, fedha hizo sio fedha za umma!.

P.
Escrow ni very tricky na ndio maana mara nyingi mjadala wa hii issue huwa nabaki kama mtazamaji!!

Ukiangalia vizuri mkataba wa IPTL ulivyokuwa wa hovyo... uhovyo uliosababishwa na sisi wenyewe!!! Ukachanganya na makesi ya hovyo hovyo yaliyokuwa yanazushwa na TANESCO kupigwa chini; kisha ukafanya reconciliation ya Escrow Account; trust me, usishangae ukakuta ni TANESCO ndie anadaiwa!!!

Tukiachana na mambo ya PAP, pale kwenye Escrow sioni cha kwetu zaidi ya kodi ambayo sina uhakika kama ililipwa au hapana!!!

Na mtu kama hataki kuumiza kichwa, anaweza kutumia just logical reasoning!!!

TANESCO wanauza umeme below unit cost. Sasa kama kuna pesa ya TANESCO ina maana TANESCO walikuwa wanapata faida kupitia IPTL!!!

Sasa tangu lini mtu anaye-charge below unit cost akapata faida!!!!

Na lisilo na mjadala ni kwamba, TANESCO ni loss making corporation!

Itakuwa ajabu TANESCO awe anapata faida kupitia mkataba wa hovyo wakati in general, ni loss making company!!!
 
Kwa Mujibu wa Zitto,Inasemekana SInga Singa alitembeza Umate Umate(Mrungula) kwa baadhi ya waandishi na baadhi ya wabunge ambao waliokuwa wanasema kwamba fedha za Tegeta Escrow sio za umma.

Kitendo cha PCCB kuwakamata na kuwafungulia mashtaka ya uhujumu uchumi hapo inamaanisha ndani ya zile fedha zilizochotwa ndani yake kuna fedha za umma.

Sipingi Msimamo wako wa kuwa Zile fedha si za umma lakini ukweli umejulikana baada ya Wakurugenzi wa PAP na VIP Engineering kufukishwa mbele ya pilato.
Tusubirie.
P.
 
Namna ya Kutumia Taasisi Huru Kufichua Ufisadi: Masimulizi ya Kashfa ya Escrow - Zitto Kabwe

Usiku wa manane nimeamka. Katikati ya msitu mkubwa, hifadhi ya Mikumi, nasikia sauti za ndege na wanyama wengineo wakilia mwituni. Watoto wamelala fofofo.

Nimeshtuka ghafla usingizini. Natafakari tukio kubwa la lililotokea jana Juni 19, 2017 la kukamatwa kwa ndugu Harbinder Singh Seth, mmiliki wa kampuni ya Pan Africa Power Solution (PAP) aliyetwaa kitapeli hisa 70% za kampuni ya kufua Umeme ya IPTL na kuchota zaidi ya shilingi 306 bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Navuta picha ya mahakamani, namwona pia ndugu James Rugemalira mmiliki wa hisa 30% za IPTL, na aliyeuza hisa hizo kwa ndugu Seth kwa malipo yaliyotokana na fedha zilizoporwa kutoka Benki ya Tanzania (BOT). Picha ya watu hawa wakiwa mahakamani chini ya ulinzi wa polisi ilinipeleka mbali Sana kimawazo.

Nakumbuka ujumbe mfupi wa simu (SMS) wa ndugu Richard Mgamba wa Februari 2014, aliyeniandika "piga". Nilikuwa Washington DC nchini Marekani wakati huo, najivuta kupiga simu maana gharama ni kubwa kupiga simu kutoka Marekani.

Napiga simu kwa ndugu Mgamba, ananiwahi kwa swali hata kabla ya salaam "POAC mlizuia fedha kwenye Escrow zisitoke, unajua zimetoka? Tunataka kuandika", ananiuliza. Wakati huo Richard Mgamba alikuwa ni Mhariri wa Habari za Uchunguzi wa gazeti la The Citizen.

Namuomba anipe muda nihakiki taarifa anazonipa. Napiga simu mbili tatu kwa watu mbalimbali kwenye taasisi za Serikali na kuthibitisha. Nikarudi Kumjibu Richard "Ni Kweli endelea. Nyaraka nikirudi".

Wiki hiyo gazeti la The Citizen wakaandika Habari ile kwa mara ya kwanza. Nilikuwa London wiki ya mwisho ya February 2014, wakati Kampuni ya PAP ilipoanza kutoa vitisho na kufungua kesi dhidi ya The Citizen. Nikawa nimerudi nchini na kuanza kukusanya nyaraka muhimu ili kuwasaidia The Citizen.

Naenda kumwona ndugu Ludovick Utouh, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Yeye na timu yake walikuwa katika ukumbi wa Hoteli ya Giraffe, Mbezi Beach, jijini Dar es salaam wakiandika Taarifa ya mwaka ya Mahesabu ya Serikali, Taarifa yake ya mwisho akiwa CAG.

Nikiwa namsubiri Mzee Utouh hotelini hapo, msaidizi wake ananijulisha kuwa amepata kikao ghafla Wizara ya Nishati na Madini, kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara, ndugu Eliakim Maswi, pamoja na Mwanasheria wa Wizara Dkt. Medard Kalemani.

Hivyo naendelea kumsubiri, baada ya nusu saa Utouh anakuja. Namwambia "nimetoka kuonana na (namtajia jina na cheo - kwa sasa nalitunza si vema kumtaja), amenipa nyaraka zote za fedha zilizotunzwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow na kutolewa kulipwa PAP kama mmiliki wa IPTL. Sisi PAC tunataka sasa ufanye ukaguzi maalumu wa suala hili".

Nikiwa London nilikuwa nimeshampigia simu mzee Utouh kumwambia asome gazeti la The Citizen. Pia nilikuwa nimezungumza na Makamu Mwenyekiti wa PAC, ndugu Deo Fulikunjombe juu ya jambo hili. Yeye baada ya kushauriana na wajumbe wa Kamati tulikubaliana kuwa njia bora ni hiyo ya uchunguzi wa CAG.

Katika mazungumzo yetu Mzee Utouh ananiambia kuwa alikuwa na kikao na Maswi na ameomba pia ukaguzi maalumu. Nikashtuka kidogo maana anayeagiza ukaguzi maalumu ndiye anapewa Taarifa hiyo. Nikajua nini cha kufanya.

Nilimaliza kikao saa nne usiku na kumfuata kwanza ndugu Mgamba na kumpa nyaraka kadhaa muhimu ambazo nilizikusanya baada ya kurudi nchini (kujihami iwapo nitavamiwa na kupoteza nyaraka husika). Nikampa nakala nyengine msaidizi wangu ili ziwe scanned na kuwekwa www.jamiiforums.com, kisha nikafanya kikao cha dharura na ndugu Deo Filikunjombe.

Tukakubaliana Deo awasiliane na Spika kumwomba idhini ya kikao cha dharura cha PAC, na Mimi niwasiliane na Katibu wa Bunge kuwaambia makatibu waitishe kikao. Baada ya siku mbili tukamwita Gavana wa Benki Kuu mjini Dodoma. Baada ya kikao kifupi PAC ikaagiza rasmi ukaguzi Maalumu kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow. Tukaagiza Taarifa iletwe Bungeni na sio Wizarani.

Mkakati huu ulitusaidia mno mbeleni kwani juhudi za Serikali kuzuia ukaguzi ziligonga mwamba maana mchezo wa Wizara tuliushtukia na kuuzuia. PAC ilitoa Taarifa kwa Umma juu ya ukaguzi husika, lakini ni The Citizen peke yake waliotoa habari ile.

Tulishindwa vita ya habari mapema sana kiasi cha taarifa rasmi za PAC kutoandikwa kabisa. Mwezi Machi nikapata jukumu la mtoto kwa mzazi ambapo mama yangu aliumwa ghafla na ikapaswa nimpeleke kwenye matibabu India. Alikuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na hivyo Bunge kulipia gharama zake za matibabu.

Hii maana yake ni kwamba sikuwa na muda wa kufuatilia suala hili, hivyo ilibidi kumpa nguvu Makamu wangu aliyebaki kuendesha Kamati ya PAC, namshukuru sana ndugu yangu Deo Fulikunjombe kwa uzalendo wake, alifanya kazi kubwa sana.

Mungu akasaidia sana, ndugu David Kafulila akajitokeza kubeba jukumu la kuweka shinikizo kwa Serikali. Yeye akitaka Kamati Teule ya Bunge yenye kuundwa na Wabunge kuchunguza suala hili. Aliongea kwenye Makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwezi Aprili na akaendelea kuibua jambo hili kila alipopata nafasi.

Mwanzoni magazeti mengi yalikuwa yanapotezea habari hii, na hata michango ya Kafulila. Nakumbuka baada ya hotuba ya Waziri Mkuu niliwaambia wahariri kuwa wamevaa miwani za mbao. Kafulila hakuchoka akaendelea kusema kila aliposimama Bungeni hali iliyopelekea aitwe Tumbili.

Tulipata msaada pia wa aliyekuwa Mbunge wa Simanjiro, ndugu Chritopher Ole Sendeka, alitoa msaada mkubwa sana kwa kamati. Naye akatukanwa kuwa hakuwa msomi na alipata zero akiwa kidato cha sita. Vyombo vya Habari vilishangilia sana vioja hivi vya Waziri kutaja matokeo ya shule ya mbunge bungeni ili kumvunjia heshima mbele ya jamii.

Mtindo huu wa kuvunjia watu heshima pia ulitumika dhidi yangu, kwa kutengeneza kijitabu cha propaganda kilichogawanywa kwa ustadi na mafanikio makubwa kwa kila Mbunge nyumbani kwake mjini Dodoma. Kijitabu hicho kilijaa uzushi kwamba nimehongwa na ndugu Seth wa PAP na mambo mengine mengi ya kutia aibu. Kukumbuka tu haya kunatia uchungu mno, na ninavuta hisia za waliotengeneza vijitabu vile na kusambaza na waliowalipa. Inasikitisha sana nikikumbuka haya.

Ilibidi kuingia kwenye kuandika makala kwenye magazeti ili kuwaelimisha wananchi kuwa fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwamo za Umma. Seth akaamua kutushitaki mimi pamoja na gazeti la Raia Mwema kwa kuchapisha makala husika, na kutudai shilingi 500 bilioni. Kesi husika inaendelea mpaka Leo mahakamani.

Magazeti mengi yalianza kuimba wimbo wa Seth. Jamii iligawanyika sana kwani PAP na Seth walianza kutoa misaada kwenye nyumba mbalimbali za ibada pamoja na taasisi za Serikali kama Jeshi la Polisi. Tulivunjwa moyo mno katika mazingira yale, lakini hatukukata tamaa.

Ilibidi niandae andiko maalumu kuelewesha jamii ya wasomi kuwa Seth na wenzake ni matapeli. Kupitia mawakili wa kimkakati tulipata nyaraka za kuonyesha kuwa Seth alipewa hisa za IPTL bila kulipa kodi ya ongezeko za mtaji.

Wakati mwengine mambo hutokea duniani kwa mipango ya mungu. Mwaka 2012 nilikuwa nimepeleka Bungeni mabadiliko ya sheria za Fedha zenye kutaka kuwa uhamisho wa umiliki wa kampuni usifanyike mpaka kwanza kodi imelipwa na cheti cha kamishna wa kodi kimetolewa, lengo lilikuwa ni kuongeza mapato ya Serikali na kupunguza ukwepaji wa mapato, hasa kwenye sekta ya madini, mabadiliko hayo ni maarufu kwa jina la "Capital Gain".

Ni mabadiliko hayo ndiyo ambayo yalikuja kuwa msaada mkubwa sana kwenye harakati hizi za uchunguzi wa kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Nilipomaliza andiko lile likalifasiri Kwa Kiswahili na kutengeneza kitabu maalumu. Nikakaa na David Kafulila na kutafuta fedha ili afanye ziara kwenye mikoa kadhaa, ikiwemo Mwanza na Mbeya ili kuzungumza na wananchi moja Kwa moja na kugawa kijitabu kile.

Ndugu yangu mmoja (sitamtaja kwa jina, namshukuru sana) akanisaidia usanifu na picha kwa ajili ya kijitabu kile, picha tuliyoitumia tuliipata kutoka kwa mpiga picha wa gazeti la mwananchi. Mdogo wangu mmoja, ndugu Balozi Jamanda akazalisha nakala za kutosha za kijitabu na kusambaza nchi nzima kwenye ziara za Kafulila ambazo nilizifadhili ili kuendeleza mjadala tukiwa tumesusiwa na vyombo vya habari.

Septemba 2014, nikaenda Kwa CAG kuwasilisha maelezo yangu ambayo kimsingi ilikuwa kitabu kile. Wakati huu sasa The Citizen walikuwa wamepata nguvu ya Raia Mwema chini ya Ezekiel Kamwaga na Mtanzania chini ya Dennis Msaki (kwa ushawishi mkubwa wa mwandishi kijana Freddy Azzah). Tukaanza kupata nguvu na shinikizo likaendelea.

Tukapata hati halisi za umiliki wa Mechmar kutoka benki ya Standard Chartered ya Hong Kong. Kimkakati tukaitoa hati hii kupitia gazeti la The Citizen na wakaichapisha. Tukawa tunapata uelewa wa wananchi kwa kuridhisha kabla ya CAG kuwasilisha taarifa yake kwenye Kamati.

Watu wa PAP/IPTL nao waliongeza nguvu. Sauti dhidi ya ukwapuaji ule ilikuwa ni ya Kafulila na PAC tu. Ilituvunja moyo sana kuwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani nchini walikuwa kimya kabisa mpaka dakika za mwisho. Tulikuwa tunajiuliza nini hasa kimetokea? Tulipata nguvu ya pamoja baada ya hoja kufikishwa kwenye Kamati na Kwa makusudi kabisa kuvujisha baadhi ya taarifa kwenye vyombo vya habari ili kupata uungwaji mkono wa wananchi.

Watu wa PAP/IPTL pia walikuwa na mikakati yao ya vyombo vya Habari. Kwanza walicheza na Taarifa ya CAG na kuisambaza kwa nguvu kabla ya taarifa rasmi kutolewa. Hawakujua kuwa sisi PAC tulikuwa na tarifa ya kwanza kabisa ya CAG ambayo ilikuwa na ukweli wote kabla ya taarifa yao iliyochezewa. Ndio maana kulikuwa na mchanganyiko mkubwa Kwa umma kuhusu Fedha ni za Umma au si za Umma, kwani ilikuwa ni mkakati maalumu wa wakwapuaji wa fedha zile.

Ili kujenga umoja ndani ya Bunge nilimwomba spika kuniongezea wajumbe kwenye Kamati, ombi ambalo lilikubaliwa. Tuliongezewa wajumbe kadhaa, akiwemo ndugu Kangi Lugola, Suleiman Zedi na Dkt. Hamis Kigwangalla. Hawa walikuwa ni viongozi wa Kamati nyengine. Lengo letu lilikuwa ni kuongeza nguvu kwenye Kamati ya Uongozi na pia sauti zenye uelewa. Tulitaka kuwe na taswira kubwa ya Kamati, isiwe tu ni PAC, iwe ni ya vyama vyote na yenye taswira ya Kitaifa. Jambo hili lilitusaidia sana.

Wakwapuaji nao walijipanga kwenye Fedha. Walikuwa wanagawa fedha Kwa kila mbunge anayechangia. Sisi tuliamua kuwachezea mchezo wa kupanga wachangiaji wetu wazuri siku ya mwisho na wao wakajaa kuchangia siku ya pili ya uwasilishaji wa taarifa bungeni, alhamis. Deo Filikunjombe alifanya kazi hiyo ya mkakati.

Spika Makinda na kabla yake Naibu spika Ndugai walitupa ushirikiano mkubwa. Ndugai alitwambia wakati wa kukabidhiwa ripoti, namnukuu "waelezeni Watanzania ukweli. Nipo nanyi". Kweli alikuwa nasi na ili kutupunguza nguvu akapewa safari ya ghafla kwenda Paris. Lakini Spika Makinda alikuwa ameelewa jambo hili vizuri sana. Alitupa mwongozo kama mzazi, kutoka mwanzo mpaka mwisho. Naushukuru sana uongozi wa Bunge.

Pia tulijua kuwa wabunge wa CCM wakiweka msimamo wa kupinga, taarifa yetu itakwama. Siasa za kibunge uamuliwe kwa msingi wa Demokrasia wa "wengi wape". Wabunge wa CCM ndio wengi bungeni, ukitaka jambo lako ni lazima ujenge ushawishi kwao. Ilibidi niongee na aliyekuwa Katibu Mwenezi, ndugu Nape Nnauye akiwa kwenye ziara mikoa ya Kusini na kumwambia amwombe Katibu Mkuu wao, ndugu Abdulrahman Kinana kuwa pasiwe na msimamo wa Chama chao kwenye jambo hili. Kuwe na Uhuru wa Wabunge wa CCM kuzungumza. Ndugu Kinana akatuhakikishia hilo.

Deo Filikunjombe akazungumza na Mzee Mangula ambaye alikuwapo dodoma kumwomba hivyo hivyo. Mzee Mangula alimwuliza "kwanini maazimio umesoma wewe na sio Mwenyekiti wako? Sio mtego kuwa wewe ndio unyonge CCM wenzako?". Bahati nzuri jambo tulilipanga vizuri kabla.

Mimi nilikuwa kwenye ugomvi mkubwa na Chama changu wakati huo Chadema. Kwahiyo kwanza ilibidi nijisogeze kwao ili taarifa isipate mkwamo, lakini pia ilibidi ionekane ni kazi ya pamoja hivyo tusome Mimi na Deo ambaye alikuwa CCM. Tulifanikiwa sana. Hii ilikuwa kazi hasa ya wabunge wote, bila kujali vyama vyao, kitaswira na kwa uhalisia.

Hata Kamati ya kuandika maazimio tukawaweka watu kama ndugu Tundu Lissu na Freeman Mbowe, na upande wa CCM, ndugu Anna Kilango Malecela ambaye mwanzoni hakuwa upande wetu. Tulifanikiwa kujenga mwafaka wa kibunge.

Watafiti watakapokuwa wanaandika kuhusu 'Siasa za Bunge'watakuta kuwa huu ni mfano bora Kabisa wa kujenga mwafaka ndani ya Bunge Kwa maslahi ya Taifa. Azimio la kwanza Kabisa likawa Harbinder Singh Seth akamatwe na kushtakiwa kwa utapeli na wizi.

Jana nilipoona picha ya Seth akiwa anapandishwa mahakamani chini ya ulinzi wa polisi nikapata msisimko mkubwa Sana. Kisaikolojia picha ile ina maana kubwa sana kwenye vita dhidi ya ufisadi nchini. Rais Magufuli amefanya jambo la kiukombozi (psychological liberation).

Naamini watu Kama David Kafulila jana walikuwa na furaha sana ya kuona matunda ya kazi yao. Alisimama kidete kuhakikisha ajenda haifi mpaka PAC ilipomaliza kazi. Wajumbe wa Kamati ya PAC ya 2013 - 2015 wote wanastahili pongezi kubwa maana tungekubali kugawanywa tu tungepoteza ajenda.

Mshikamano tulioonyesha ilikuwa silaha kubwa. Wapo mashujaa ambao siwezi kutaja majina yao (Unsung Heroes), hawa ni wengi mno, wengine ni watumishi wa bunge. Sitaki kuwataja lakini vijana wale na mama yule chini ya katibu wa Bunge walipata majaribu makubwa Sana. Walisimama kidete.

Mtu mwengine muhimu kwenye jambo hili ni mzee wangu Edward Hosea wa Takukuru. Yeye, Utouh pamoja na watumishi wa Ofisi ya CAG walisaidia Kamati kwa kiwango cha juu kabisa. Mpaka Leo nikimuwaza Hosea kwenye sakata hili kama nimevaa kofia ninaivua kwa heshima kubwa sana kwake.

Aliyekuwa Kamishna wa TRA, ndugu Rished Bade alikata mzizi Wa fitina kwa kuithibitishia Kamati ya PAC ushahidi nyeti sana kuhusu masuala ya kodi. Ni ushahidi huu ambao kama tungeukosa pengine tusingekuwa na taarifa kama ile.

Bunge lilifanya kazi yake, kwa ufahari kabisa, likasaidia Taifa kwa kuleta maazimio yale yaliyolipa heshima. Naona fahari sana kuhudumu kwenye bunge lile.

Jambo hili la Tegeta Escrow limenionyesha kuwa "Watu wema hawafi, hata kama miili yao iko mchangani tayari (kaburini)", na hili ndilo linalojidhihirisha kwa ndugu yangu na rafiki yangu wa karibu mno, aliyekuwa makamu wangu wa uenyekiti wa PAC, Deo Fulikunjombe. Miaka miwili tangu afariki sasa, bado taifa linakumbushwa juu ya uzalendo wake.

Sijui Deo angekuwa hai jana angekuwa katika hali gani. Ninamlilia ndugu yangu. Kitu kimoja ambacho watu wengi hawajui ni kwamba muda wote wa kuandaa tarifa maalum ya PAC kuhusu Tegeta Escrow yeye ndiye aliandaa ulinzi wangu kuhakikisha sidhuriwi. Alimwambia dada yangu aje dodoma kuhakikisha ninakula kile tu kilichpikwa na dada yangu. Shujaa wa kazi hii ni yeye. Ingawa Mimi na yeye tulikubaliana kuwa Gazeti la The Citizen ndiye haswa lililohitaji kutambuliwa kwa kazi hii.

Bahati mbaya sana sisi wanasiasa ndio huonekana zaidi kwa sababu tuna sauti, jambo hili hufanya historia isiwataje wasio wanasiasa, ndio msingi wa waraka wangu huu, kuwapa haki yao wale wasio wanasiasa waliofanikisha kazi hii ngumu kwa maslahi ya Taifa letu.

Mhariri wa gazeti la The Citizen, ndugu Richard Mgamba na waandishi wake kama Mkinga Mkinga ndiyo mashujaa hasa wa jambo hili, kwa niaba ya wenzangu tuliokuwa kwenye Kamati ya PAC, ninawashukuru sana. Tulivunja mwiko na kwenye Taarifa ya Kamati yetu, tulitambua rasmi kazi ya chombo cha Habari katika vita dhidi ya rushwa.

Gazeti la The Citizen lilitimiza wajibu wake katika wakati ngumu Sana wa kupingwa na waandishi wenzao na hata waajiri wao. Mnastahili heshima kubwa sana. Ahsanteni sana.

Funzo kubwa muhimu katika kadhia hii yote ni umuhimu wa uhuru wa kiutendaji wa taasisi mbalimbali nchini. Taasisi huru husaidia uwajibikaji mahali penye makosa, husaidia kufichua ufisadi, na huleta uwazi. Yawezekana bila Uhuru wa Takukuru, CAG, BOT, TRA, Vyombo vya Habari pamoja na Bunge leo nisingekuwa nazungumza haya, ni muhimu sana tupiganie na kulinda uhuru huu wa taasisi.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Juni 20, 2017
Mikumi
Tanzania
 
Escrow ni very tricky na ndio maana mara nyingi mjadala wa hii issue huwa nabaki kama mtazamaji!!

TANESCO wanauza umeme below unit cost. Sasa kama kuna pesa ya TANESCO ina maana TANESCO walikuwa wanapata faida kupitia IPTL!!!

Sasa tangu lini mtu anaye-charge below unit cost akapata faida!!!!

Na lisilo na mjadala ni kwamba, TANESCO ni loss making corporation!

Itakuwa ajabu TANESCO awe anapata faida kupitia mkataba wa hovyo wakati in general, ni loss making company!!!
Mkuu Chige, kwanza ni kweli Tanesco ni loss making corp kwa sababu inanunua umeme kwa bei kubwa kutoka kwa independent producers, na kuuza kwa bei ya chini kuliko iliyonunulia, hili niliwahi kushauri humu
Utumbuaji: Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila ...
Wanabodi,

Nasisitiza Tanzania ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima kwanza tujenge mifumo, systems, ukimess unajitumbua mwenyewe wala huna haja ya kusubiri kutumbuliwa!. Lazima tuwe wakweli kwa kuacha kuingiza siasa kwenye taaluma za watu, kama gharama za uzalishaji umeme per unit ni Kubwa kuliko tozo ya umeme, ukweli ni kwamba umeme lazima upande bei tutake tusitake, hili la Tanesco kuendelea kulishwa kwa spoon feed na serikali huku ikilazimishwa kuuza umeme kwa bei ya hasara, sio sustainable na ni short lived! .

Ili Tanzania tuweze kupiga hatua za kweli za maendeleo na kusonga mbele ni kwanza lazima tuwe wakweli, na pili tuache siasa kwenye kila kitu! .

Let's stop politicizing everything, politicians do politics and leave professionals Alone! .
Heri ya Mwaka Mpya.
Paskali
Paskali
 
Escrow ni very tricky na ndio maana mara nyingi mjadala wa hii issue huwa nabaki kama mtazamaji!!

Ukiangalia vizuri mkataba wa IPTL ulivyokuwa wa hovyo... uhovyo uliosababishwa na sisi wenyewe!!! Ukachanganya na makesi ya hovyo hovyo yaliyokuwa yanazushwa na TANESCO kupigwa chini; kisha ukafanya reconciliation ya Escrow Account; trust me, usishangae ukakuta ni TANESCO ndie anadaiwa!!!

Tukiachana na mambo ya PAP, pale kwenye Escrow sioni cha kwetu zaidi ya kodi ambayo sina uhakika kama ililipwa au hapana!!!

Na mtu kama hataki kuumiza kichwa, anaweza kutumia just logical reasoning!!!

TANESCO wanauza umeme below unit cost. Sasa kama kuna pesa ya TANESCO ina maana TANESCO walikuwa wanapata faida kupitia IPTL!!!

Sasa tangu lini mtu anaye-charge below unit cost akapata faida!!!!

Na lisilo na mjadala ni kwamba, TANESCO ni loss making corporation!

Itakuwa ajabu TANESCO awe anapata faida kupitia mkataba wa hovyo wakati in general, ni loss making company!!!

chige,

Hili suala lilifanywa tricky makusudi. Kumbuka huu ulkuwa ni mradi mkubwa wa kihalifu ambao ulihusisha watu wa kada mbalimbali.

Neno "escrow" lina maana ya utaratibu wa kifedha ambapo mtu wa tatu (third party) anadhibiti na kuratibu fedha zinazohusisha miamala ya watu wawil kwa makubaliano maalum. Third party hapa ilikuwa ni serikali kupitia BoT.

Hata hivyo mjadala kama fedha za escrow zilikuwa za serikali au la kuhusiana na suala la IPTL ulikuwa na lengo la kuuhadaa umma tu. Dhana ya umiliki wa serikali wa fedha za escrow inaweza kuwa na tafsiri kwamba serikali ilichukua dhamana ya kuhakikisha usalama wa hizo fedha, kwa upande mmoja, na katika mzingira kama ilivyodaiwa kuwa IPTL iliuzwa, serikali ilipaswa kuwa na mgawo wake (kama kodi), kwa upande mwingine.

Lakini pia mamlaka pekee na sahihi ya kulitolea tafsiri suala hili alikuwa ni CAG kama alivyofanya.

Hivyo mjadala hapa unapaswa uwe uhalali wa Singa Singa kumiliki IPTL - kitu ambacho ndicho kimempandisha kizimbani.
 
Mkuu Kinkongu, humu jf tunabishana kwa hoja, mtu akipotosha, unauleta ukweli ambao ni tofauti na upotoshaji.
Kipi nilichopotosha, kama ni kuhusu fedha za escrow, msimamomo ni ule ule, fedha hizo sio fedha za umma!.

P.
Tunaheshim mawazo yako ila kwa sake ya mjadala je kivp ruge na seth wagawe pesa namna ile kwa watu wazito serikalini??? Kwanni ampe mgao katibu wa rais??? Kma hela ni zako za kihalali unawezaje kugawana nao mabilion wakati uliyafanyia kazi mwenyewe!!!!
 
Back
Top Bottom