Nimesitisha kutoa mahari

Nimesitisha kutoa mahari

clearmind

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
813
Reaction score
1,913
Tarehe 20 ya mwezi huu niliahidi kwenda kutoa mahari ukweni kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano.

Niliazimia kufanya hivyo baada ya kukaa na mchumba wangu kwa zaidi ya miaka miwili sasa katika mahusiano. Baada ya kutoka safarini wiki iliyopita, nilishikwa na simanzi sana.

Nilimuona rafiki yangu wa karibu wa siku nyingi ambae alikuwa msaada kwangu toka tukiwa shuleni. Physics, chemistry na maths nilifaulu kwa sababu ya uwepo wake.

Nimetafakari mno na hatimaye, jana nilimueleza wazi mchumba wangu kwamba siwezi kuendelea na zoezi la utoaji mahari kwao kwa sababu kuna mtu ambae nahitaji kumshika mkono aondokane na magumu yanayomkabili kwa sasa.

Alisema hakuna shida na kisha kuomba kuvunja uchumba wetu. Sikuchukua muda tena kulifikiria hilo. Nimekubali na kumtakia kila la kheri katika maisha yake mengine.

NITASIMAMA NA RAFIKI YANGU!
 
Ni jambo zuri unalofanya kumsaidia rafiki, kwa maana tupo duniani kusaidiana. Ila swala la wewe na mchumba wako usingelimaliza kwa kumwambia yote hayo.

Maana ameona humthamini (wanawake wanapenda ndoa) ilihali mlikuwa wote kwa miaka 2. Ungetafuta sababu nyingine kusogeza mbele zoezi.

Labda hakuwa mwanamke unayestahili ukaamua kumtema kwa namna hiyo.
 
Hakutaka kusubiri. Huyu mwamba amekuwa nami katika kila hali kabla mimi sijkaa sawa. Ni mateso kwangu kumuona anahangaika. Ngoja mwanamke aondoke. Muda sahihi ukifika atapatikana mwingine.
 
Hujafanya poa na unakaa ujinga Fulani, kwenye mahari ungependa kutoa hata nusu na rafiki Yako ungeweza msaidia tu.

Umefikiria hata kidogo maumivu anayopitia na aibu uliyemsababishia mwenzako. Alafu kama kweli ulikuwa una mpango wa ndoa na uliamua kuoa kwa mahari ya m2.5 Ina maana Hela nyingine unayo?

Yaan ingekuwa ni dada yangu na ulishakuja kujitambulisha Kuna kitu ungelipa!
 
Hujafanya poa na unakaa ujinga Fulani, kwenye mahari ungependa kutoa hata nusu na rafiki Yako ungeweza msaidia tu,
Umefikiria hata kidogo maumivu anayopitia na aibu uliyemsababishia mwenzako,
Alafu kama kweli ulikuwa una mpango wa ndoa na uliamua kuoa kwa mahari ya m2.5 Ina maana Hela nyingine unayo?

Acha hasira mkuu.
 
Tungemchomelea na zile mashine zetu kwenye mbupu
 
Nilipomsihi awe na subira, alikataa.
Ingawa pia ungetumia busara fulani kukamilisha yote mawili, mfano ungemsaidia rafiki huku mahari ungepeleka nusu sio kuahirisha kabisa. Huwezi jua aliwapanga vipi familia yake so anaona aibu kwa kuahirisha kwako.
Pia ungempa sababu nyingine ya kusogeza mbele tofauti na hiyo, rafiki ni muhimu lakini pia mpenzi wako ana umuhimu wake since ndo ubavu wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakutaka kukubali. Mfano, nilimsihi nipeleke mahari tarehe 28 badala ya tarehe ya mwanzo. Tena kwa kunyenyekea sana lakini bado akesema hapana. Nilitumia busara sana ila hakuwa tayari kuelewa.
 
Hio Ni Moja Kati ya maamuzi magumu ambayo yanaweza kufanywa na mwanaume yeyote.

Ila mchumba wako naye kuzingua Sana jamani.Inaonekana alikuwaga na back up ya mwanaume mwingine na alikuwa anakusubiri uzingue tu kidgo afu ye asepe mazima.
 
Likely,,,
 
Tarehe 20 ya mwezi huu niliahidi kwenda kutoa mahari ukweni kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano.

Niliazimia kufanya hivyo baada ya kukaa na mchumba wangu kwa zaidi ya miaka miwili sasa katika mahusiano. Baada ya kutoka safarini wiki iliyopita, nilishikwa na simanzi sana.

Nilimuona rafiki yangu wa karibu wa siku nyingi ambae alikuwa msaada kwangu toka tukiwa shuleni. Physics, chemistry na maths nilifaulu kwa sababu ya uwepo wake.

Nimetafakari mno na hatimaye, jana nilimueleza wazi mchumba wangu kwamba siwezi kuendelea na zoezi la utoaji mahari kwao kwa sababu kuna mtu ambae nahitaji kumshika mkono aondokane na magumu yanayomkabili kwa sasa.

Alisema hakuna shida na kisha kuomba kuvunja uchumba wetu. Sikuchukua muda tena kulifikiria hilo. Nimekubali na kumtakia kila la kheri katika maisha yake mengine.

NITASIMAMA NA RAFIKI YANGU!
Huyo rafiki yako ni jinsia gani? Tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom