Tarehe 20 ya mwezi huu niliahidi kwenda kutoa mahari ukweni kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano.
Niliazimia kufanya hivyo baada ya kukaa na mchumba wangu kwa zaidi ya miaka miwili sasa katika mahusiano. Baada ya kutoka safarini wiki iliyopita, nilishikwa na simanzi sana.
Nilimuona rafiki yangu wa karibu wa siku nyingi ambae alikuwa msaada kwangu toka tukiwa shuleni. Physics, chemistry na maths nilifaulu kwa sababu ya uwepo wake.
Nimetafakari mno na hatimaye, jana nilimueleza wazi mchumba wangu kwamba siwezi kuendelea na zoezi la utoaji mahari kwao kwa sababu kuna mtu ambae nahitaji kumshika mkono aondokane na magumu yanayomkabili kwa sasa.
Alisema hakuna shida na kisha kuomba kuvunja uchumba wetu. Sikuchukua muda tena kulifikiria hilo. Nimekubali na kumtakia kila la kheri katika maisha yake mengine.
NITASIMAMA NA RAFIKI YANGU!