Maseto
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 944
- 545
Nilinunua kitabu cha "KUPANDA NA KUSHUKA KWA KIPILIMBA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TISS" kilichoandikwa na Bwana Evarist Chahali.
Kwa kweli lazima nieleze kuwa Mimi nina uchu sana wa kujua masuala ya usalama wa Taifa tangu nikiwa mdogo.Huwa najiuliza kwa nini sipati jibu. Nilikuwa na mategemeo makubwa kujua hasa ni sababu ipi iliyofanya Kipilimba atimuliwe lakini sikupata jibu katika kitabu hicho.
Pia mwandishi anaeleza kwa kujiamini kuwa Kipilimba ni Mkurugenzi wa kwanza wa TISS kutumbuliwa tangu Tanzania izaliwe.Jambo hili siyo kweli. Mwaka 1975 Nyerere alimfukuza kazi Emirius Mzena baada ya kuonekana kuna "uhuni na majungu" kwenye idara.
Lakini pia Dokta Kitine anasimlia kuwa alitimliwa mwaka 1980 na nafasi yake kuchukuliwa na mhehe mwenzake Dokta Mahiga. Kitine alieleza sababu za kutimliwa kuwa ni kununua gari bila kumtaarifu Mwalimu jambo ambalo lilitafsiriwa kuwa alikwepa kulipa kodi na aliiba pesa ya mwajiri wake.
Evarist anajitahidi sana kutujuza masuala ya usalama wa Taifa wa Tanzania, lakini napenda kuthibitisha kuwa Rais Magufuli hachukiwi kwa kiasi alichoeleza Chahali. Wananchi wa kawaida wanampenda mno Rais Magufuli.