Nimetafakari sana juu ya uwezo wa Askari Polisi

Nimetafakari sana juu ya uwezo wa Askari Polisi

Charliemic

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
602
Reaction score
969
Majuzi lilipotokea tukio la kutupiana risasi baina ya vijana wetu wa jeshi la polisi na bwana Hamza vimenifanya nifikirie saana juu ya uwezo wa polisi katika kulenga shabaha! Hamza alikuwa sehemu ya wazi! Lakini zilitumika risasi nyingi saana na polisi kumshambulia hamza. Mwishowe tulisikia wameuwawa askari 3 (polisi). Huku 6 wakiwa majeruhi!

Mara kadhaa huwa tunapewa taarifa na polisi ya kuuwawa kwa watu wanaosasikika ni majambazi waliokuwa wakijibizana na risasi na polisi. Cha ajabu huwa hakuna polisi anayejeruhiwa au kudhurika. Lkn tukio la hamza linanifanya niwaze mara 2, hawa askari ambao huwauwa wote wanaojaribu kutupiana nao risasi bila ya kudhurika iweje hamza aliweza kuwasumbua vile!? Tena akiwa stationary tena eneo la wazi!

Mtu mmoja tu tena akajeruhi idadi kubwa ya vijana wetu!

Sitegemei eti kuwa watajitetea kuwa walishtukizwa maana kitendo cha askari kwenda armory ukachukua silaha na kuingia doria tafsiri yake ni kuwa upo tayari katika mapambano kwa muda wowote
 
Laana za waPemba hizo zinawaandama polisi,polisi ambao nyakati za uchaguzi wao ndio wanaohesabu, wao ndio wanalinda kura,wao ndio wanaokimbia na masanduku ya kura wakiondoka nayo kwenye vituo, hili tukio limewafariji wapemba vibaya sana.

Kati ya chombo kinachopendwa na wananchi polisi walikuwa nambari wani ila upendo huo polisi wenyewe wameutupa.

Na mara nyingi wananchi wamekuwa wakiwanasihi polisi kuwa nyinyi ni kwa ajili ya watu wote aka vyama vyote kuna leo na kesho, msijiweke kuwa nyinyi ni maccm na kila kitu ni lazima CCM ashinde mtawasaidia kwa hali na silaha mnafikia kuwauwa watu ili muwasimike CCM. Polisi rudisheni upndo kwa kuwa fair bila ya kupendelea wazi wazi pasipo kificho, hili litawagalimu bei mbaya.

Japo tukio limetendwa na mwanaccm mjenzi wa ofisi nzima ya chama cha mapinduzi waliofurahia ni wapinzani wananchi waliohujumiwa na vyombo hivi, Pemba ni sherehe kila nyumba nyuso zimekunjuka.
 
Walikusudia kumpiga miguu ili watunze ushahidi lakini lisasi ilikwenda seemu za sili, si unajua lisasi za polisi wetu zinamaajabu inapigwa juu inaludi chidi kuuwa ntu.

Bila ya aibu unamsikia polisi anasema alipiga lisasi juu.
 
Ukisikia polisi wameua jambazi wakati wanarushiana risasi.

Shika kichwa, fumba macho, hapo kilichotokea, ni kwamba hao majambazi walikamatwa, wakapperekwa sehemu wakawa executed in cold blood, hiyo ndio "modus operandi" ya polisi yetu uongo uongo mtupu
Not all the time
 
Ukisikia polisi wameua jambazi wakati wanarushiana risasi
Shika kichwa, fumba macho,hapo kilichotokea,ni kwamba hao majambazi walikamatwa, wakapperekwa sehemu wakawa executed in cold blood,hiyo ndio "modus operandi"ya polisi yetu uongo uongo mtupu
Unataka kusema kama vile walivyofanya kina Christopher Bageni na wenzake katika lile sakata la kuuwawa kina Sabinus Chigumbi?

Wale wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge?
 
Kwenye matukio ya ujambazi mara nyingi polisi ndio wanatega mtego, majambazi wanakuwa 'surprised'

Kwa Hamza polisi walivamiwa bila kutarajia wala kujiandaa. Kwenye mazingira hayo hata komando anaweza kuuawa.
Unaelewa maana ya komando kweli?
 
nadhani polic wa kwanza walifanyiwa ambush hawakuwa aware. ndipo marehem alijichukulia advantage. ila wangejiandaa kama wanavyoenda kwenye matukio ya kijambaz sidhan kama angetoboa
Na ndiyo inavyotakiwa adui unamsuprise kwa ambush, sio unaenda vitani face2face utapasuliwa mapema Bwashee.

IMG-20210830-WA0000.jpg
 
Mi nadhani hivi vipolisi vya sasahivi pia havina nidhamu. Mara kadhaa unavikuta vimeshika silaha mikononi viko lindo lakini havina tahadhari yoyote.

Muda mwingi vinachati na simunkulikonumakininwa kazi. Ningenshauri Siro azuie polisi kuchati akiwa kazini. Hii inawezekana kuwapatia device za mawasiliano zisizoruhusu mtu kuchati.

Hiki kizazi cha polisi wa miaka ya 1985 kuja mpaka juu huku 90 hamna kitu. Maarifa na umakini mdogo sana.
 
Back
Top Bottom