Kwa dsm kwa mtaji wako huo wa laki 3 anza na biashara ya kuuza matunda sio ule wa kutembeza kwenye beseni ule una una vishawishi vingi toka kwa sisi wanaume unaweza kukutoa kwenye mstari
1)Tafuta location ya barabarani ambayo utaweza kufanya biashara yako...hakuna malipo wala kodi ila wengine hujifanya wanakuuzia nafasi...huwenda akahitaji 20k au 30k itaegemea
2)Tengeneza meza yako ya mbao ambayo kwa bajet yako isiwe kubwa sana maana utakua na kazi kuibeba muda unaoenda kwenye kazi yako na muda wa kurudi...hapa bajet yako isizidi 30k ya hiyo meza
3)Nunua mwamvuli ile mikubwa maana kipindi hiki mvua za hapa na pale hazikosekani bajet yake isizidi 50k
4)Nunua kiti cha kukalia uwapo kazini kwako bajet yako 20k
5) Nenda sokoni nunua mzigo wako wa Matunda...Masoko yenye bei za kutupa ni Buguruni,Ilala,Tandika,Mbagala itategemea na ww ulipo rahisi unaweza fika wapi
6)Matunda ya kuanza nayo Ndizi hizi utachukua nyingi maana zinalika sana kwa dsm,Tikiti maji,Machungwa,Parachichi, vingine utaanza kuongeza kwa kadri utakavyoona...kwa kuanzia matunda yote hayo bajet yako isizidi 50k
Pesa itakayobaki iweke sehemu salama wakati unaangalia ulichoanza nacho