Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu...

Kama ni biashara kwanza wapaswa kujua eneo lako vizuri, pia haiba yako ipo vipi,uwezo wako binafsi,mwisho una connection zipi.

But kuhusu mtaji ulo nao zipo biashara nyingi unaweza ukafanya na zikakupa kula kuzuri.

Mi binafsi naweza kukushauri upate balow la nguo za watoto/ au viatu, kwa iyo ela unaweza fanya bila huitaji wa frame pia zipo nyingi tuu naweza kukushauri kama utakua ready.
 
nenda kaliakoo,ununue vyombo vya ndani,nguo za kawaida,nguo za ndani, mashuka uwe unakopesha wenzako, au ukopeshe wafanya biashara wadogo wadogo mitaji midogo midogo mf 30 n.k.

Tengeneza juis uwe una sambaza maofisini n.k,anzisha genge la matunda mbogamboga,kaanga mihogo mf shuleni stendi,anzisha mama ntilie n.k.

Mbona mawazo yako mengi tu
 
Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu...
Anzisha page ya udalali.... unaweza anzia watsap status....watu wanaouza vitu unavi post unaweka na bei yako...
 
Unasema tu 300k na hatuioni huku bar mmmnh inasikitisha sana..... nipo na mtt mwenzako hapa nae anasema amejenga nyumba na tupo bar nimemwambia akaifunge nyumba matairi aje nayo bar maana mi nipo stim kichwani ndo maana mwandiko upo iv
 
Angalia mtaa wako unahitaji nini au hata mtaa wa jirani kisha anza na hilo,

1. Waweza kuanza biashara ya kukaanga vipande vya kuku, kukaanga samaki, kupika vitafunwa asubuhi na jioni kama vitumbua na sambusa jioni vinalika sana, chapati na maandazi vinalika sana asubuhi....

2. Wewe ni msomi tengeneza vipeperushi vya MENU za bites au vyakula (kama wajua kupika lakini) sambaza kwenye ofisi mbali mbali hadi vijiweni, upate oda uwe unapika chakula/bites nyumbani kwako kisha unawasambazia wateja wako
 
Kwanza Hongera kwakuchukua Hatua kwaajili ya kesho yako",

Pili Hakuna mtaji mdogo,Ila ulicholenga kufungua ndo kinaweza kikubwa kuliko mtaji ulionao",

Cha kwanza kubariana na hali halisi,usilenge vitu vikubwa kwasasa anza kidogo kidogo.

pili na nakushauri usiwaze frame tafuta saiti ya kukodi maeneo yaliochangamka mkubaliane na mwenye eneo kias cha kumlipa kama ni 10000 au 15000 kwa mwezi kisha tengeneza banda lako la mbao na mabati",

Nenda mjini nunua mitumba kwa bei ya jumla mitumba 70000 si haba kuanzia,Nunua yebo na ndala hazina bei sana ni kuanzia 2000 mpk 7000 kwa bei ya jumla kutokana na zilivyo,pia nunua vitu vya urembo kama heleni,cheni,saa havina bei sana afu nenda kafungue banda lako",

Naamin hutokosa chochote kwasiku kila lakheri kwako".
 
Back
Top Bottom