Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Hongera kwa kuwaza mbali
Naona chakula kinalipa kama upo dar tafuta eneo zuri ila sio frame maana utapunguza mtaji.
1. Sasa hivi ni msimu wa mihogo kaanga mihogo weka na visamaki na vikuku broiler unaweza weka na deli ukauza soda baridi

2. Pika chapati na maharage au utumbo either asubuhi na jioni au jioni tu

3. Pika chakula cha mchana sambaza kwenye vijiwe au ofisi

4. Uji point, saga Unga wa lishe vizuri weka hiliki unukie uwe unapika asubuhi na jioni unasambaza kwenye vijiwe au ofisini. Unaweza tengeneza na uji wa mchele kama hujui kajifunze YouTube. Uwe na maziwa kwa atakayehitaji

5. Mtindi point: hii unaweza Pata ubungo pale Kuna kituo cha maziwa asubuhi sana unaenda kujumua unauza reja reja kwa glass unauzia nyumbani au unatembeza kwa vijiwe au ofisini...hii inaweza kwenda sambamba na no 4 hapo juu au ukatafuta frame ukawa unauza maziwa tu yaani fresh na mtindi

NB biashara ya chakula inahitaji usafi wa hali ya juu, plus uchangamfu ila pia biashara Ina tuvituvitu... uwe mtu wa sala kila wakati utatoboa
Labda auze mwenyewe asishirikishe binti,
 
Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu.

Naombeni ushauri japo wa mawazo nifanyie biashara Gani ambayo naweza nikazalisha na kupata walau faida Na baadae hata kurudisha both vilivyopotea.

Nawaza biashara Nyingi Lakin Naona kama mtaji hautoshi. NB: Msiniseme naombeni mawazo mazuri ya kunijenga natamni nisimame mwenyewe kama wengine.

Location nipo Dar es Salaam
Kama upo dar,nunua matikiti,katakata vipande,weka kwenye deli jeupe,uwe unatembeza maeneo ya shekilango,haswa kwenye ofisi za mabasi ya mkoani, au matunda mchanganyiko ya peki kwenye viFungashio, kuna abiria muda wa mchana jua kali wanakula matunda,Nitafute nikupe idea
 
Unasema tu 300k na hatuioni huku bar mmmnh inasikitisha sana..... nipo na mtt mwenzako hapa nae anasema amejenga nyumba na tupo bar nimemwambia akaifunge nyumba matairi aje nayo bar maana mi nipo stim kichwani ndo maana mwandiko upo iv
Mkuu tafadhali naomba usiongeze tena pombe maana kifuatacho ni kumpiga huyo dogo makofi😂😂
 
God be with you dada Violar. Endelea kupambana, you gonna break through.

Saloon yako ulifunga?

-Kaveli-
 
Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu.

Naombeni ushauri japo wa mawazo nifanyie biashara Gani ambayo naweza nikazalisha na kupata walau faida Na baadae hata kurudisha both vilivyopotea.

Nawaza biashara Nyingi Lakin Naona kama mtaji hautoshi. NB: Msiniseme naombeni mawazo mazuri ya kunijenga natamni nisimame mwenyewe kama wengine.

Location nipo Dar es Salaam
Njoo nikuoe,ntakupa mtàji wa milion moja ufanye unachotaka.
 
Kwa hali hiyo inabidi ujiweke kwenye survival mode kwanza kwa six months ukiwa unafanya hizo biashara ndogo ndogo.

Anza na hivi kutegemea na circle yako.

1. Nunua vile vicontainer vidogo vidogo vya plastic ingia sokoni nunua kisamvu, mchicha na mboga zingine za majani ziandae vizuri zipaki vizuri kisha pita maofisini ukiuza huko utapata wateja na utapata connection za kazi na biashara zingine. Watu wengi walioko maofisini ni lazy kujitafutia mahitaji yao lakini pia wana matumizi ya hovyo ya hela hivyo unapata wateja na utajua vitu vipi wanavihitaji zaidi.

2. Kama unajua kupika keki anza kupika keki jiji la Dar ni jiji la Starehe visherehe vidogo vidogo haviishi so unaweza kupata wateja.

3. Uza heleni na vifuniko vya asali japo kuna wenzako wengi sana wanafanya hiyo biashara.
Asante Sana
 
Hiyo hela si haba, naona waungwana wachache wamekushauri vyema kabisa. Una elimu au ujuzi gani?
Mimi ni mwalimu by professional Ila pia ninaujuzi wa marketing nimefany sehm tofauti tofauti
 
Kama ni biashara kwanza wapaswa kujua eneo lako vizuri, pia haiba yako ipo vipi,uwezo wako binafsi,mwisho una connection zipi.

But kuhusu mtaji ulo nao zipo biashara nyingi unaweza ukafanya na zikakupa kula kuzuri.

Mi binafsi naweza kukushauri upate balow la nguo za watoto/ au viatu, kwa iyo ela unaweza fanya bila huitaji wa frame pia zipo nyingi tuu naweza kukushauri kama utakua ready.
Napokea
 
Kwanza Hongera kwakuchukua Hatua kwaajili ya kesho yako",

Pili Hakuna mtaji mdogo,Ila ulicholenga kufungua ndo kinaweza kikubwa kuliko mtaji ulionao",

Cha kwanza kubariana na hali halisi,usilenge vitu vikubwa kwasasa anza kidogo kidogo.

pili na nakushauri usiwaze frame tafuta saiti ya kukodi maeneo yaliochangamka mkubaliane na mwenye eneo kias cha kumlipa kama ni 10000 au 15000 kwa mwezi kisha tengeneza banda lako la mbao na mabati",

Nenda mjini nunua mitumba kwa bei ya jumla mitumba 70000 si haba kuanzia,Nunua yebo na ndala hazina bei sana ni kuanzia 2000 mpk 7000 kwa bei ya jumla kutokana na zilivyo,pia nunua vitu vya urembo kama heleni,cheni,saa havina bei sana afu nenda kafungue banda lako",

Naamin hutokosa chochote kwasiku kila lakheri kwako".
Asante Sana be bless
 
Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu.

Naombeni ushauri japo wa mawazo nifanyie biashara Gani ambayo naweza nikazalisha na kupata walau faida Na baadae hata kurudisha both vilivyopotea.

Nawaza biashara Nyingi Lakin Naona kama mtaji hautoshi. NB: Msiniseme naombeni mawazo mazuri ya kunijenga natamni nisimame mwenyewe kama wengine.

Location nipo Dar es Salaam
1. Laki tatu ni mtaji tosha. Tafuta ofisi ambayo hawana mgahawa wala huduma ya chakula. Ongea na HR wao, chukua order ya chai na chakula. Unakuwa na jiko pamoja na vyombo. Asbuhi unawapelekea chai na mchana chakula.
2. Unaweza pia kuanzisha kijiwe cha supu na chapati
3. Karanga pia sio haba, unakaanga na kuuza
4. Unaweza pia kuongea na watu wa saloon, wewe unachukua rasta na kuwapitishia kila saloon
5. Skonz pia zinalipa, unatengeneza na kusambaza madukani
6. Biashara vijora pia sio ndogo
7. Unaweza kuagiza korosho mtwara kwa bei ya jumla na kuziuza rejareja
8. Kuna kutengeneza sabuni za maji na kuuza pia.
Yaani huo ni mtaji mkubwa sana
 
Back
Top Bottom