Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Samahani kwa majibu uliyopewa , kwa changamoto unayopitia kiasi cha kuuza simu na radio hukustahili kupewa maneno haya ya dhihaka ila usikate tamaa katikati ya upuuzi mwingi ulioandikiwa wapo wachache waliokupa ushauri mzuri zingatia hayo.
 
Njoo nikuuzie nguo,bei rahisi sana blauz nitakuuzia 2500,surual za kike 5000 kama una acc ya Facebook na Instagram nitakuelekeza kulipia matangazo.tayari utakuwa unarun duka online
 
Elimu yangu wewe na ukoo wenu wote hamuwezi kuifikia hata nusu yake.

Shule kwangu haijawai kuwa tatizo.

Na ndiyo maana sio mod.

Mod hawezi kuwa mtu mwenye akili finyu kama wewe.

Kwa Biology uliyosoma form Two C sio?Wacha muda uzungumze.
 
Umesimamia kwenye faida zipo nyingi,mbona hauzitaji.
Nimeshataja.

Ni wewe tu umeamua kutoiona.

Nimesema faida ya kwanza ni kupata mtaji kupitia mahari atakayopewa na mumewe.

Fikiria mtu atakaemuoa ampe mahari ya milioni tano je ni faida au hasara kwake?

Kumbuka mahari ni pesa ya anayeolewa hata mzazi wake hausiki nayo.
 
Mbio zako fupi mbona,siku sio nyingi utakuja sema hapa matusi sio dili
Dogo nimejiunga JF 2015.

Huu ni mwaka wa 8 sasa sijawai kutishwa nikatishika.

Ulichoandika ni kile waswahili wanaita dua la kuku halimpati mwewe.
 
Inategemea umejifunza nini katika maisha
Mapishi? Kama bites
Kwa kweli sijui kingine kwa mtaji huo
 
Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu.

Naombeni ushauri japo wa mawazo nifanyie biashara Gani ambayo naweza nikazalisha na kupata walau faida Na baadae hata kurudisha both vilivyopotea.

Nawaza biashara Nyingi Lakin Naona kama mtaji hautoshi. NB: Msiniseme naombeni mawazo mazuri ya kunijenga natamni nisimame mwenyewe kama wengine.

Location nipo Dar es Salaam
Hongera sana dada yangu, huwa napenda sana wanawake wanaofanya kila juhudi njema kujikomboa.
Hio laki tatu ulio nayo ni nyingi mno unauwezo wa kukufikisha sehemu hutaamini.
Wengi wetu tulianza na robo ya hio na tupo sehemu tunadhubutu kusema asante Mungu.

Binafsi huwa naamini katika shuguli au biashara ya mfumo wa kuzalisha na kuuza, kuliko kununua na kuuza.

Unapozalisa unajiweka katika nafasi ya kukua na kujenga msingi wa biashara inayo dumu.

Naomba nitoe mifano mdogo , kwa vile umesema upo dar, unaweza kutafuta bonde au sehemu unayo weza kulima mboga, kwa hiyo hela inatosha kikamilifu, utalima mboga zinaweza kua za aina yoyote, zikisha fikia wakati wa kuvuna unazinua kama vile ungenunua kwa mtu au mkulima mwingine, unaenda kuuza kwa bei iliyopo sokoni, hapo unaweza ukawa umetengeza faida mbili,na kwa mwendo huo unaweza siku ukajikuta upo mbali sana, kumbuka pia mboga karibu zote hakuna zinazo vuka miezi miwili.

Unaweza pia ukaanzisha biashara kuchoma vitu, mfano mihogo ya kuchoma, mahindi ya kuchoma, ndizi za kuchoma, viazi vya kuchoma nyama na kadhalika, yaani pasiwe na kitu cha kuchemsha wala kukaanga ni kuchoma tu.
Mwanzo inaweza kuwa na ugumu kidogo lakini baada ya muda itazoekeka na itakua sehemu amazing sana.

Unaweza pia kuvunja mwiko, mfano kijiwe cha kahawa mara nyingi kinahudumiwa na wanaume, sasa ukifanya wewe mwanamke unaweza ukafanya biashara kuliko unvyo dhani , kuandaa kahawa na tangawizi na kashata unaweza ukajifunza kwa muda mfupi na hio hela ulio nayo unaweza kufika mbali sana.

Unaweza pia ukatafuta sehemu yenye mzunguko wa watu wengi ukaweka meza ukawa unauza vitu kama mwiko wa kupikia, fagio za Chelewa vibao vya chapati, viboksi vya kuhifadhia hela au vibubu, Vigari vya watoto, stendi za friji,vigoda enga za kutundika nguo nk, kwa hela ulio nayo ukaenda kwa fundi local akakuelekeza aina za mbao za kununua then anakuchongea hivyo vitu , ukamlipa kiasi natumaini utafanya biashara na utakuwa Brand kubwa.

Yote nakutakia kufanikiwa ndugu yangu, kumbuka Mungu huibariki nia njema, jitihada hazizidi kudra, hivyo sambamba na unavyotafuta cha kufanya uwi hivyo kwa kumtegemea Mungu na kuweka nia njema, Asante.
 
Nimeshataja.

Ni wewe tu umeamua kutoiona.

Nimesema faida ya kwanza ni kupata mtaji kupitia mahari atakayopewa na mumewe.

Fikiria mtu atakaemuoa ampe mahari ya milioni tano je ni faida au hasara kwake?

Kumbuka mahari ni pesa ya anayeolewa hata mzazi wake hausiki nayo.
[emoji23] achaga mawazo ya ki kabudi kabudi mkuu
 
Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu.

Naombeni ushauri japo wa mawazo nifanyie biashara Gani ambayo naweza nikazalisha na kupata walau faida Na baadae hata kurudisha both vilivyopotea.

Nawaza biashara Nyingi Lakin Naona kama mtaji hautoshi. NB: Msiniseme naombeni mawazo mazuri ya kunijenga natamni nisimame mwenyewe kama wengine.

Location nipo Dar es Salaam
Mkuu
Kwa mtaji huo wa laki 3 fanya hivi

Jichanganye kariakoo uwe winga kwa mtindo huu ufuatao

Fungua account ya instagram, thread, twitter, facebook na whatsapp
Afu facebook jiunge kwenye magroup ya machimbo ya kariakoo, yapo mengi we jiunge yotee

Chagua bidhaa ambazo utakuwa unauza mfano
Nguo za kike
Za kiume
Track suit
Electronics
Dawa za binadamu
Furniture
Vyombo
Urembo
Nk
Chagua kimoja base nacho

Ila mi nakushauri u deal sana na viungo vya chakula

Nenda kwenye maduka yanayouza jumla wambie unataka kuwa winga kwahyo watakuwa wanakupa picha unapost kwenye mitandao yako hiyo yoote

Afu unajitangaza kupitia ads ya kulipia
Na magroup ya FB yanawateja wengi ila chunga kuna utapeli mwingi pia

Ukipata mteja wa delivery unachukua kitu dukan unalipa nusu Afu unampelekea mteja,akikulipa unaenda kulipa dukani

Hii biashara inapesa za haraka
Kwa situation YAKO ni bora uanze na biashara itakayokupa pesa mapema kuliko za kusubiri

Ila uwe mwaminifu sana utajenga jina na kukuza mtaji fasta coz wateja wengi ni wamikoani watataka uwatumie mzigo
Ukileta utapeli ndio unajimaliza kibiashara

NB; kwa ishu hii hakikisha unashinda kariakoo hapohapo mda mwingi

Kupitia hiyo laki 3 yako sidhan km utafeli

Kama hii ni ngumu sema nikupe nyingine
 
Yes naona watu wenye positive mindset wamejitokeza sasa kupitia huu uzi watu wengine wananufaika kwa namna moja au nyingine,hatujuan kwa sura wala majina halisi but jamii forum imetukitanisha nimeshawahi saidiwa na mtu humu wala hatujuan na hata sasa hatujawahi onana ni ubinadam wa hali ya juu sana
 
Back
Top Bottom