Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu.

Naombeni ushauri japo wa mawazo nifanyie biashara Gani ambayo naweza nikazalisha na kupata walau faida Na baadae hata kurudisha both vilivyopotea.

Nawaza biashara Nyingi Lakin Naona kama mtaji hautoshi. NB: Msiniseme naombeni mawazo mazuri ya kunijenga natamni nisimame mwenyewe kama wengine.

Location nipo Dar es Salaam

Pole sana binti, kila la kheri kwenye mapambano yako.
 
Mawazo umepata, ukifanikiwa kuanzisha biashara yoyote kabla ya mwaka kuisha, nicheki PM nikithibitisha, nitakuunga mkono kwa kununua na pia kukuongezea Bonus ya 100k kwenye mtaji wako. ✌️
 
Binti tafuta eneo dogo ununue matunda uuze kwa kukata vipande vidogo vya 500 kwa 200.

Unaweza kununua tikiti, embe, chungwa nanasi n. k.

Ukifanya hiyo biashara unaweza ukapata mwangaza wa kujiongeza na kukaanga mihogo nk kadiri utakavyoona inafaa.

Anza kidogo kidogo kwa sababu mwanzo mgumu na hakuna kazi wala biashara rahisi
 
Kama upo Dar es salaam fanya biashara ya matunda. Weka meza barabarani, barabara hizi kuu za lami na uuze.
Maembe
Machungwa
Ndizi
Parachichi

N. K

Pia unaweza kuwa unauza tangawizi zilizosagwa na ndimu iliyokamuliwa.

Watu wengi Dar wamenenepeana siku hizi wanafanya sana diet za mchongo wapungue. Tumia kama fursa.
 
Sijawahi kukutana na mjinga Kama wewe 🥺 jitambue mkuu acha mawazo ya kipumbavu jaribu kushirikisha ubongo una mikono yako ili utambue unachoandika
Wewe ndiye mjinga wa kwanza.

Hujui tu.
 
Kwa mtaji huo, usitoke nje ya biashara ya vyakula...
Uza matunda
Uza vinywaji
Uza chakula
Tafuta sehem ambayo kuna viwanda..au garage uanze kupiga kazi...
Kama upo kigamboni, maeneo ya kiwanda cha afya kuna viwanda vingine viwili pale pale karibu...fanya reseach yko
 
Jitahidi Sana kuombea watoto wako wasije kuwa na mawazo ya kipumbavu Kama wewe yaishie kwako
Binti mbona unapenda kunifatilia?

Au umehisi wivu nilipomuuliza mwenzio kama anataka kuolewa au la?

Ulitaka nikuulize wewe?
 
Back
Top Bottom