Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?

Labda auze mwenyewe asishirikishe binti,
 
Kama upo dar,nunua matikiti,katakata vipande,weka kwenye deli jeupe,uwe unatembeza maeneo ya shekilango,haswa kwenye ofisi za mabasi ya mkoani, au matunda mchanganyiko ya peki kwenye viFungashio, kuna abiria muda wa mchana jua kali wanakula matunda,Nitafute nikupe idea
 
Unasema tu 300k na hatuioni huku bar mmmnh inasikitisha sana..... nipo na mtt mwenzako hapa nae anasema amejenga nyumba na tupo bar nimemwambia akaifunge nyumba matairi aje nayo bar maana mi nipo stim kichwani ndo maana mwandiko upo iv
Mkuu tafadhali naomba usiongeze tena pombe maana kifuatacho ni kumpiga huyo dogo makofi😂😂
 
God be with you dada Violar. Endelea kupambana, you gonna break through.

Saloon yako ulifunga?

-Kaveli-
 
Njoo nikuoe,ntakupa mtàji wa milion moja ufanye unachotaka.
 
Asante Sana
 
Hiyo hela si haba, naona waungwana wachache wamekushauri vyema kabisa. Una elimu au ujuzi gani?
Mimi ni mwalimu by professional Ila pia ninaujuzi wa marketing nimefany sehm tofauti tofauti
 
Napokea
 
Asante Sana be bless
 
1. Laki tatu ni mtaji tosha. Tafuta ofisi ambayo hawana mgahawa wala huduma ya chakula. Ongea na HR wao, chukua order ya chai na chakula. Unakuwa na jiko pamoja na vyombo. Asbuhi unawapelekea chai na mchana chakula.
2. Unaweza pia kuanzisha kijiwe cha supu na chapati
3. Karanga pia sio haba, unakaanga na kuuza
4. Unaweza pia kuongea na watu wa saloon, wewe unachukua rasta na kuwapitishia kila saloon
5. Skonz pia zinalipa, unatengeneza na kusambaza madukani
6. Biashara vijora pia sio ndogo
7. Unaweza kuagiza korosho mtwara kwa bei ya jumla na kuziuza rejareja
8. Kuna kutengeneza sabuni za maji na kuuza pia.
Yaani huo ni mtaji mkubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…