Nimetapeliwa/kuibiwa kiboya sana, ilinibidi nicheke tu. Jifunze hapa

Nimetapeliwa/kuibiwa kiboya sana, ilinibidi nicheke tu. Jifunze hapa

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kwanza nikiri kuwa February 2023 haikua nzuri sana kwangu maana ile 5 February 2023 nilikua safarini, jamaa wakapita na bag la laptop. Lilikua na vitu kibao....hio tuache!

Siku chache kabla ya Safari yangu ya Mkoani, nilifika Sinza Makaburini nikitokea shekilango. Kuna Traffic Lights za kizushi pale. Nataka kukunja nitokee Mlimani City gahfla akaja kijana wakati tumeruhusiwa kwenda akaniambia tairi zimeisha ila anauza tairi mpya.

Nikaondoa gari nikapinda kushoto nikasimama pale Mwika Social Hall. Akaja tukaongea akanipa price yake kuwa ataniuzia kwa 150,000 Kwa Kila tairi.

Nikamjulisha kuwa muda ule Sina pesa na natakiwa kusafiri ila nikirudi nitamtafuta, basi tukaishia hapo.

Akawa ananicheki mara Kwa mara, nikarudi Dar huku nina majanga ya kuibiwa PC na vitu vingine kwenye bus, akawa anapiga Kila mara nikimwambia sina pesa hanielewi.

Mwishoni mwa February nilikua nimekaa mahali Kuna kazi nilikua nafanya, akapiga kwa namba nyingine, nikapokea akaniambia amepewa mzigo wa kusambaza (tairi) kwahio alikua ananicheki kama Niko poa nimtoe anipatie tairi.

Ili kumkatisha tamaa nikamwambia sina pesa ila Nina 150,000 kama anaweza kunipa, nikijua kuwa atasema HAPANA.

Akasema poa, dah ikabidi nitoe ile pesa nikatafuta boda nikamtuma maana nilikua busy, boda akaenda akampa pesa akapewa tairi mbili zimefungwa akaja nazo.

Dah kesho asubuhi nikaenda kwa jamaa anibadilishie tairi, lahaula! Ni tairi zimechoka kabisa hazifai, na zilikua size 15 wakati juu wameweka karatasi ya size 17/265 .

Basi mchezo ukaishia hapo hata sikutaka kumtafuta tena. Kuweni makini kununua tairi mtaani.
 
Ndiyo maana nakwambia hujatapeliwa wala kuibiwa, hujataka kumtafuta tu.

Unajuaje kwamba hakukufungia mzigo kimakosa mzigo wako akauweka pengine na mzigo aliotaka kuutupa akakuletea wewe?

Mtafute umuulize angalau.
Hahahhaahhaa Hahahaaa ndugu yaani itakua kama Jamaa mmoja aliibiwa gari akaenda kuitafuta chumbani
 
Chai nzito halafu haina sukari. Uliibiwa kwenye basi wakati ulikua unasafili na private. Ulimwambia 150 ili akatae wakat yy ndio bei yake
 
Back
Top Bottom