Nimetapeliwa na mtu aliyejitambulisha kama afisa Mikopo Mo Dewji Foundation

Joined
Apr 7, 2016
Posts
9
Reaction score
22
Nimetapeliwa na mtu aliyedai ni afisa mikopo wa Mo Dewji Foundation kwa kunilaghai nikope mikopo nafuu Kwa riba ndogo, ila nitoke dhamana ya asilimia 10. Nilitoa shs 35,000 na kulipa katika namba 0789 223 590 (Khatibu Khamis) na kuahidiwa kupewa mkopo wa shs laki 3, ndani ya muda mfupi.

Baada ya muda mfupi nililetewa meaeji ikinitaka niongeze Tshs 47,000 Ili itumike kufungua account ya mkopo na itareshwa pamoja na mkopo.

Mimi nimkopaji wa mitandaoni hivyo nilijiridhisha. Namba ya afisa imesajiliwa na Nida na ana kitambulisho cha hiyo taassisi daiwa.

Baada ya kujiridhisha kuwa nimeibiwa nilipiga simu kwa mtandao wangu (halotel) na wakaniambia hela imeshatolewa na kukata simu.

Maswali yangu
1) Jina la taassisi ni kubwa , je muhusika hana habari ya jina lake kutumika vibaya?
2) Kama kujiaminisha muhusika alinitumia video ya Mo akiinadi taasisi yake.
3). Hawa watu naweza kusaidiwaje na vyombo vya usalama kurudishiwa hela yangu?

Soma Pia:



 
Hiyo picha ya afisa mikopo ni ya mnigeria huko😂😂😂😂😂😂😂

Ila wewe jamaa unatia huruma. Yani unataka mkopo halafu unalipishwa. Ungewaambia hiyo pesa ya dhamana waikate humo humo kwenye mkopo.

Halafu ukute Bw. Khamisi yupo zake humu JF anacheka saa hizi.

Na ulivyo zwazwa kwenye hiyo screenshot yako umeweka mpaka anuani yako ya makazi. Yani sasa hivi JF yote inajua namba ya nyumba unapoishi😂😂😂.

Hapo umemuandikia Bwana Khamisi kuwa umeongea na Mo, vipi hajakupa mrejesho bado😂😂😂😂😂😂😂😂.

Nakuvutia picha ulivyokuwa unasubiria laki 3 yako toka kwa Bw. Khamisi👇



Nitumie 5000 nikuunganishie mkopo wa laki 5😂😂
 
Watu wajinga ka wewe ni faida kubwa sana Kwa matapeli,tuma hiyo elfu 47 upate mkopo wako,hofu Yako nini?
 
Tanzania mabongo zozo ya kuyatapeli hayaishi yani unapiga pesa kama utakavyo... ukishirikisha akili kidogo tu utajua kuwa sijui tulia foundation, sijui mo, sijui nandy supermarket ni utapeli. shirikisheni akili zenu.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Halafu matapeli wengi hawajui kuandika wanakwambia subilii[emoji1787][emoji1787]
 
Unawezaje kumuamini mtu ambaye hawezi kutofautisha R na L kwenye serious conversation kama hiyo? Kwa namna yeyote ile, nilishafutilia mbali kutuma pesa kwa mtu yeyeto bila kupata ninachotaka. Iwe huduma au biashara, sheria yangu ní hiyo, fikisha mzigo au huduma nikulipe hutaki basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…