Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Ni hivi huyu mwanamke aliishatarakiana na mumewake (ambaye ni marehemu) na baada ya taraka waligawana nyumba na viwanja....na kabla hajafariki alikuwa ni mstaafu na aliwagawia wanae urithi (fedha) na hivyo kila mmoja ana maisha yake kivyake ila siku ya kuuziana kiwanja walikuwepo watoto wake wawili tu kati ya wanne
 
Unatoa maelezo mazuri sana lakini watanzania hawaelewi. Haya mambo ya kuhusisha mabalozi wa nyumba kumi kumi, wenyeviti wa mitaa au vijijini yapo sana. Na mbaya zaidi huwa wanachaji fedha nyingi sana. BTW kuhusu utapeli wa viwanja au nyumba hata serikali haiwezi kukwepa lawama. Nina uhakika wakiweka taratibu nzuri utapeli utapungua kwa kiasi kikubwa.
 

serikali ya kijiji /mtaa wanakosaje nguvu kwenye kuhalalisha mikataba ya mauziano kama majirani au kama wanahusika na mtaa/kijiji husika
 
[emoji106]
 
serikali ya kijiji /mtaa wanakosaje nguvu kwenye kuhalalisha mikataba ya mauziano kama majirani au kama wanahusika na mtaa/kijiji husika
Sio suala la kubishana, ila kwa sheria ya ardhi ya Tz, haiwatambui hao kuwa wanaruhusiwa kisheria kusimamia mauziano ya ardhi hasa baina ya mtu na mtu.kama una bishana na sheria sawa.wale ni hiyo sio kazi kazi bali zile 10%tu za mauziano ndio zinawafanya afanye kama ni jukumu lao, lakini utakapo tokea mgogoro wowote ule wa kisheria hawana uwezo wa kukusaidia kwa makaratasi yao hayo.
 
Kama ni hivyo relax, endelea kula maisha. Hapo hata hao wanae wasingekuwepo kabisaaa ni sawa tu maana umeuziwa na mmiliki halali.
 
Hela inatafutwa mkuu poke sana Ila umejifunza
 
Kama hauja ikopa piga moyo konde ili maisha mengine yaendelee
 
Mkuu vp kama umetumia mwanasheria na ujumbe wa mtaa bila kuhusisha serikali ya mtaa?
 
Kama ni hivyo relax, endelea kula maisha. Hapo hata hao wanae wasingekuwepo kabisaaa ni sawa tu maana umeuziwa na mmiliki halali.
Daaaah afadhar.....tena kesho napeleka trip mbili za mawe ya msingi
 
Mkuu mimi hapa ninaamini na nitazidi kuamini kuwa utapeli katika viwanja kwa zaidi ya 85% unachangiwa na sisi wenyewe wanunuzi. Mkuu mimi ni mwanasheria, ila nikwambie ukweli kabisa kuna wateja hamshaurikiiii hamtaki kusikiliza ya wataalamu na mwisho wa siku mnapigwa.
Mfano, mteja anatafuta kiwanja anaona dalali amepost. Baada ya hapo anaenda kuona kiwanja, dalali anatia maneno ya kuonesha kuwa wengi wanahitaji kiwanja hicho, anamleta mtu ambaye anadai kuwa ndiye mmiliki(kumbe ni msimamizi tu wa familia na sio mmiliki). Mnaenda kwa mwenyekiti wa mtaa anakula 10% dalali anakula % yake halafu mnaandikishana pale kisha mnampelekea wakili makaratasi yenu kuwa 'AWAGONGEE MUHURI' mna laki 5πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wakili anakuuliza kama umefanya utafiti kuwa hakuna shida yoyote? Unajibu ndioooo na mwenyekiti ametuthibitishia, wakili anakwambia kama umejiridhisha basi hakuna shida(huku akitabasamu) maana hata akikukatalia utaenda kwa mwingine na unaweza kukutana na karani wake akagonga huo muhuri kwa laki 2.
Kinanuka baadae ndio unatambua kuwa dalali na mwenyekiti hawatambuliki kwa namna yoyote katika mikataba ya ardhi binafsi, unamfuata wakili anakukumbusha maswali ya siku hiyo na mwisho wa siku hata kesi yako hawezi kuisimamia mahakamani tena unabaki kumuachia Mungu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu vp kama umetumia mwanasheria na ujumbe wa mtaa bila kuhusisha serikali ya mtaa?
Mkuu, kisheria anayetakiwa kusimamia mauziano ya ardhi binafi hapa nchini ni WAKILI na HAKIMU, hao ndio wapo na mandate ya kuweza kuandaa mikataba hiyo na kukuelekeza taratibu sahihi, kuna mauziano ya ardhi yalibatilishwa na mahakama kisa tu stamp duty haikulipwa na hiki huwa hakifanyiki mkiuziana huko kwa mtendaji.
Huyo mtendaji awe kama shahidi wala hulazimishwi chochoteee yeye kuwepo kwenye list ya mashahidi ama yeye kuidhinisha mauziano ya ardhi bali WAKILI ndio mwenye nafasi hiyo mkuu. Kuna mahali kuna uzi niliwahi kueleza haya wakasema tunataka hela na kutangaza biashara na mtu akanusurika kupigwa akanishukuru palepale kwenye uzi.

Tuzingatie taratibu maana siku hizi matapeli wamekua smart kwa hiyo ikitokea upenyo kidogo tu umekwishaa
 
Hivyo ndio waganga hua wanawatapeli ukute mganga mwenyewe choka mbaya balaa kosa ajisaidie yeye atoke kwenye umaskini eti akisaidie wewe ulienshinda uwezo
Mganga sio choka mbaya, na mganga hatoi utajiri mganga Ni Kama dalali anakuunganisha wewe (mteja) na majini (ndo wanatoa utajiri) mganga anahitaji pesa Kama malipo yake lakini majini hayahitaji pesa maana yanazo nyingi tuu!yenyewe yatahitaji ufate masharti ambayo utaelekezwa na mganga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mwanasheria? Sio kaa tunabishana ukiweka hiyo perception tunakua hatujifunzi, haya swali langu ni hivi nguvu yao ni kwenye ushahidi kwanini useme hawana kitu juu ya sheria ya ardhi? Mauziano bila shahidi mkataba unakuaje hapo sio valid, ila pia mawakili wanaweza pitisha mikataba kisheria lakini hawajui background ya hiyo ardhi
 
Ahsante,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…