Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Daaah, Kumbe kweli humu wana Kulanaa??
Aje Mdada Mmoja basi PM tuya Jengeee
 
Wee huna akili,MTU mmejuana mtandaoni,haja kupeleka kwao,wala ndugu zake huwajui labda...then unagawa mbususuu pekupeku bila kinga...
Mkuu unamsimanga mwenzako kwenye matatizo sio poa,wanaume huwa wanakuwa na nguvu kubwa Sana ya kushawishi chochote kwa mwanamke....usitoe kauli Tata.
 
Nachofaham huyu mtu alishasaidika muda sana

Alipata mtu humu humu na akampa mchongo wa kazi na anapiga kazi
Ushuhuda alitoa
 
Wee huna akili,MTU mmejuana mtandaoni,haja kupeleka kwao,wala ndugu zake huwajui labda...then unagawa mbususuu pekupeku bila kinga...
Ila kwer saiv mmbo raisi pesa. Mbele iyo Kinga atakumbuka sangapi
 
Watu wa Mungu mpoo?

Mimi ni member wa JF tangu miaka ilopita nimekuja na ID tofauti ili nieleze yaliyonikuta iwe funzo na ushuhuda kwa wengine.

Niliweka post hapa mika ilopita na kwa bahati tu sijui niseme nzuri au mbaya ila Mungu ndio anajua, nikapata mwanaume ambaye tulianza mahusiano ambayo yalikuwa siriazi kidogo.

Baada ya muda tukapanga mipango ya kuanza mikakati ya kufunga ndoa. Na wakati huo huo ujauzito ukawa umeingia kwangu. Sasa tangu nilipomwambia yule mwanaume kuwa nina ujauzito aliniblock simu na namba zote mawasiliano hakuna. Hadi leo amenitelekezea ujauzito. Alichoniambia mara ya mwisho kabla hajanikimbia ni "wewe ulivyobeba ujauzito si ulijua unabeba ujauzito na sina pesa za kukutunza" kwa maana hiyo nipambane na hali yangu mwenyewe.

Kiukweli maisha kwangu yamekuwa magumu maana ujauzito umefikisha miezi saba na siwezi kufanya kazi nilokuwa nafanya hapo mwanzo. Daktari alinisahuri niachane nayo maana ni kazi ya kusimama zaidi ya masaa saba endapo nitapata wateja mfululizo.

Me nimeleta hili janga lilonipata ili tuendelee kuwa makini humu. Tusikurupukie watu sio wote ni wazuri kama tunavyodhani

Pia nimekuja kuomba kwa yeyote anayeweza kuniajiri kwa kazi yoyote ambayo sio ya kusimama muda mrefu kwa muda wa miezi hii mitatu ya mwishoni nina uhitaji wa kazi ili walao nipate pesa kwa ajili ya kujifungua maana sina msaada wowote wa kifedha wala vifaa vya kujifungulia. Sina matatizo yoyote ya afya hadi sasa yatakayonifanya nishindwe kuhuduria kwenye kazi hiyo nitakayoipata.

Kwa vigezo mimi ni mhitimu wa elimu ya kidato cha sita najua lugha ya kiswahili na kiingereza pia ninajua kutumia komputa vizuri. Naahidi kwamba atakaeniajiri hatajuta licha ya kuwa mimi ni mjamzito.

Mungu awabariki sana.

Tulishatoa onyo kuhusu wanaume wa humu ndani, ila wewe ni Dada yetu hatuwezi kukutupa na uncle wetu mtarajiwa.

Ombi:

Muweke wazi huyo barazuli humu.
 
Wee huna akili,MTU mmejuana mtandaoni,haja kupeleka kwao,wala ndugu zake huwajui labda...then unagawa mbususuu pekupeku bila kinga...
Rafiki hii mada ilishamalizwa. Kazi nilishapata maana lengo hasa ilikuwa ni kupata kazi. nilishajifungua tayari na nikimaliza uzazi naendelea na kazi. Alishapatikana mtu mwema huku akani connect na kazi. Kwa hiyo haya maneno ya karaha jitahidi uyahifadhi moyoni mwako. Matatizo yameumbwa kwa wanadamu lisipokukuta kama langu basi linaweza kukuta lingine japo sikuombei. Mungu akutunze na akusaidie sana ili majanga yapite mbali nawe
 
Ila hilo jina unalotumia nilamikakati sana
 
Na mtoto umempa jina gani? Nawaza tu
 
Na mtoto umempa jina gani? Nawaza tu
Kuhusu jina karibu nyumbani. Tule mtori wa uzazi kisha jina utalijua ukifika huku kwetu rafiki. Usiwaze sana njoo pm nikuelekeze uje umuone anko wetu mpya wa JF aliyezaliwa.
 
Back
Top Bottom