Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Best achana na hawa vinyamkera wana stress za maisha, don't give up be strong mama jikaze utafanikiwa mm nachokushauri jitahid upate hata elfu 10 nunua beseni tembeza mihogo mibichi na machungwa kwenye sehemu za ujenzi au bodaboda utauza au nunua trey ya mayai chemsha anza kuzungusha kikubwa kuwa msafi na smart na usikae kwa huruma au huzuni just smile and be happy with anyone utafanikiwa dear.
Ngoja nikupe mfano Kuna dada mmoja alipitia magumu alipata mimba lakin baba hamjui wanaume waliokua nae wakamkimbia alipambana akanunua kigodoro cha shule akawa analala site alilea mimba alipojifungua yule mtoto ni kama baraka maisha yamemnyokea sasa hivi yupo kwake na amepata mme mzuri. Kikubwa muombe Mungu
Asante sana kwa ushauri. Nimeshapata kazi ya kujishikiza kwa wakati huu rafiki yangu yani nina furaha sana kiukweli. Huku jf kuna wakatisha tamaa na watu wazuri pia wapo. Kikubwa nitapambana hadi tone langu la mwisho la damu ili huyu kiumbe aje duniani. Mungu ni mwema
 
Sijatumia ujauzito kama CV wangu. Ukiangalia thread vizuri Cv nimeandika mwishoni kabisa. Elimu yangu nimeiandika na vigezo vingine nitavieleza na kuvithibitisha kwenye interview..
Interview nitafanyia ofisi popote nitakapoelekezwa niende Sir Midabwada. Asante
Mkuu
Umeeleweka Sana JF Ina Watu Tele Utapata Msaada Sahihi
 
Kuna vivulana huu uzi kazi kucheka cheka tu na kukebehi..lakini deep inside walilelewa na mama tu ..shame !.huyu dada atakuja toa iushuhuda Mungu atakavyomwinua
Kabisa. Na ninachoamini ni kwamba ukiona mwanamke yeyote amebeba ujauzito na kupitia shida na kukataliwa ujue kwamba kinachopigwa vita ni kiumbe kilichoko tumboni kinakua kimebeba hatma kubwa ya maisha ndio maana anakataliwa asizaliwe. Kwa hiyo siwezi kumlaumu mtu hapa sio wao ni shetani anataka kukatisha hatma ya kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa... kikubwa tuombeane tu wana jf hii dunia ina mengi na hapa tunapita tu sio kwetu tukumbuke na tujifunze kuneneana na kutamkiana mema.... J2 njema niwatakie
 
Ujumbe mzito sana ...! Ongea na mwanao akiwa tumboni mwambie unampenda na kumthamini
 
Watu wa Mungu mpoo?

Mimi ni member wa JF tangu miaka ilopita nimekuja na ID tofauti ili nieleze yaliyonikuta iwe funzo na ushuhuda kwa wengine.

Niliweka post hapa mika ilopita na kwa bahati tu sijui niseme nzuri au mbaya ila Mungu ndio anajua, nikapata mwanaume ambaye tulianza mahusiano ambayo yalikuwa siriazi kidogo.

Baada ya muda tukapanga mipango ya kuanza mikakati ya kufunga ndoa. Na wakati huo huo ujauzito ukawa umeingia kwangu. Sasa tangu nilipomwambia yule mwanaume kuwa nina ujauzito aliniblock simu na namba zote mawasiliano hakuna. Hadi leo amenitelekezea ujauzito. Alichoniambia mara ya mwisho kabla hajanikimbia ni "wewe ulivyobeba ujauzito si ulijua unabeba ujauzito na sina pesa za kukutunza" kwa maana hiyo nipambane na hali yangu mwenyewe.

Kiukweli maisha kwangu yamekuwa magumu maana ujauzito umefikisha miezi saba na siwezi kufanya kazi nilokuwa nafanya hapo mwanzo. Daktari alinisahuri niachane nayo maana ni kazi ya kusimama zaidi ya masaa saba endapo nitapata wateja mfululizo.

Me nimeleta hili janga lilonipata ili tuendelee kuwa makini humu. Tusikurupukie watu sio wote ni wazuri kama tunavyodhani

Pia nimekuja kuomba kwa yeyote anayeweza kuniajiri kwa kazi yoyote ambayo sio ya kusimama muda mrefu kwa muda wa miezi hii mitatu ya mwishoni nina uhitaji wa kazi ili walao nipate pesa kwa ajili ya kujifungua maana sina msaada wowote wa kifedha wala vifaa vya kujifungulia. Sina matatizo yoyote ya afya hadi sasa yatakayonifanya nishindwe kuhuduria kwenye kazi hiyo nitakayoipata.

Kwa vigezo mimi ni mhitimu wa elimu ya kidato cha sita najua lugha ya kiswahili na kiingereza pia ninajua kutumia komputa vizuri. Naahidi kwamba atakaeniajiri hatajuta licha ya kuwa mimi ni mjamzito.

Mungu awabariki sana.
Aiseee pole sana [emoji119]
 
Pole sana,aliyekutelekeza kazingua sana,alitakiwa ashirikiane nawewe hadi mtoto azaliwe.Makosa yameshatokea,lakini kukata mawasiliano mazima,kwakweli siyo vizuri.Mtoto tarajali,amekosewa pia.Pole,pambana,nina uhakika unapata msaada stahki.
 
Kabisa. Na ninachoamini ni kwamba ukiona mwanamke yeyote amebeba ujauzito na kupitia shida na kukataliwa ujue kwamba kinachopigwa vita ni kiumbe kilichoko tumboni kinakua kimebeba hatma kubwa ya maisha ndio maana anakataliwa asizaliwe. Kwa hiyo siwezi kumlaumu mtu hapa sio wao ni shetani anataka kukatisha hatma ya kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa... kikubwa tuombeane tu wana jf hii dunia ina mengi na hapa tunapita tu sio kwetu tukumbuke na tujifunze kuneneana na kutamkiana mema.... J2 njema niwatakie
double click.
 
Back
Top Bottom