Nimetembea mikoa mingi Tanzania, moja ya mikoa iliyochoka mbaya basi ni Mara

Ukimaanisha Tarime inachangia mapato makubwa hasa kwa madini naweza kukuelewa lakini kinachopatikana hakiendani na maendeleo ya Tarime, ni sehemu iliyochoka
Tarime haiwezi na haitakaa iweze kuchangia mapato makubwa kuliko Arusha....NEVER, aweke hapa rekodi ya mwaka jana tu au miaka mitatu nyuma
 
Tarime haiwezi na haitakaa iweze kuchangia mapato makubwa kuliko Arusha....NEVER, aweke hapa rekodi ya mwaka jana tu au miaka mitatu nyuma
For sure, Arusha kuna viwanda, maduka makubwa, mahoteli, nyumba nyingi sana, biashara kibao, n.k. vyote hivi ni vyanzo vya kodi.

Tarime wanachotengenea zaidi ni madini tu na kwa kiasi kikubwa wanufaika ni kampuni za wazungu ambao wana mkataba tayari.
 
Mapato tu ya Ngorongoro peke yake yanaizidi hayo ya Tarime
 
Kamda ya ziwa ukiondoa Mwanza, Tena Mwanza yenyewe ni zile wilaya mbili kulikobaki kote ni Takataka na hii ni karibia kanda zote nchi nzima kuna umaskini sana miondombinu mibovu sanaaa

Kama Taifa wamekazana na Dar na DOM, Pesa yakujenga Barabara Dar au project yoyote huwa haikosekani kabisa, ila Pesa ya kuungamisha Mtama na Newala hakuna Bunda kwenda Mungumu serengeti kupitia Nyamuswa hakuna, Ukifika Kahama manemo unayosikia inavyosofiwa na ukifika ni ardhi na Mbingu mji umechoka, Katikati ya Dodoma na Singida kuna umaskini wa kufa mtu, Singida Manispaa hapa mjini unaumaliza mji kwa Dakika 3

Issue nchi yetu haina vipaimnele kabisa na miji mingine zaidi ya Dar na DOM!!
 
Umeandika mkoa wa Mara kana kwamba ndo mkoa wa hovyo zaidi Tanzania.. sema ni maoni yako Lazima yaheshimiwe...

Ila kwa uzoefu wangu mkoa wa Mara haujachoka kiasi hicho ulichoandika vinginevyo una chuki zako tu binafsi...

Mi ntazungumiza mambo mawili tu kiuchumi na kijamii

Umesema mkoa wa Mara mzunguko wa pesa upo chini... Lakini reference yako umetumia musoma peke yake je vipi kuhusu wilaya ya Tarime? Ushafika sirari au Nyamongo ? Ukishindwa kutoboa hapo we ndo basi tena...

Hata Kule Musoma mjini fursa zipo kibao tu kuanzia biashara ya Mazao ya majini kama samaki, dagaa na mabondo..

Kuhusu mtu kutahiriwa kwa kisu Kuna mdau kashachangia vyema...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…