Nimeishi Dar, Mwanza, Mbeya, Iringa, Njombe, Tanga, Mtwara, Singida, na Mara, nichukue fursa hii kusema wazi mkoa wa Mara unatia huruma.
- Naweza kusema kwa uhakika ndio mkoa wenye stendi mbovu zaidi nchi nzima, stendi ya Musoma Mjini haina tofauti na kiwanja cha wazi chenye madimbwi.
- Musoma mjini pamepoa sana, mzunguko wa pesa ni mdogo sana, mji mdogo.
-Mkoa mzima hauna chuo chochote wala kampasi inayofahamika kitaifa, chuo kinachofahamika zaidi ni vya diploma kama Musoma utalii college wanachotoa kozi za udereva, upishi, ualimu wa chekechea, n.k. kuna chuo kipo Butiama kinajengwa tangu enzi za kikwete
- Mkoa una Mbuga ya Serengeti yenye umaarufu mkubwa duniani na kutembelewa na watu wengi maarufu lakini mapato yanaenda Arusha, hadi kuna muda watu huwa wanadhani mbuga ipo Arusha, Utalii ni sekta inayoongoza kwa pesa kuzidi hata madini.
- Kielimu bado mkoa upo nyuma, wanaosifiwaga kuelimika mkoa wa Mara ni wakerewe, Ukerewe ipo Mwanza sio Mara, ukitaka kuhakikiha hili fuatilia matokeo ya form 4 shule za Mara, ufaulu ni mdogo sana !
- Kisiasa mkoa upo active zaidi kwenye siasa za upinzani na imekuwa sehemu ya kutoa wanaharakati wengi kwenye mambo ya mabadiliko, ila kwenye siasa za chama tawala ccm bado mkoa upo nyuma, hakuna wabunge wenye vyeo vikubwa au ushawishi mkubwa kitaifa
- Kuna mambo ya kizamani ya kuendelea kuamini uanaume ni kutahiriwa bila ganzi wakati ulimwengu wa sasa unajali zaidi elimu, pesa na nguvu ya kisiasa
- watu wa Mara ni moja ya kundi lenye watu waliofanikiwa mikoa ya nje lakini hawana utamaduni wa kujenga mkoa wao,