Nimetembea mikoa mingi Tanzania, moja ya mikoa iliyochoka mbaya basi ni Mara

Nimetembea mikoa mingi Tanzania, moja ya mikoa iliyochoka mbaya basi ni Mara

Moshi nitaitafutia wiki niende kuicheki vizuri
mzee moshi hamna kitu kimji kimedumaa hakibadiliki majengo ni yale yale kila siku.bora hata wilaya ya siha ina majengo mapya mengi. Mkoa wa kilimanjaro umedumaa. Asusha ukiondoa jiji na meru wilaya zake zote chovu tofauti na mkoa kama mbeya wilaya zake zote zimechangamka kama mbarali chunya rungwe busokelo na kyela mungu kawapendelea hawa watu. Mkoa mwingine wa hovyo kuliko hata mara ni kagera
 
Yaleyale tu, nafuu ipo mjini Ila wilayani huko kugumu. Nenda simanjiro, kiteto au mbulu utaelewa
Ulisemalo kweli.. nimekaa moshi mjomba vumbi la pale moshi qmmk ni hatari.. sasa jaman wachaga wavijijini wanataabika jmn mpk huruma naona mimi 😪😪 CCM waache hii nchi tujaribu wapinzani...
 
Nimeishi Dar, Mwanza, Mbeya, Iringa, Njombe, Tanga, Mtwara, Singida, na Mara, nichue fursa hii kusema wazi mkoa wa Mara unatia huruma.

- Naweza kusema kwa uhakika ndio mkoa wenye stendi mbovu zaidi nchi nzima, stendi ya Musoma Mjini haina tofauti na maegesho ya magari

- Musoma mjini pamepoa sana, mzunguko wa pesa ni mdogo sana, mji mdogo.

-Mkoa mzima hauna chuo chochote wala kampasi inayofahamika kitaifa, chuo kinachofahamika zaidi ni Musoma utalii college wanachotoa kozi za udereva, upishi, ualimu wa chekechea, n.k. kuna chuo kinajengwa tangu enzi za kikwete bado kinaendelea kujengwa hadi leo.

- Mkoa una Mbuga ya Serengeti yenye umaarufu mkubwa duniani na kutembelewa na watu wengi maarufu lakini wakazi wa Mara wamelala kwenye hii fursa, wengi wanaishia kuwa walinzi huku wageni wakichuma pesa nyingi, Utalii ndio sekta inayoongoza kwa pesa nyingi Tanzania kuzidi hata madini.

- Kielimu bado mkoa upo nyuma, wanaosifiwaga kuelimika mkoa wa Mara ni wakerewe, Ukerewe ipo Mwanza sio Mara, mkoa wa Mara hata ukiangalia wabunge wao wengi ni Darasa la saba, form 4, form 6 na Diploma. Ccm ilibidi iiingilie kati kuweka wenye degree na masters angalau mkoa upate wabunge wenye sifa za kushika vyeo vikubwa

- Kuna mambo ya kizamani ya kuendelea kuamini uanaume ni kutahiriwa bila ganzi wakati ulimwengu wa sasa unajali zaidi elimu, pesa na nguvu ya kisiasa

- Vijana wengi wanaofanikiwa nje ya mkoa hawana utamaduni wa kujenga mkoa wao
Utakuwa umepita kitambo kidogo mkoa wa Mara:
1. Musoma mjini walishabomoa ile stendi yote. Kwa sasa panajengwa nyingine
2. Wilayani Butiama kipo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere
3. Tohara ya hadharani bila ganzi ni mila ilianzia kwa Nabii Ibrahim. Hii leo hawa wanaoitwa wabantu (wakiwamo wana Mara wengi) chimbuko lao ni early hebrews-Israelites (search google). Makabila mengi tuu waliifanya bila ganzi
4. Udumavu wa mzunguko wa hela Musoma ni kwa vile sio njia panda kuu na hamna viwanda. Kama umeitembea Tanzania utagundua miji yote ambayo sio njia panda kuu au haina viwanda ina tatizo la mzunguko wa hela
 
Ona hii TAKATAKA!

Wewe wala huufahamu mkoa wa mara wala musoma yenyewe! Stendi ya Bweri Ni stendi bora kabisa, acha kuongelea Stand ya zamani Pale Hussein Sokoni!

Unasema Mara hakuna chuo?! Hapo MUSOMA UTALII COLLEGE sio Chuo hicho?! Ama ni MADRASSA?!

Unasema Umekaa mtwara? ...Umekaa mtwara hata mkoa jirani tu hapo kwa (mamwinyi) LINDI na ufukara uliopo nao hauujui? Ama unajitoa ufahamu?

Bado huaujatembea!
Naijua Mara na Mtwara.
Nasikitika kusema Mara imepitwa mbali sana na Mtwara.
Hakuna wilaya hata moja ya Mara unaweza kufananisha na Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Hapo hujafika Mtwara makao Makuu ya Mkoa.
 
mzee moshi hamna kitu kimji kimedumaa hakibadiliki majengo ni yale yale kila siku.bora hata wilaya ya siha ina majengo mapya mengi. Mkoa wa kilimanjaro umedumaa. Asusha ukiondoa jiji na meru wilaya zake zote chovu tofauti na mkoa kama mbeya wilaya zake zote zimechangamka kama mbarali chunya rungwe busokelo na kyela mungu kawapendelea hawa watu. Mkoa mwingine wa hovyo kuliko hata mara ni kagera
Acha porojo wewe, moshi mjini inabadilika taratibu mno, na hiyo inatokana na tabia ya wachagga na wapare kupendelea kujenga kwenye maeneo walipozaliwa kuliko mjini, pale moshi mjini ni market place, watu wanakuja pale asubuhi na jioni wanarudi migombani kulala, hebu tuambie hao wanaotaabika huko kijijini ni kitu gani wamekosa? Maana sehemu kubwa ya kilimanjaro hasa upande wa juu, hawana shida ya maji, barabara,umeme, chakula, hiyo shida unayoisema wewe ni ipi?
 
sasa wewe mwenyewe ukubali moshi hakubadiliki na mimi nimeandika tofauti na ulicho kiandika?
 
Inasikitisha sana kuona raia wa Mara na wilaya zake zote inawalazimu kupita Mwanza/Simiyu-Shinyanga-Nzega-Singida-Manyara ili kuufikia mkoa jirani yao kabisa wa Arusha hali wangekuwa na lami yao kuingia Arusha bila mzunguko usio wa lazima.
 
sasa wewe mwenyewe ukubali moshi hakubadiliki na mimi nimeandika tofauti na ulicho kiandika?
Nasema moshi mjini inabadilika taratibu, wewe unasema ipo vilevile tokea zamani, nimepita huko miezi miwili iliyopita,

Nimeona majengo mengi tu mapya hali inayoonyesha kuwa mkoa umeanza kuchangamka tena,

Hali ya maisha kwa upande wa vijiji hasa vya uchagani ni nafuu sana kulinganisha ni vijiji vingi vya mikoa mingine, bila hata jitihada binafsi za wakazi wa huko nature inawabeba, kule maji watu wameyakuta tu yanatiririka kutokea juu mlimani huko,

Kuna mtu anasema kuna vumbi sana, hali hiyo ipo upande wa chini ambao wenyeji wa ukanda wa juu hupaita porini, sehemu kama kahe huko vumbi ni nyumbani kwao, sehemu ya Mwanga pia, ila kwa sehemu kubwa hasa uchagani pana nafuu sana.
 
wewe umepita mimi nipo hapa na mda huu nipo kwenye noah naenda rombo kisha tarakea kwa walevi wa mapombe
 
Back
Top Bottom