Nimetembea mikoa mingi Tanzania nimegundua kuwa Dodoma kuna nyoka wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania

Dodoma kubwa mkuu tuambie na maeneo waliopo hao nyoka ili tusiende
 
Wanazidiana kwa idadi, aina na wingi. Mapori mengi ambayo hayana watu wengi yana nyoka wengi. Sehmu kama mkoa wa Kilimanjaro hauna mapori makubwa hivyo nyoka siyo wengi.
Kwa mkoa wa Kilimanjaro ,Nenda wilaya ya same mlima shengena ,utapewa habari za kule, ukiangalia mazingira ya Same hayatofauti sana na dodoma au Tabora,

Same kuna nyoka wa kila aina ,pia kuna Mbuga ya Mkomazi nahisi hili pia linachangia
 
Hujafika tabora ...ndio makao makuu yao wakitoka hapo ndio wanahamia mikoa mingine
 
Huko Nachingwea nadhani kunaweza kuwa kunaongoza kwa Nyoka hapa Nchini.

Wale Nyoka wengi waliletwa na Wakoloni kipindi wanaendesha shughuli za kilimo kwenye yale mashamba yao ya kuanzia farm 1 hadi farm 17 ili kudhibiti panya na wadudu wengine waharibifu wa mazao.

Baada ya Wakoloni kuondoka waliacha wale Nyoka wamezaliana kupita kiasi na kuwatelekeza huko maporini.
 
Duuh!
 
Dodoma ipi me nimekulia na kusomea dodoma ila hao nyoka nimekutana nao mara chache sana pia tuna mashamba kuanzia veyula,mzakwe,zanka na mayamaya kipindi cha kilimo muda mwingi huwa tunakuwa huko lakini ni mara chache sana utakutana na nyoka
Dom hakuna nyoka, nmekaa dom zaidi ya miaka 7 nimewahi kuona nyoka mara moja tu tena kipindi cha masika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…