A
Anonymous
Guest
Mimi ni fundi seremala kutoka Shinyanga Mjini. Mnamo tarehe 17 Agosti 2023, nilipewa kazi na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) wa Shinyanga Mjini ya kutengeneza samani, zikiwemo viti, benchi, meza na rafu za dawa katika zahanati za Seseko na Ihapa.
Thamani ya kazi hiyo ilikuwa jumla ya Sh8,720,000. Hata hivyo, hadi sasa, baada ya kupita miaka mitatu na zaidi, sijalipwa fedha zangu kwa kazi niliyoifanya.
Nimejaribu kuchukua hatua mbalimbali kufuatilia malipo yangu, ikiwemo kuandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya, lakini jitihada hizo hazijazaa matunda.
Hali hii imenikosesha haki yangu ya kupata malipo ya kazi niliyoifanya, licha ya kutimiza wajibu wangu.
Naomba mamlaka za juu zinazohusika ziingilie kati suala hili, zifuatilie malalamiko yangu na kuhakikisha nalipwa fedha zangu stahiki.
Ninaomba haki yangu ipatikane.