NIMETHIBITISHA: Dunia haipo, ni unaota tu!

Fafanua maelezo haya tafadhali.

Unawezaje kusema kitu ambacho hakina uhai kwamba na chenyewe kina dhani kiko "real", unaweza kututhibitisha hili ?
Thought experiment.
Tutumie AI tutengeneze simulation ndani yake tuweke mtu(katuni) ambaye kwenye core program yake aamini kuwa yeye ni mtu halisi na ameumbwa na Mungu na yupo katika dunia hiyo anaishi...halafu kwenye hiyo simulation tuweke character mwingine halafu kwenye core program yake ajue ukweli kuwa yeye yumo ndani ya simulation.. Unadhani akienda kumuambia yule character wa kwanza kuwa yeye sio real atakubali??

Kwamfano kuna tofauti gani ya sisi kuwa real au kuwa ndani ya game ila tukaaminishwa kuwa tuko hai?ila kuna watu wanatucheza??

Kwasasa binadamu tunatengeneza watu ndani ya game lakini wanakuwa made of electronic signals sasa Lets say watu 'halisia'/aliens walikuwepo miaka billioni iliyopita hivyo wakapata technolojia kubwa ya kutengeneza game ambalo watu wake wako kama ndani ya uhalisia yani wana damu na nyama na wanapumua O² kama uhalisia instead of electronic signals..
Hao watu watakuwa wanatuangalia kwenye screen zao jinsi tunavyobishana kuwa tuko real kumbe wanatucheza..

Inshort huwezi kuprove au kudisprove kuwa hii ni reality au simulation..

Inaweza kuwa tumo ndani ya game halafu Mungu na malaika zake ndo walitengeneza game wanatucheza.
 
Kwani wewe unajijuaje kuwa uko 'hai'??
 
Mfano nikikuambia mtu akipanda treni ambalo linakimbia kwa speed ya mwanga na akakaa humo ndani ya treni kwa muda wa wiki moja, siku akishuka baada ya hiyo wiki moja atakuta imepita miaka 100 na watu wote aliowaacha wamshakufa, ila kwake ni wiki moja tu, utaamini au utaona hiyo ni kama ndoto tu? Ila that is the real REALITY!

Dah we jamaa maana ya usafiri wa haraka utakuwa umeipoteza kwa huu mfano wako

Labda useme huyo mtu atakuwa kasafiri umbali ambao ulipaswa utumie miaka 100 yeye akatumia wiki moja

Lakini si kusema atakuta watu aliowaacha wakiwa vikongwe au wamekufa yeye bado akiwa bado ni chalii tu..! Hapo hapana

Mabadiliko ndani ya mwili yanahusiana vipi na kifaa cha usafiri.!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thought experiment.
Tutumie AI tutengeneze simulation ndani yake tuweke mtu(katuni) ambaye kwenye core program yake aamini kuwa yeye ni mtu halisi na ameumbwa na Mungu na yupo katika dunia hiyo anaishi...halafu kwenye hiyo simulation tuweke character mwingine halafu kwenye core program yake ajue ukweli kuwa yeye yumo ndani ya simulation.. Unadhani akienda kumuambia yule character wa kwanza kuwa yeye sio real atakubali??
Naona huelewi unachokiandika. Unajua sifa ya kitu chenye ufahamu ni lazima kiwe na uhai, na kiweze kuelezea hali ambayo kinayo, na sio kitu ambacho ni "progammed". Kitu ambacho ni "progammed" hakina maamuzi wala utashi nje ya vile kilivyo wekewa, yaani hakina "uhuru wa kuchagua wala hakijitambui". Ndio maana hata hiyo "AI" kiuhalisia haipo na haifanyi kazi.

Elezea kwamba ataamini vipi kuwa yeye ni mtu halisi, wakati inajulikana sio mtu halisi ?
Kwamfano kuna tofauti gani ya sisi kuwa real au kuwa ndani ya game ila tukaaminishwa kuwa tuko hai?ila kuna watu wanatucheza??
Tofauti ni kubwa sana, kwanza sisi tuna uhai, tuna uhuru wa kuchagua na kufanya tunachotaka, tuna akili na milango ya fahamu. Hivi vinajenga mwanadamu timamu.
Kwasasa binadamu tunatengeneza watu ndani ya game lakini wanakuwa made of electronic signals sasa Lets say watu 'halisia'/aliens walikuwepo miaka billioni iliyopita hivyo wakapata technolojia kubwa ya kutengeneza game ambalo watu wake wako kama ndani ya uhalisia yani wana damu na nyama na wanapumua O² kama uhalisia instead of electronic signals..
Hao watu watakuwa wanatuangalia kwenye screen zao jinsi tunavyobishana kuwa tuko real kumbe wanatucheza..
Hao hawaitwi watu bali ni wanasesere mtu hatengenezwi, bali mtu anaumbwa.

Hala hutakiwi kuishi kwa dhana, yaani unachofanya wewe ni uvivu wa kufikiria mambo na kutafuta "shortcuts" ambazo hazikupi majibu zaidi ya kujidanganya tu. Tujikite katika matumizi mazuti ya akili na kuutafuta uhalisia.
Inshort huwezi kuprove au kudisprove kuwa hii ni reality au simulation..
Nakuliza swali rahisi ili uone ya kuwa uhalisia upo na si lazima uwe proved yaani kuwepo kwake tu hakuhitaji evidence. Wewe umezaliwa au hujazaliwa ? Hizi
Inaweza kuwa tumo ndani ya game halafu Mungu na malaika zake ndo walitengeneza game wanatucheza.

Hizi ni dhana ambazo huwezi kuthibitisha, kwanini mnaishi kwa dhana wakati uhalisia tuko nao.
 
Kwani wewe unajijuaje kuwa uko 'hai'??
Swali zuri, najijua niko hai kwa mengi sana, kwanza naishi, naona, nahisi nakula,natafakari,nafanya maamuzi, napatia, nakosea, nina ufahamu, najifunza na mengine mengi.
 
Inaonekana wewe huijui AI vizuri..labda hujafatilia..anyway hiyo ni homework yako lakini usiassume kwasababu huijui vizuri eti 'haofanyi kazi'
Umeongea mengi lakini point mbili tu kuwa
Sisi tunatofauti na hao unaowaita wanasesere kuwa sisi tuna
1.uhai 2.uhuru wa kuchagua.

Tuanze na uhuru wa kuchagua.
Wewe unajuaje kuwa una uhuru wa kuchagua? Hata game wale characters ukiwaprograme kufanya kitu wao watahisi walichagua kumbe walikuwa wamepangiwa kufanya hivyo.
Unaweza kuprove kuwa unao huo uhuru wa kuchagua?
Kabla hatujafika mbali unaamini uwepo wa Mungu?
 
Swali zuri, najijua niko hai kwa mengi sana, kwanza naishi, naona, nahisi nakula,natafakari,nafanya maamuzi, napatia, nakosea, nina ufahamu, najifunza na mengine mengi.

"Naona,nahisi,natafakari,nafanya maamuzi, napatia, nakosea, nina ufahamu, najifunza"
Hayo mambo hata AI anafanya

Halafu hayo wewe ndiyo umeyaweka kama definition ya kuwa hai...huenda kuwa hai ni zaidi ya hayo sema wale viumbe walio hai waliotutengeneza walituweka kwenye simulation wakatuaminisha kuwa ili uwe hai inabidi uwe hivyo tu basi...ila kuna vitu hatuna wakituona kwenye screen wanatucheka..
Kwasababu definition ya uhai na uhalisia tumeijenga sisi wenyewe kwenye ulimwengu huu haimaanishi ni universal yawezakuwa kwenye ulimwengu mwingine inamaaanisha vitu vingine kabisa na kwenye ulimwengu wa game kuwa hai inaweza isimaanishe kula na kupumua inaweza kumaanisha uwezo wa kubadilishana code
ila katika ulimwengu huo wao nao wanabishana kuwa wako hai na maana ya uhai na uhalisia ndiyo hiyo

Hatakama tukiassume kuwa hai maana yake ni hayo yote uliyotaja ukiwa sahihi haimaanishi pia kuwa tupo hai 100% yawezekana tumepewa vyote hivyo na aliyetutengeneza kwahiyo kwake sisi sio 'halisi' kama ambavyo tunaona characters tuliowatengeneza kwenye game kuwa sio 'halisi'
Na kila tunachokifanya na kukiona kwenye huu ulimwengu kipo ndani ya screen yake a/waliotutengeneza na huenda a/wameweka baadhi ya vitu kama dini kutupa robo ya ukweli kuwa kuna watu wako nje ya huu ulimwengu wanatucheza kama game kina Allah,Yesu,Budha,Krishna n.k

Hata mimi nawewe tukitengeneza simulation ya kaulimwengu ketu ndani ya computer tunaweza tukaweka mule ndani makanisa ya kutuabudu Mungu citizenB na Mungu Jurjani
wale characters watatusoma na kutuabudu kulingana na code tuliowapa
 
Tuanze na uhuru wa kuchagua.
Wewe unajuaje kuwa una uhuru wa kuchagua?
Sababu bafanya nachotaka muda nao taka.
Hata game wale characters ukiwaprograme kufanya kitu wao watahisi walichagua kumbe walikuwa wamepangiwa kufanya hivyo.
Naona hutaki kuelewa, nakuuliza swali, ili kitu kihisi kinatakiwa kiwe na sofa gani ? Maana naona unaandika bila kufikiri.
Unaweza kuprove kuwa unao huo uhuru wa kuchagua?
Bila shaka kabisa, mpaka nimeamua kujiunga na "jf" hapa nimetumia uhuru wa kuchagua kujiunga na kama ningetaka pia nisinge jiunga "jf". Kadhalila nimechagua kujadiliana na wewe na kinyume chake pia ningeweza kufanya.
Kabla hatujafika mbali unaamini uwepo wa Mungu?
Naamini kabisa bila chembe ya shaka.

Tuendelee....
 
"Naona,nahisi,natafakari,nafanya maamuzi, napatia, nakosea, nina ufahamu, najifunza"
Hayo mambo hata AI anafanya
Thibitisha hili.

Kisha uniambie hayo mambo yanahitaji msingi mkuu upi ?

Roboti ikikosea, wakulamiwa ni Roboti au yule aliyeitengeneza ?
Halafu hayo wewe ndiyo umeyaweka kama definition ya kuwa hai...huenda kuwa hai ni zaidi ya hayo sema wale viumbe walio hai waliotutengeneza walituweka kwenye simulation wakatuaminisha kuwa ili uwe hai inabidi uwe hivyo tu basi...ila kuna vitu hatuna wakituona kwenye screen wanatucheka..
Mzee unaandika vitu vya kufikirika ambavyo huwezi kuvithibitisha. Viumbe ganu vimetutengeneza ? Umejuaje hili ? Kwanini unadhani dhani kama kitu hukijui bora uulize au ukae kimya.
Kwasababu definition ya uhai na uhalisia tumeijenga sisi wenyewe kwenye ulimwengu huu haimaanishi ni universal yawezakuwa kwenye ulimwengu mwingine inamaaanisha vitu vingine kabisa na kwenye ulimwengu wa game kuwa hai inaweza isimaanishe kula na kupumua inaweza kumaanisha uwezo wa kubadilishana code
ila katika ulimwengu huo wao nao wanabishana kuwa wako hai na maana ya uhai na uhalisia ndiyo hiyo
Mzee naona huna hoja zaidi ya kuandika vitu vya kufikirika na dhana, jikite kwenye hoja na kuijenga sio "....huenda.... " mara "....inaweza kuwa.... "
Hatakama tukiassume kuwa hai maana yake ni hayo yote uliyotaja ukiwa sahihi haimaanishi pia kuwa tupo hai 100% yawezekana tumepewa vyote hivyo na aliyetutengeneza kwahiyo kwake sisi sio 'halisi' kama ambavyo tunaona characters tuliowatengeneza kwenye game kuwa sio 'halisi'
Na kila tunachokifanya na kukiona kwenye huu ulimwengu kipo ndani ya screen yake a/waliotutengeneza na huenda a/wameweka baadhi ya vitu kama dini kutupa robo ya ukweli kuwa kuna watu wako nje ya huu ulimwengu wanatucheza kama game kina Allah,Yesu,Budha,Krishna n.k
Jaribu kujenga hoja na kujibu hoja, hizi story za dhana achana nazo, zinakupotezea muda.
Hata mimi nawewe tukitengeneza simulation ya kaulimwengu ketu ndani ya computer tunaweza tukaweka mule ndani makanisa ya kutuabudu Mungu citizenB na Mungu Jurjani
wale characters watatusoma na kutuabudu kulingana na code tuliowapa
Fanya hivyo. Maana ya kuabudu unajua ni nini ? Kisha uyape ufahamu na kuwa huru.
 
Sababu bafanya nachotaka muda nao taka.
Unauhakika kuwa unachofanya ni wewe umepanga au umepangiwa??kwasababu hata characters kwenye game wanafanya mambo kwa kupangiwa ila wao wanadhani ndo wamepanga
QUOTE="Jurjani, post: 35459213, member: 483599"]
Naona hutaki kuelewa, nakuuliza swali, ili kitu kihisi kinatakiwa kiwe na sofa gani ? Maana naona unaandika bila kufikiri. [/QUOTE]hili swali mm ndo nilikuuliza umenigeuzia tena...ila kuhisi ni kurespond to external stimulus... Kitu ambacho hata machine zinaweza

Bila shaka kabisa, mpaka nimeamua kujiunga na "jf" hapa nimetumia uhuru wa kuchagua kujiunga na kama ningetaka pia nisinge jiunga "jf". Kadhalila nimechagua kujadiliana na wewe na kinyume chake pia ningeweza kufanya.
ungeweza lakini hukufanya kwasababu aliyekuprogram hakutaka uache kujadiliana namimi ila amekupa illusion tu kuwa una uwezo wa kuacha ila kiuhalisia unafanyo ulichopangiwa

Naamini kabisa bila chembe ya shaka.

Tuendelee....
ok kama una amini uwepo wa Mungu...je Mungu anaijua future yako?
 
hili swali mm ndo nilikuuliza umenigeuzia tena...ila kuhisi ni kurespond to external stimulus... Kitu ambacho hata machine zinaweza
Hukuuliza swali hilo kwangu.
Unauhakika kuwa unachofanya ni wewe umepanga au umepangiwa??kwasababu hata characters kwenye game wanafanya mambo kwa kupangiwa ila wao wanadhani ndo wamepanga
QUOTE="Jurjani, post: 35459213, member:
Ndio nina uhakika.

Pili, unaposema wao wana dhani bila kuweka ushahidi huu ni utoto na kutumia akili vibaya. Embu mchukue muhusika mmoja umuulize kuhusu hiki unachokidai akikujibu uje kutuwekea ushahidi hapa.
ungeweza lakini hukufanya kwasababu aliyekuprogram hakutaka uache kujadiliana namimi ila amekupa illusion tu kuwa una
Thibitisha hilo.
ok kama una amini uwepo wa Mungu...je Mungu anaijua future yako?
Anaijua bila shaka kabisa.

Tuendelee ....
 
Nilichogundua ni kuwa huijui AI inavyofanya kazi na either hutaki kujua au unapenda kubaki na imani yako.
Ndiyomaana unaona kama nayosema ni "nadharia"
Hata wewe ukiingizwa kwenye game saivi ukawaambia wale watu kuwa huu sio uhalisia watakuona kama unawaambia "nadharia"
Jaribu kufanya research fikiria zaidi kinadharia kama Einstein ili ujitofautishe na Zinjanthropus maybe unaweza kugundua kuna ziada ya yale unayoyafahamu kuhusu ulimwengu huu nje ya uliyofundishwa shule na kanisani
 
Kwanini hujibu maswali ninayo kuuliza ?
 
Hukuuliza swali hilo kwangu.
Haya nimekujibu

Ndio nina uhakika.
Thibitisha

Pili, unaposema wao wana dhani bila kuweka ushahidi huu ni utoto na kutumia akili vibaya. Embu mchukue muhusika mmoja umuulize kuhusu hiki unachokidai akikujibu uje kutuwekea ushahidi hapa.

Thibitisha hilo.
Again unaundermine uwezo wa AI...kitu kikiwa preprogrammed kuamini kitu fulani ni ngumu kukiyumbisha kama wewe ulivyokuwa programmed na aliyekutengeneza kuwa wewe ni halisia...yawezekana hata hapa nachati na roboti...unaweza kunithibitishia wewe ni mtu halisia??

Anaijua bila shaka kabisa.

Tuendelee ....
Sasa kama anajua kesho utaenda kanisani kesho ukienda kanisani utasemaje kuwa wewe ndo umepanga kwenda wakati ni kama unacheza igizo na unafata script
 
Back
Top Bottom