Kwanza, Sio kila "yawezekana " ni nadharia nyingine ni probability kwasababu huwezi kuwa na uhakika na chochote kwa 100%.
Sasa mbona hujui hata tofauti ya hayo maneno ? Hili tatizo lingine mzee, nadharia ndio yawezekana na ndio "probability" yenyewe,hujaandika kipya hapa zaidi ya kudhihirisha kutokujua maana ya mananeno husika.
Ndomana nikasema sina uhakika kuwa wewe ni mtu au ni program nachati nayo kunipotezea muda...
Nilikwambia huko nyuma ya kuwa unavyo andika ni dhana tu na huwezi kuthibitisha hata kimoja, haya ni matumizi mabaya ya akili.
badala ya kuruka kuhusu neno moja ungenithibitishia wewe ni mtu 'halisi'....
Inaonekana unakubali bila kusoma, nimekuthibitishia ya kuwa mimi ni mtu kwa nukta nyingi huko nyuma, nukta ambazo hao wanasesere hawana sifa na ithibati moja ni kuwa mimi ni hai sababu nina ufahamu na uhuru wa kuchagua. Sasa wewe ambae unadai hata hao wanasesere wana dhani halafu unashindwa kuonyesha kudhani kwao, huu ni ujinga ulio chupa mipaka.
Nikuthibitishie mara ngapi kama mimi ni mtu halisi ? Ninaona, nina shika, ninafanya maamuzi nina kumbukumbu, nina hisia na mengine mengi,na hapa naandika muda huu.
mimi sijui aliyekutengeneza kama vile wanavisesere hawatujui tuliowatengeneza lakini nachojua umetengenezwa...au wewe umejitengeneza??
Haoa naona najadikiana na mtu asie jitambua halafu anasema kuwa anajua nimetengenezwa lakini hajui nani amenitengeneza, sasa kwanini unajadiki jambo usilolijua mzee ?
Mimi nimeumbwa na mwanadamu hatengenezwi mzee. Hata matumizi ya maneno hujui.
Pili,wewe kama msomi tafadhali weka arguments kisomi...kama Huyo Mungu anajua kesho utaenda kanisani,unataka kusema haihusiani na uwezo wa machaguo yako ya kwenda kanisani??
Sio kwamba niweke "arguments" kisomi, sema hujaelewa kilicho andikwa. Haihusiani sababu hanizui mimi kufanya hilo sababu amenipa uhuru. Hili jepesi sana, nashangaa kwanini huelewi, inaonyesha hufikirii zaidi ya ugonjwa wako wa kufata dhana hili tatizo lako, na hoja nimekuwekea.
Kama kweli una uwezo wa kuchagua inamaana kesho ndo angejua pindi unaenda kanisani lakini kama hata leo anajua basi wewe hauna free will inamaana kesho lazima uende tu hata ufanyeje umeshapangiwa ivyo.
Hii ndio maana ya Mola wetu kuwa muweza wa kila kity, yaani hana kizuizi, na unayotaka wewe yawe ambayo hayawezi kuwa wala hayajawahi kuwa ni udhaifu, na Mola wetu sisi ni mkamilifu.
Chagua moja huwezi kuwa na vyote either Mungu haijui kesho yako au wewe hauna free will
Hapo hakuna cha kuchagua moja, kwani kufanya hivyo ni kuipibga akili iliyo salama.
Mola anajua vyote ndio maana anajua hata yale ambayo hayajatokea na laiti yangetokea anajua yangekuwaje.