Nimethibitisha: ukimuomba Mungu jambo lolote atakupa – ukitimiza vigezo na masharti haya

Nimethibitisha: ukimuomba Mungu jambo lolote atakupa – ukitimiza vigezo na masharti haya

I am my own rule maker ,I set the guidelines .. I decide how well I'm doing ...
I understand where you're coming from — that mindset makes sense outside of the Christian faith. But in true Christianity, we don’t make our own rules. We follow a holy God who has revealed His will through His Word.

You see, faith in God isn’t just believing He exists — it’s submitting to His authority. As Proverbs 14:12 warns, 'There is a way that seems right to a man, but its end is the way to death.' And Jesus said clearly, 'I am the way, the truth, and the life. No one comes to the Father except through me.' (John 14:6).

So yes — you can set your own rules if you’re walking alone. But if you ever truly seek to walk with God, it won’t be on your terms. It’ll be on His. Search the Scriptures and see!
 
Ameen Barikiwa,
Nb: Mungu ni roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
 
Mtaka cha uvunguni huinama! Fasting ina faida hata kwa afya yako tu.
Nikae na njaa alafu ndo nipate hitaji langu flani ?hii concept na Ile ya kutoa kafara au rushwa kuna utofauti wowote?
 
Kama Mungu amekujibu maombi yako, mshukuru tu na uendelee na maisha.
Ushuhuda huo ni njia ya kumshukuru Mungu na kumsifu
Wala usidhani uliomba vizuri sana kuliko wengine, au una haki sana kuliko wengine.
Sijasema hayo ndugu! Na Mungu asingenipa kama ningekuwa na nia hiyo ya kujivuna
Mungu humpa amtakaye, na kwa wakati wake mwenyewe.
Hiyo kauli umeitoa wapi? Mungu hana upendeleo. Acha kukata tamaa!
Hujawahi kujiuliza kuna watu hawaabudu Mungu, wala shetani lakini mambo yao yanafanikiwa tu?
Hilo swali nimeishalijibu. Soma post #38
 
Sawa lakini kwako kuna feedback.kwa Mungu hiyo kitu haipo
Feedback ni majibu ya maombi. Ukiomba ukapata unachohitaji hiyo ndiyo itakuwa feedback. Na Mungu akipenda anaweza akakujibu instantly! Mimi nimeomba mara nyingi Mungu aniponye magonjwa, na nimekuwa nikipona papo hapo. Anza sasa utaona faida za kuomba.
 
Si uje uone nyumba na gari yangu. Halafu uwaulize niliokuwa nikifanya nao kazi ya mshahara mdogo, watakueleza jinsi nilivyopata kazi ya mshahara mnono. Watakuthibitishia jinsi ninavyopenda kumuomba Mungu. Usipoamini vinywa vya mashahidi wawili au watatu basi hata malaika wakikuthibitishia utaona mashaka tu. Jaribu wewe mwenyewe kutimiza vigezo hivyo na uombe uone kama hutapata. Mungu hana upendeleo!
yani we kilaza kweli[emoji57] , kwa hiyo kila mwenye mshahara mdogo na ana gari na nyumba vimeshushwa from no where? watu wanapambana in different ways ili wafanikishe mambo ikiwemo kujinyima then we unaongea nini?

unaweza kunieleza suala moja tu nione akili yako ilivo then nikufafanulie uelewe?.

Kiwanja ulichojengea nyumba ulikipataje? na fedha ya kununulia hio gari uliipataje?

ukinijibu haya takuambia nachotaka kukuambia.
 
Niombee biashara ikue
Nakuombea sasa hivi:
Ee Mungu Baba, umeiona imani ya Lastmost . Naomba sasa Mungu uitimize ahadi yako kwamba tukiomba lolote tutapewa. Mungu Baba nakusihi umpe ndugu huyu wateja wengi. Mpe maarifa ya kipekee ya kufanya biashara hiyo. Mfungulie milango ya pesa za kuongeza mtaji wake. Mlinde atokapo na aingiapo. Ilinde biashara yake dhidi ya maadui zake. Asante Mungu kwakuwa umesikia na utafanya, katika Jina la Yesu Kristo, amen.

Tarajia kuona biashara yako ikikua.
Usisahau kuzingatia kigezo #3 na #10
 
Ni kweli kabisa kama Yesu alivyoahidi katika Yn 14:13-14 tukimuomba Mungu jambo lolote tutapewa au tutafanyiwa. Nimethibitisha hilo mimi mwenyewe. Niliomba pesa ya kujenga nyumba na kununua gari nikapata - nilikuwa na kazi ya mshahara mdogo nikapata kazi yenye mshahara karibu mara kumi ya huo wa mwanzo! Niliomba mwenzi mzuri wa ndoa ninaye. Niliomba nifanikiwe kibiashara-wateja napata! Mungu amenipa maarifa na kunifanyia mambo mengi ambayo kwa akili zangu au kwa njia za kawaida nisingeweza kuyapata. Muda hautoshi kuyaeleza yote hapa.

Inawezekana umekuwa ukimuomba Mungu jambo fulani kwa muda mrefu hujapata. Usikate tamaa. Zingatia vigezo na masharti yafuatayo, hakika Mungu hana upendeleo, atakufanyia:

1. Omba kwa imani
"Lakini na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari..." (Yakobo 1:6)

2. Omba sawasawa na mapenzi ya Mungu
"Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia."
(1 Yohana 5:14)

3. Tii amri za Mungu
"Na yo yote tutakayoomba tutapokea kwake, kwa kuwa tunazishika amri zake..." (1 Yohana 3:22)

4. Omba kwa Jina la Yesu
"Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya.." (Yohana 14:13)

5. Usiwachukie waliokukosea. Wasamehe kabla hujaanza maombi
"Na kila msimamapo kuomba, sameheni..." (Marko 11:25)

6. Usichoke kuomba. Omba kwa bidii mpaka upate
"Ombeni bila kukoma." ( Wathesalonike 5:17)
Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii (Yak 5:16)

7. Usiombe kwa ajili ya tamaa zako - kwa mfano, usiombe jambo fulani ili upate kisha ujionyeshe kuwa wewe ni bora kuliko wenzako
"Mnaomba wala hampati kwa sababu mnaomba vibaya, ili mpate kutosheleza tamaa zenu."
(Yakobo 4:3)


8. Funga na kuomba. Mambo mengine yanafanyika ukiongeza "gia" ya maombi(kufunga)
"Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga." (Mathayo 17:21)

9. Omba kwa Roho
"...Nitaomba kwa roho, na pia nitaomba kwa akili yangu." (1 Wakorintho 14:15)

10. Usitende dhambi. Dhambi ni kikwazo kikubwa cha kujibiwa maombi. Hivyo, tubu dhambi zako, na kuziacha kabla hujaanza kuomba. Watu waliookoka na wanaoishi maisha matakatifu wana nafasi nzuri ya kupewa lolote wanaloliomba.
"Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia." (Isaya 59:2)

Anayekataa kuisikia sheria, huyo hata sala yake ni chukizo kwa Mungu." (Mithali 28:9)
kwaiyo ww n mwema kuliko yule lazaro aliyekuwa anakula makombo mezani kwa tajiri( maana alikuwa maskini) au ww n mwenye aki kuliko yule mjane ambaye hakuwa na kitu (aliyetoa senti 2) au ww n mwenye haki kuliko wale ( thenashara )wale wavuvi wabangaizaji na maskini wa maisha ya kidunia.....?? ko wote wanaofanikiwa n watakatifu? ....sisi waovu hatufanikiwi?...........na mbona ww kuna amri 1 hutaki hata kuisikia?
 
Nimethibitisha hilo mimi mwenyewe. Niliomba pesa ya kujenga nyumba na kununua gari nikapata - nilikuwa na kazi ya mshahara mdogo nikapata kazi yenye mshahara karibu mara kumi ya huo wa mwanzo!
Uzi wako ungeishia hapa tu!
Haya, tumeshajua kuwa wewe ni milionea, una gari na una mjengo.

Hongera sana mkongwe!!!
 
Nitarudi asee KWENYE hii MAADA natamani gari na million kama 30 hv ila nishinde betpawa nimpige muhindi
 
kwaiyo ww n mwema kuliko yule lazaro aliyekuwa anakula makombo mezani kwa tajiri( maana alikuwa maskini) au ww n mwenye aki kuliko yule mjane ambaye hakuwa na kitu (aliyetoa senti 2) au ww n mwenye haki kuliko wale ( thenashara )wale wavuvi wabangaizaji na maskini wa maisha ya kidunia.....?? ko wote wanaofanikiwa n watakatifu? ....sisi waovu hatufanikiwi?...........na mbona ww kuna amri 1 hutaki hata kuisikia?
Usinilishe maneno ndugu. Mimi sijaandika uzi huu ili kujilinganisha na Lazaro na yule mjane. Nimeandika kuelezea ukweli wa ahadi ya Mungu ya kutujibu maombi. Niliomba nikapewa. Period!
Hata hivyo Lazaro alienda kukaa kifuani kwa Ibrahimu. Hiyo si ni baraka kubwa tu. Na yule mjane Yesu alimsifia kuwa ametoa kuliko wote.
 
Back
Top Bottom