Nimetoa sharti la kupewa laki kila mwezi ....vinginevyo atambae

Nimetoa sharti la kupewa laki kila mwezi ....vinginevyo atambae

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Kuna mtanashati ameonesha nia kutaka kunioa. Nami nikaona niwe muwazi kwake mapema isije ikazua balaa siku za usoni.

Nimefunguka kinaga ubaga kuwa mwanamke mazingira, mwanamke matunzo. Nikaenda mbali zaidi kwa kumpa usemi usemao "ukiona mbwa anakonda lawama zinaenda kwa mwenye mbwa". Na mm sitaki kuchakaa nitakapo olewa.

Basi nikamuambia ili kuhakikisha naendelea kupendeza nitataka uwe unanipa pesa kwa ajili ya matumizi yangu ya dharura isiyopungua laki. Hii pesa pamoja na mshahara wangu usiiihesabie kwenye matumizi yoyote ya nyumbani wala usiichukulie kama ndiyo hela ya matunzo yangu. Hii ni kama pocket money tu. Ili mtoto wa watu niendelee kuchanua na nisichake kwa stress.

Ndiyo. Huko ndiyo kuolewa, mwanaume si ni kichwa cha nyumba!?? Siyo niolewe halafu bado niendelee kuishi kwa kuiwazia hela ya kula, kodi, kuvaa, kunywa,n.k. Hela ya kuendesha maisha ya familia inatafutwa na mwanaume mm si nimeolewa bhana.!?Mshahara wangu ni kwa ajili ya mambo yangu. Kazi yangu kubwa ni kuzaa tu. Ndiyo maana nchi za kiarabu huko mwanamke akibeba mimba mumewe inabidi alipe hela nyingi sana kama asante kwa mkewe. Na bado wanawake wengi ktk nchi hizo siyo tu kwamba hawaendi maofisini, bali hata sokoni hawaendi.

Nimempa hilo sharti, akiliona analiweza poa, akishindwa basi ajue siyo fungu lake.

ONYO; Wanaume bebeni jukumu la kulea familia, msioe kwa kuangalia mishahara ya wake zenu. Wanawake wanapaswa kutunzwa. Mishahara yao ipo kama ziada kwa matumizi yao binafsi.
 
Duh!Kwa hiyo yeye ndiye anakuhitaji zaidi kuliko unavyomhitaji?
Umeweka sharti la laki moja kwa mwezi kwa kuzingatia kipato chake au hali yako?Maana naona kama umejipimia kiasi kidogo lakini wanaofaidi pesa ya mwanaume huwa hawaombi hata senti na hiyo humfanya mwanaume atoe zaidi kuliko angepangiwa kiwango.Vipi ukichumbiwa na mtu kama Dangote utaomba laki?Naona umejipangia bei kulingana na thamani yako.Basi hiyo ni kama mipaka ya baraka na dalili ya kutojitambua.Hakuna kitu muhimu kama utu kwenye mahusiano yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtanashati ameonesha nia kutaka kunioa. Nami nikaona niwe muwazi kwake mapema isije ikazua balaa siku za usoni.

Nimefunguka kinaga ubaga kuwa mwanamke mazingira, mwanamke matunzo. Nikaenda mbali zaidi kwa kumpa usemi usemao "ukiona mbwa anakonda lawama zinaenda kwa mwenye mbwa". Na mm sitaki kuchakaa nitakapo olewa.
Mbona unapewa mshara mdgo ivyo
 
[emoji116]
 

Attachments

  • IMG_20170813_220818_920.JPG
    IMG_20170813_220818_920.JPG
    56.8 KB · Views: 94
Huyu mtoa mada itakuwa anaota ingekuwa vizuri aliye karibu nae amshtue kidogo naona kashafika us anawaza madolali ,hakuna mwanaume wa hivyo usitusingizie.
 
Bora mngefanya joint business na sio mapenzi..ukiendelea hivo hutokaa uolewe na mwanaume anaejitambua labda mburura ndio ata fall kwako

What goes around always comes around
 
Uwezo ni majaaliwa na wawili kusaidiana ni muhimu hasa katika zama hizi....wenye mishahara midogo wasioe??na nyinyi mtadorora tu kusubiria wenye pesa
 
Back
Top Bottom