Nimetoka kuwaangalia Wydad Casablanca FC wakicheza wakiwa Kwao nimejikuta Huzuni kunipata na Machozi kunitoka

Nimetoka kuwaangalia Wydad Casablanca FC wakicheza wakiwa Kwao nimejikuta Huzuni kunipata na Machozi kunitoka

Kwani akiwa kwao ndio wanakuwa na miguu mitatu? Its all anout mindset, ingekua mimi ningeudanganya ubongo kwamba tupo nyumbani na hao mashabiki ni wetu.

Huwa nafanya hivi hata katika mambo mengine ya kimaisha kwa mafaniki makubwa sana
Miye naamini mnyama atatoboa
 
Siyo kwa Wydad Casablanca FC tena akiwa katika Ardhi ya Kwao huku Majukwaani wakiwa Wanahanikizwa vilivyo na Mashabiki wao Wakorofi utadhani ni Wavuta Bangi wakati kumbe hata hawaivuti.
Usiseme "Utadhani wavuta bangi". Wale bangi wanatafuna kabisa hawavuti.
 
Usiseme "Utadhani wavuta bangi". Wale bangi wanatafuna kabisa hawavuti.
Huwezi amini Mimi nilijua Waarabu hawavuti kabisa Mpepe / Bangi ila kuna Watu hapa Wamenielimisha kuwa tena Wao ndiyo Wanaivuta hata Hayati Bob Marley anasubiri.
 
Ni sawa na leo nimsikie Bondia Hassan Mwakinyo akitamba kuwa atamgharagaza vilivyo Bondia Antony Joshua au Bondia Tyson Fury.

Mtanisamehe tunaenda Kuzikoga / Kufungwa mno Jumamosi huko nchini Morocco kwa Wydad Casablanca FC.
Mkuu naona umeikatia tamaa sana timu yetu. Japo mechi itakuwa ngumu ila naamini watapambana kurudisha heshima inshallah.
Tusubiri dakika tisini zitaamua.
Nina imani hatuaibika.
 
Ni kweli Moira unadunda pale Simba watakapokuwa wanacheza wenyewe, ila kama watakuwa wanacheza na hao Wehu, basi utadundia kwenye nyavu za Simba, hii ni utake usitake utapigwa tu hata kwa goli la shabiki
 
Kwani akiwa kwao ndio wanakuwa na miguu mitatu? Its all anout mindset, ingekua mimi ningeudanganya ubongo kwamba tupo nyumbani na hao mashabiki ni wetu.

Huwa nafanya hivi hata katika mambo mengine ya kimaisha kwa mafaniki makubwa sana
Huwezi kuudanganya ubongo kwenye mambo yasiyowezekana kabisa, kama huamini udanganye huo ubongo wako kuwa wewe utakuwa Kocha wa Wydad uone kama itawezekana. Ubongo utaudanganya pale unapoweza kufanya na kushinda uvivu ila sio kushinda uhalisia wa kile ambacho hujawekeza na hata Mungu hawezi kukupa abadan, jifanye wiki ijayo utakuwa Rais tuone kama hiyo nguvu itawezekana. Simba hata ajidanganye hilo jambo halipo, anachoweza kufanya ni kujipa nguvu kupunguza idadi tu na sio kushinda
 
Mkuu naona umeikatia tamaa sana timu yetu. Japo mechi itakuwa ngumu ila naamini watapambana kurudisha heshima inshallah.
Tusubiri dakika tisini zitaamua.
Nina imani hatuaibika.
Mkuu hakuna aibu yoyote ile ambayo Simba ataipata akifungwa na bingwa mtetezi. Simba inapaswa apitie tanuru la moto kama huo mara 4 ili waweza kufunga team calibre ya Waydad Casablanca. Simba inafanya vizuri sana ukilinganisha wachezaji iliyo nao. I mean uwekezaji wa team ( Gharama ya mchezaji mmoja mmoja). Gharama ya team ya simba ni kwenye 5 billion. Wakati akina Waydad ni kwenye 80 + billion
 
Mwaka 2012 iliaminika hivyohivyo kwamba Nou Camp ni machinjioni lakini mwaka huo Barca alitupwa nje ya mashindano na timu ya Chelsea ambayo haikutegemewa sana kufanya hivyo.

Unaweza kufungwa na wewe ukafunga at the end aggregate ndiyo itaamua na hata Simba akishindwa bado atakuwa kashindwa mbele ya timu kubwa zaidi yake na ili Simba achukue kombe hili sharti acheze na timu hizihizi tena home and away la sivyo aachane na ndoto za ubingwa huo.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Yaani Unazungumzia Chelsea iliyokuwa na kina Droghba, Tores ambao ni World class prayers ukiwafananisha na kina Kibu? Hupo serious wewe, kwasasa ungesema Wydad wanaweza kushangazwa na Raja, Mamelodi na sio Simba, yaani ungesema mwaka huo Barcelona angeshangazwa na Arsenal kidogo ila sio Chelsea kabisa kwani walikuwa na beki bora kabisa na viuongo wakatili na washambuliaji wenye nguvu na ubunifu pia.
 
Huwezi kuudanganya ubongo kwenye mambo yasiyowezekana kabisa, kama huamini udanganye huo ubongo wako kuwa wewe utakuwa Kocha wa Wydad uone kama itawezekana. Ubongo utaudanganya pale unapoweza kufanya na kushinda uvivu ila sio kushinda uhalisia wa kile ambacho hujawekeza na hata Mungu hawezi kukupa abadan, jifanye wiki ijayo utakuwa Rais tuone kama hiyo nguvu itawezekana. Simba hata ajidanganye hilo jambo halipo, anachoweza kufanya ni kujipa nguvu kupunguza idadi tu na sio kushinda
 
Na nahisi huenda GENTAMYCINE Usiku wa Saa Nne ( 4 ) Jumamosi ijayo ya tarehe 29 April. 2023 Nikalia zaidi na Kuhuzunika Kunakotukuka.
Haujawangalia Wydad na simba yako vizuri embu rudia tena ukirudia utajua WAC ana mechi ngumu sana ndomana walivyoona wanashambuliwa baada ya goli la kwanza wakachoma uwanja ili kupumzisha wazee wao waliokua wamekamatwa pale kati maana walishambuliwa mfululizo
 
Na nahisi huenda GENTAMYCINE Usiku wa Saa Nne ( 4 ) Jumamosi ijayo ya tarehe 29 April. 2023 Nikalia zaidi na Kuhuzunika Kunakotukuka.
Lia machozi ya damu.Wewe Ni mmbea km wambea wengine tu.

Ila mnyama anaenda kutinga nusu fainali
 
Shuhuli ilishaisha kwa Mkapa...

Raja atalia kama mtoto kumuona Simba katoboa. Ndo mpira ulivyo
 
Back
Top Bottom