Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Ndio mana kuna watu wanapinga mambo za mahari sababu ndio kama hizi. Kwani angepokea hyo 1M angepungukiwa kitu gani wazee wengine nuksi sana.

afu mahali milioni 4 huyo binti hatarudi kwao??? sema sishangai bro wangu alitajiwa mahali 6M akalia lia wakapunguza mpaka 4M[emoji23][emoji1787][emoji174][emoji174] mama angu ana hasira mpaka leo na hiyo pesa mwanae katajiwa[emoji119][emoji119]
 
Usinitishe bhanaaa, kwani nilibaka?
Mimba ni matokeo ya nyege zetu, haina lawama hiyo!
 
Huyu hajui kila jamii ina tamaduni zake, huyu angekuwa kamfanyia binti waki Zanzibar ndiyo angejua vizuri ni jambo baya la kuishi kinyumba na binti wawatu bila ndoa, kule Zanzibar angefungwa jela kwa kosa la kutorosha binti chini ya uangalizi wa wazazi na kumbaka na kuishi naye kinyumba yani mpaka leo angekuwa yupo mahabusu, yani Wazanzibari wanatushangaa sana sisi watanganyika tunaishi na wanawake bila ndoa, hii tabia ya hovyo wazanzibari hawana ya kuishi kinyumba na mtoto wa mtu.
 
Kwa hiyo ningeamua kukaa kimya bila kwenda huko kujitambulisha ndo ingekuwa sawa?
 

it make sense hata angeenda mmoja hivi unadhani kigoma ni safari ya kariakoo-kimara[emoji23] kule ni dar-kigoma kwa mtu mwelewa anaelewa na sio mjini ni kijijini labda niambir hilo la kumzalisha bila kwenda kuonekana ila la kwenda na ndugu mmoja weee kawaida hiyo sana tuu kama hana uwezo wa kusafirisha watu???
 
Jamaa anatakiwa awe mpole tuu, wazee wa huyo binti ni wazee wa kimila sasa mwamba wetu yeye ni Mzee wa dot.com , kimila ni aibu binti kuzaa bila ndoa ...yeye aendelee Tu na binti alafu M4 siyo hela nyingi Kwa binti ambaye umezaa naye na ana upendo wa dhati .... Jamaa bado maziwa mdomoni aisew
 
Kwa hiyoninsyodharaulika ni familia ya mwanamke tu, lakini ya mwanaume haidharauliki?
Ndiyo ya mwanamke, ndiyo maana kila siku zinatungwa sheria za kumlinda mtoto wakike.we unafikiri huyo binti wazazi wake wamejibana kiasi gani ili kumsomesha mtoto wao usikute huyo mzee kauza mashamba na mifungo ili mtoto wake aje awasaidie wadogo zake.
 
Ningekua mm hata 100 nisingetoa. Kwanza nilivoona amekasirika ningejifanya kukubaliana nae kwa kika kitu. Na kusema anisamehe fidia nitatoa pia. Yaan kumuaminisha kua Niko tayar kwa lolote atakalo. Baadae sasa tukishakuabaliana nawaambia leo nimekuja kuelewana mahari na gharama zote maana sikujua gharama na mahali. Waniruhusu nirudi siku nyingine kuvilipa.

Baada ya hapo nisingerudi. Huyo binti ningeondoka nae kufika mbele kidogo ningemtelekeza kwa mshenga na kuondoka milele. Nisingerudi kigoma kamwe. Na huyo mtoto wangemsomesha wao na kumtunza baadae akiamua kunitafuta atanitafuta.
 
Pole sana kiongozi, umepata baba mkwe mkoloni sana.Ana tabia zote za Wazee Wa zamani.

Baba mkwe wako,kasimamia misingi ya Mila na tamaduni za kwao. Kimsingi ulikosea ulipo Anza kukaa na Binti Yao kienyeji,Hadi kufikia kumpa ujauzito , akaenda kujifungulia kwao(pasipo wewe kujurikana), akaja akafikwa na msiba(hukuoneka pia).

Matukio yote hayo uliyafanya na Binti Yao na kuwasiliana na Binti Yao tu. (hapa walitafasiri kuwa una jeuri).
Bado haitoshi ukapereka zawadi(unapereka usasa Kwa watu wenye misimamo ya kikoloni).

Sasa kwakuwa mambo yameshatokea, Haina budi kupambana, Ili muwe na mapenzi bora na salama wewe na familia yako. (Tambua mkwe ni Muha wa mipakani).

Jichange, ukipata ata 1M fanya kwanza mawasiliano na mshenga wako, Mshenga ndiyo afanye mawasiliano na baba mkwe wako! Amtaarifu kuwa "mmebahatika kupata 1M hivyo mnaomba aipokee, nyingine mtazidi kutuma mbeleni".Baada ya muda ukipata kama 500K fanya hivyo hivyo, alafu ndiyo uhanze Kutengeneza mawasiliano na mama mkwe wako. Kira Utakapo kuwa una wasiiliana nae mkumbushe amsalimie baba mkwe wako.

Baada ya muda tengeneza mazingira iyonekane mnapitia Hali ngumu sana, lakini unazuga kutuma ata pesa kidogo ya sukari na chumvi(hapa tuma Kwa mama mkwe au baba mkwe alafu mpe mwanao Simu awasalimu).Endelea kuwa Julia Hali na kushiriki mambo madogomadogo ya upande wa ukwenu.

Kuna muda atajirudi tu na anaweza kurudisha moyo nyuma, lakini pia mahali ata isipo isha siyo mbaya. Kikubwa umeonesha nia na utayari. Pia wamesha ona na Kutambua wewe ni mtu wa namna Gani.

Ndoa ni baraka toka pande zote mbili.
 
Siku Nilipoondoka Kigoma Kurudi Dar Es Salaam (Mzizima) Sikutaka Tena Kurudi Tena Huko
Mwezi Wa Nne Mwaka Huu Nimekwenda Kigoma Kupitia Kaliua Nilipofika Kigoma
Ilibidi Niondoke Kesho Yake Asubuhi Mapema Sana


Kigoma Ni Mbali Mno Zamani Tulikuwa Tunapitia Kahama Na Kulala Hapo
Mleta Mada Kigoma Ni Kipengere Mno
 
Kwa hiyo ningeamua kukaa kimya bila kwenda huko kujitambulisha ndo ingekuwa sawa?
Kwao ni sawa tu ndiyo maana hawaja kushobokea, watalea mjukuu wao maisha yataendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…