Nimetokea kumpenda binti yao lakini wazazi wake walikuwa na uadui wa miaka 16 na mama yangu

Nimetokea kumpenda binti yao lakini wazazi wake walikuwa na uadui wa miaka 16 na mama yangu

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
Takribani miaka 6 Sita Sasa tangu uangalizi wangu kwa binti wa majirani zetu, nampenda yule binti nayeye pia ananipenda pia kwao walizaliwa 6 lakini wa kiume mmoja binti Huyo Alifunga kizazi na ndio pekee aliyeweza kusoma

1.ugomvi wa visima vya maji
Ugomvi ulianza kwenye kisima cha maji mwaka 2007 wakati huo visima vya futi 7 had 8 ndo vilikua vyanzo maji mkoani kwetu mama yake binti, watoto wa kiume, yao pamoja Dada zake watatu mara kwa mara waligombana na mama walikuwa wakivunja uzio ule wa nyasi na Kuiba maji Bila idhini ya mama!
(huu ulifika mwsho Baada ya 2023)Baada ya mimi kuongeza uref

2.ugomvi wa mipaka ya nyumba (huu ugomvi umedumu miaka 16)

(Nimekuja kuumaliza mwaka Jana Baada ya mama kufariki 2023 )
(lakini hapa ndipo nitamnukuu Dr. Jakaya kikwete(usirithi adui wa mtu mwingine) naongezea kwa vile mama yetu alitufunza kuwa ata kama tunaona
watu fulani wanagombana nayeye tusiache kuwasalimia kwa adabu wala tusijiingize kwenye vita zao

3.ugomvi wa kibiashara
Kwa miaka 15 tangu 2009 wao (biashara zetu zilifanana) hawakuwahi kununua kwetu wala sisi hatukuwahi kununua kwao na maduka yalikuwa ni nyumba jirani mimi nilimaliza miaka 5 Bila kupitia njia yao na hadi Leo ni ngumu kupitia kwenye njia iliyo mbele ya nyumba yao

4.Baada ya mama kufariki mama yao hao majirani waliuhudhuria msibani na kwenye mapishi walishiriki Tena vizuri mno nakumbuka Ata mapishi ya mwisho mama yao jirani zetu alikesha hadi asubuhi na hakuna mtu wa familia yangu aliyedhurika Kati yetu kwa Kula chakula kilichopikwa na jirani yetu Huyo ambaye tunabeef nao

Mwisho wa story binti yao mimi nampenda lakini kuna dosari mbili
1.mzazi wangu aliyebaki hasalimiani nao
2.ndugu zangu pia

Wale Ile familia mm nasalimiana nao wote baba yao, mama yao, kaka zao mwanzoni wali jaribu kunichokoza waakanzisha vita za mitaro 🤣mimi nikawa jibu shortly "sijibizanagi na wanawake sana sana mtakula makofi tu"

Waka jaribu mara nyingine kunichokoza kuhusu maji ya mtaro maana tunashare mifereji ya maji taka nkafumua shimo lililopo nikaliongezea futi wote kimya

Mpaka sasa yapata mwaka tunasalimiana vizuri mno (mama yao ni mchuuzi mdogo mdogo sokoni) japo sijawahi kumuungisha Nina wasiwasi nao, baba yao anauza duka la home access zijawahi muungisha pia Ila ninawasalimia kwa adabu wote mama na baba yao!

kuna mda wananiletea hadi wapangaji kwenye nyumba yetu na wale wapangaji Hawana shida kabsa,sometimes kwenye biashara wanasontesha(kwenye biashara yangu ndogo ndogo wateja waniungushe)

Mwisho, mimi binafsi natamani bifu yetu iishe maana ni bifu baridi
(na binti yao Alishawahi kuniuliza wazazi walikuwa na ugomvi wakigundua uhusiano wetu na yule binti itakua vipi)

NB. Binti yule ametulia pekee kapiga shule kuliko wote kwao amebahatika na kuajiriwa sehemu nzuri (tulisoma shule moja wakati yuko formtwo mimi nilikuwa fomfsix na kiumri namzidi miaka 6), namzidi Kila kitu exposure, elimu, status Kila kitu


Ila angalau ni mtulivu(madhaifu mengine yanaeleweka) ya kawaida tu

Niache bifu baridi iendelee au nilimalize??
 
Hujui kupiga cross ndefu za kina Modric. Ulitakiwa umalize ugomvi muda mrefu uliopita, sasa wewe unataka zimamoto. Unamaliza ugomvi kwa kutangaza mahusiano unaonekana umelazimika na sio kutoka moyoni.
 
Changamoto ni jambo la kawaida ktk maisha, hivo usizifanye kikwazo cha kutomuoa binti uliejiridhisha anakufaa kwa mda mrefu.
 
USHAURI WANGU:

Huyo binti usimuoe, kwasababu hatapata ushirikiano wowote kutoka kwenye familia yako kwa sababu mna ugomvi, kuwa makini katika hilo kama inawezekana jaribu kumuuliza na baba yako na wazee wa hapo mtaani kwenu ili walishughulikie hilo jambo kama unataka kweli liishe, lakini usitegemee et mahusiano yako na huyo binti ndio yamalize ugomvi kumbuka ugomvi umeanza muda mrefu
 
Na hapo kuna penzi la kweli ila ndo hivyo mtakutana na kila aina ya vikwazo,
 
Muoe, ndoa yako itakua imechangamka muda wote hadi raha......

Mara leo shemeji kaja kugombana kuhusu mtaro, kesho ba mkwe nae kaanzisha ugomvi wake, mara mke nae ndani anakumind haujawahi muungisha baba yake, hapo hapo nawe unamchenjia hajawahi kununua kitu kwenu.

Ndoa haitapoa hii, tia mimba huyo binti chap ugomvi uendelee hadi raha yani.
 
Back
Top Bottom