Nimetongozwa na kavulana kauza bucha la nyama

Enyi watoto wadogo, wakiume, wavulana nani amewaloga?

Mmekuwaje mbona hamna hofu ya kuogopa wakinamama wakubwa waliowazidi umri mara 20000?

Mnapata wapi ujasiri huo?

story iko vile:
Jana nilipita kwenye bucha la nyama ambako huwa ninapenda kununulia hapo kwa kuwa wana nyama ya kutoka wilaya ya Ukerewe. Kwa ufupi nyama inayotokana na ng'ombe wa Ukerewe ni nzuri kwa kuwa ng'ombe wa Ukerewe wanalishwa tu maeneo jirani na nyumbani, hawajachoka na pia nyama ya Ukerewe ina ladha nzuri na ni laini. (sio tangazo za biashara mjue)

Baada ya kununua nyama, wakati nafungua mkoba kutoa hela, hako kavula kakawa kananiangalia sana, na mie nikakazia macho. Kakawa kanaonesha ishara ya kuomba namba za simu (yaani kakawa kanaweka mkono wake kwenye sikio kama vile kanapokea simu). Nilikaelewa nikakausha tu. Nikamlipa mwarabu hela yake.

Nilivyotoka hapo kuelekea kwenye usafiri, ghafla nikaona dogo yuko nyuma yangu. Mazungumzo yakaanza:

Dogo: Mama shikamoo.

Mie: Marahaba.

Dodo: huku akiwa anatoa tabasamu kama la panya, samahani mama naweza kupata namba yako ya simu.

Mie: Kwa ajili ya matumizi yepi?

Dogo: Ili niwe nakupigia kukupa taarifa za nyama inapoingia toka Ukerewe.

Mie: Mbona ratiba naijua tu, kwani ni lini niliikuja hapo nikakosa nyama?

Dogo: hahahaha, basi tuyaache hayo ya nyama, nataka tu nipate namba zako tuwe tunachat, kwa ufupi nimependa uwe mtu wangu!

Mie: Mxeeeewuu (nikaondoka zangu nikakaacha kamesimama hapo)
Tatizo lenu ninyi KE ni rahisi sana kuwadaka hata kama kwa siku ya kwanza umeonyesha hasira , dharau na matusi. Huwa mnakaa na kuanza kufikiri tena na kujifanya kuonea huruma mwisho wa siku mkikutana siku nyingine mnaanza kujilegeza msimamo. Mbaya zaidi ukute nyumbani jamaa kakukoromea au kuna kaugonvi utajipeleka mwenyewe kwa dogo anayeonekana anakujali
 
Mdada/Mmama unaombwa namba kistarabu unakaza "yanini sasa" we mpe namba then msikilizie atakwambia nini,unajua sometimes hawa watu wanaotupenda kimapenzi sio wa kuwapuuza sana maana huweza kutuambia mambo ya siri mengi ambayo tulikua hatuyafahamu.

Mfano: hako kadogo tu assume umempa namba then siku moja ktk kuchat ukamuuliza nyama ipo? akakujibu "Usije kesho nyama ya kesho ng'ombe hajatoka ukerewe,ni wa hapa hapa halafu ng'ombe nyama tumeipata ki ujanja ujanja" sio salama sana. ungejiskiaje?

unaweza ukaona unakula nyama salama ya ng'ombe ila siri ya hiyo nyama anaijua huyo dogo na maboss zake,vitoto vya namna hyo ni vya kutumia kupata details zako muhimu,chukulia ule upendo wake kama wa mwana na mama,usimtafsiri vingine.
 
Mkuu naona unampigia pande dogo [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
okay, tumekosoma

bucha ya nyama ya Ukerewe iko maeneo gani ?
 
Sasa anaenda kukutana na juchiii lililopoteza matumaini unafikiri ni kazi ndogo??[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119] Sawa bwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enyi watoto wadogo, wakiume, wavulana nani amewaloga?

Mmekuwaje mbona hamna hofu ya kuogopa wakinamama wakubwa waliowazidi umri mara 20000?

Mnapata wapi ujasiri huo?

story iko vile:
Jana nilipita kwenye bucha la nyama ambako huwa ninapenda kununulia hapo kwa kuwa wana nyama ya kutoka wilaya ya Ukerewe. Kwa ufupi nyama inayotokana na ng'ombe wa Ukerewe ni nzuri kwa kuwa ng'ombe wa Ukerewe wanalishwa tu maeneo jirani na nyumbani, hawajachoka na pia nyama ya Ukerewe ina ladha nzuri na ni laini. (sio tangazo za biashara mjue)

Baada ya kununua nyama, wakati nafungua mkoba kutoa hela, hako kavula kakawa kananiangalia sana, na mie nikakazia macho. Kakawa kanaonesha ishara ya kuomba namba za simu (yaani kakawa kanaweka mkono wake kwenye sikio kama vile kanapokea simu). Nilikaelewa nikakausha tu. Nikamlipa mwarabu hela yake.

Nilivyotoka hapo kuelekea kwenye usafiri, ghafla nikaona dogo yuko nyuma yangu. Mazungumzo yakaanza:

Dogo: Mama shikamoo.

Mie: Marahaba.

Dodo: huku akiwa anatoa tabasamu kama la panya, samahani mama naweza kupata namba yako ya simu.

Mie: Kwa ajili ya matumizi yepi?

Dogo: Ili niwe nakupigia kukupa taarifa za nyama inapoingia toka Ukerewe.

Mie: Mbona ratiba naijua tu, kwani ni lini niliikuja hapo nikakosa nyama?

Dogo: hahahaha, basi tuyaache hayo ya nyama, nataka tu nipate namba zako tuwe tunachat, kwa ufupi nimependa uwe mtu wangu!

Mie: Mxeeeewuu (nikaondoka zangu nikakaacha kamesimama hapo)
kwanini usimwambie akukatie kiuno 2 mmalizane
 
Back
Top Bottom