Nimetukanwa matusi ya nguoni na mtoto wa shangazi yangu

litutumbwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
642
Reaction score
1,303
Kwema wandugu
Kuishi na watu kazi sana, kuishi na ndugu kazi sana

Huyu kijana wa shangazi yangu ni mhuni, mlevi, mvivu, si muwajibikaji na hana, nidhamu.

Namgharamia kwa vingi, kuanzia kumlisha, mavazi, malazi na kadhalika

Kazi nimemtafutia mimi, nilitumia jina langu apate kazi ingawa hakuwa na vigezo

Jana amekuja usiku hapa na kuanza kunitukana matusi ya nguoni akinituhumu kwa uongo kuwa namtaka mchumba wake, jambo ambalo ni uongo

Alikuja akiwa amelewa na ana kiboko mkononi ili anichape, oneni alivyo na laana kijana huyu

Akiwa kama mita 25 nje, niliweza kumuona, kutokana na taa za uani na alifunguliwa get na mlinzi kwa kuwa anajulikana hapa

Nikaona ameashika gongo, nikakumbuka yote niliyomfanyia na anayonilipa nikapata hasira sana

Nikiwa ndani bila kutegemea nikavuta pumzi kwa nguvu nikaivuta fimbo yake akiwa kule nje na nikamnyang'anya, nikaanza kumtandika mwenyewe mgongoni na mikononi huku nikiwa ndani

Kama haitoshi huku akiwa nje mimi ndani, nikamtapisha pombe yote na ghafla akili ikamrudi

Alishtuka kuona fimbo yake imemchapa mwenyewe ila hakujua ilikuwaje sababu alikuwa amelewa..

Mke wangu hakuamka alikuwa fofofo

Nimempa nafasi ya mwisho, othrwise next time ataamkia kituoni

Nipo naye hapa anakandwa na shemeji yake

Ndugu sina hamu nao kabisa
 
Mpaka leo hii bado una ndugu??
 
unalea ujinga si umuondoe hapo nyumbn kwako akajitegemee.

kijana anataka uhuru.
 
My guy is back πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„.Nimekumbuka ule mkasa wako uliiojitoa copy ,halafu nakala ikaenda mtaani kufanya mbishe nyingine .Halafu nakala halisi ikabaki na wife imelala.
 
Umempa nafasi mawazoni mwako au umemueleza uso kwa macho?
 
Ulevi mbaya sana, sikuwahi kujua ulevi unaweza kuharibu career ya mtu kabisa.
 
So hapa Content n nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…