Nimetukanwa matusi ya nguoni na mtoto wa shangazi yangu

Nimetukanwa matusi ya nguoni na mtoto wa shangazi yangu

Kwema wandugu
Kuishi na watu kazi sana, kuishi na ndugu kazi sana

Huyu kijana wa shangazi yangu ni mhuni, mlevi, mvivu, si muwajibikaji na hana, nidhamu.

Namgharamia kwa vingi, kuanzia kumlisha, mavazi, malazi na kadhalika

Kazi nimemtafutia mimi, nilitumia jina langu apate kazi ingawa hakuwa na vigezo

Jana amekuja usiku hapa na kuanza kunitukana matusi ya nguoni akinituhumu kwa uongo kuwa namtaka mchumba wake, jambo ambalo ni uongo

Alikuja akiwa amelewa na ana kiboko mkononi ili anichape, oneni alivyo na laana kijana huyu

Akiwa kama mita 25 nje, niliweza kumuona, kutokana na taa za uani na alifunguliwa get na mlinzi kwa kuwa anajulikana hapa

Nikaona ameashika gongo, nikakumbuka yote niliyomfanyia na anayonilipa nikapata hasira sana

Nikiwa ndani bila kutegemea nikavuta pumzi kwa nguvu nikaivuta fimbo yake akiwa kule nje na nikamnyang'anya, nikaanza kumtandika mwenyewe mgongoni na mikononi huku nikiwa ndani

Kama haitoshi huku akiwa nje mimi ndani, nikamtapisha pombe yote na ghafla akili ikamrudi

Alishtuka kuona fimbo yake imemchapa mwenyewe ila hakujua ilikuwaje sababu alikuwa amelewa..

Mke wangu hakuamka alikuwa fofofo

Nimempa nafasi ya mwisho, othrwise next time ataamkia kituoni

Nipo naye hapa anakandwa na shemeji yake

Ndugu sina hamu nao kabisa
Matatizo ya familia yenu unatuletea huku mtandaoni , huko mlipo mmekosa suluhisho kabisa?
 
Mtaa mada anaandika wakati kiwa ndani mlevi nje huyu wa ndani akilifikia gongo la mlevi na kumpiga nalo mgongongoni huku akiwa ndani,pamoja na kumtapisha.
I read between the lies
 
Back
Top Bottom