Nimeua nyoka mkubwa Mikumi

Huyo nyoka itakua alikua amejichokea au kameza kiumbe hawezi kusogea. Asingekuachia nafasi umsogelee zingatia jeki ni fupi inamaana Hadi umpige, ulimkaribia sana.

Na kama hakua na madhara, kwanini umuue? Si ungepita pembeni tu uendelee na safari Yako?
 
Green label
 
Mtaani kuna story Mikumi wameweka Camera,Ukigonga mnyama yeyote utakamatwa! Hii ina ukweli?.
 
Umekosea na pia una case ya kujibu,umeua nyoka hifadhini
 
Kuna watu pia ni nyoka nitakutafuta mkuu uje na jeki yako na fimbo unimalizie.
 
Angalia sana siku moja utajuta kuzaliwa ukaambiwa bei yake milioni tano
 
Morally wewe unakosea sana usiue kiumbe foe no reason yaan unabonda mpaka anakufa huna kazi naye. Huwezijua umeathiri viumbe wangapi kwa kumuua huyo nyoka may be alikuwa na watoto ama mayai, kuna nyani wala nyoka umewadhurumu msosi wao, umewakosesha watanzania kipato coz kuna watalii huja kutazama nyika tu
 
Faini ya kuua nyoka hifadhini ni bei gani, KILA mnyama ana bei yake
 
Nikaona sio kesi, nikashuka nikachukua jeki, nikamtandika mgongoni nadhani nilivunja kabisa uti wa mgongo akawa anarandaranda tu pale nikatafuta kipande cha fimbo nene nikamtandika kichwa shughuli ikaisha nikamtupa pembeni safari ikaendelea.
Usirudie tena huu ujinga. Hebu fikria kama angekuwa koboko ulivyoshuka ungefanyaje?
 
Unauwa Nyala za Serikali
 

Eti nikachukua jeki nikamtandika nayo ya mgongo!!!!daaa,.ngoja nikapupute mchanga kwenye gari kwanza
 
Wewe umo ndani ya gari unakiona kiumbe kinapunga upepo wa alfajiri wala hakina nia ya kuyauma magari, unalianzisha kwa sababu tu ya ubabe unakiua kiumbe kisichokuwa na ugomvi nawe, huo ni ujinga.
Kuua au kukipa chakula kiumbe chochote ndani ya hifadhi ni kosa la jinai.
Nyie ndio mnaoua nyoka akiingia chumbani mwako huku nyoka akiwa hana nia mbaya nawe.
 
Acha uongo. Hivi unamjua koboko au black mamba, yule nyoka ni hatari mno, akikuwahi tu hata dakika 10 hufikishi. Na kwa wewe kumuua siyo rahisi lazima atakimbis tu, na mbio zake siyo utani. Kama kweli umeua koboka tupe picha otherwise wewe mwongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…