Nimeua nyoka mkubwa Mikumi

Kumbe ni wewe, naomba kesho asubuhi ujisalimishe kituo cha polisi kilicho karibu nawe ili tuyamalize mapema la sivyo tunawatonya Maliasili .....!
 
Sasa umeuuwa wa Nini?

Infact wala sio sifa. Huyo nyoka umemfuata hifadhini, ndio kwake hapo ni wewe ndio hukutakiwa kuwa hapo sio yeye. Umemuonea Bure na Wala hujafanya ushupavu wowote!
Kuna mwana alianzisha uzi humu ukisema kila mtu aseme aliwahi piga wanyma gani bila sababu za msingi..!!
 
Habari kama hii usipo weka na kapicha wala hainogi 75% ya wadau tulitegemea kukuta bonge la picha
 
Kwa hiyo ukimkuta mwanaume labor naye atakuwa mama mja mzito?
Mimi mwanaume nikafanye nini labor, ila ukiingia kwenye mbuga ya Mikumi kuna ubao ambao wameorodhesha kiasi cha pesa utakayolipa ukiua kiumbe chochote yaani wanyama, ndege na wadudu, nyoka naye yumo, pia nenda kwenye zoo yoyote ya maliasili utakuta nyoka wanao.
 
Umemdhulumu na umevunja Sheria pia kuuanmnyama pori bila kibali
 
Dah!.. huo ni ujangili, umeua kivuto cha utalii karibu na eneo la hifadhi.
 
Watanzania mnafundishwa makanuni ya hesabu ila hamjui kuwa nyoka akiwa eneo lake akiwa anavuka unatakiwa upunguze mwendo na apite bila kumdhuru kuua viumbe maeneo yao na hana nia ya kukudhuru karma ipo hata kwa viumbe...unashuka kwenye gari unaamua unakuja kujisifu huku wakati panya road mnakimbia hovyo hovyo wala hamji kujisifu hii taarifa mimi sijaipenda kabisa ukizingatia huwa siui viumbe hovyo hovyo tena hifadhini sio nyumbani kwako...wanaposema Elimu yetu ipo chini ni pamoja na matukio kama haya..
 
Hukuua koboko uliua nyoka mkubwa tu.

Koboko siyo mjomba wa kukuona kisha akaendelea kurelax. Anakupelekea moto na unataga mayai ya rangirangile
 
Kwa mtazamo wangu hujafanya sawasawa! Kwa sababu umemkuta eneo lake sahihi kabisa, nyoka ni kiumbe kama viumbe vingine vyote. Ikiwa yuko nyumbani kwenye makazi ya watu unaweza muua, hata hivyo sehemu zenye wataramu huwaita ili waje wamuondoe akiwa hai. Binafsi nikimkuta nyoka porini siwezi wala sijawahi kumuua kwa kuwa ndiyo sehemu yake ya kujifai, bali namfukuza ili apotelee polini.
 
Ushaharibu ikolojia ya mikumi mkuu
 
Nimependa hapo kwenye mstari wa mwisho [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Umehujumu uchumi wa nchi.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…