Nimeuziwa mbwa maeneo ya Victoria, nilipomfikisha nyumbani mume wangu akasema eti sio mbwa ni fisi

Nimeuziwa mbwa maeneo ya Victoria, nilipomfikisha nyumbani mume wangu akasema eti sio mbwa ni fisi

View attachment 2413508
Jana jioni nilipokuwa nikitoka kazini, nikafika Victoria, nikakuta kuna jamaa ana mbwa watatu, wawili wakubwa na puppy mmoja.

Nikavutiwa na puppy nikaenda naye nyumbani. Mume wangu alirudi akiwa amechoka na amepiga mambo yake, lakini nilimjulisha kuwa nimenunua mbwa.

Asubuhi ya leo akaenda kumwangalia, nilikuwa nimemuweka garage sababu bado hatujapata kibanda chake. Nikashangaa mtu ananiita kwa hasira ananizodoa kuwa sina akili kabisa, nimeletaje fisi nyumbani?

Kwa kweli mimi wakati namnunua nilifurahia umbo lake alivyonona, sikujua fisi kuwa wako kama mbwa. Lakini pia nadhani nilirogwa.
Umeuziwa fisi kweny gunia
 
Si tutakamatwa kwa ujangili? Kesho ntaamka saa kumi alfajiri, kwa kuwa siendi kazini nitakabwaga maeneo ya Coco Beach, sitaki kesi mie
Coco Beach utakamatwa na walinzi, Bora umrudishe Serikalini, hawatakukamata, watafanya utaratibu wa kumrudisha, asije akadhuru watu
 
mpeleke ktk ofisi yoyote ya fisi em atakuwa amefika kwao, hyena hynea
 
Tumuamini nani
IMG_20221111_174853.jpg
 
Hii story sio ya kweli umetunga eti puppy wee mjinga nini... [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom