Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,075
- 11,682
Hilo la wanachama wa Chaumma kutaka kurudi Chadema ni muendelezo wa tactics zile zile chafu za kabla ya uchaguzi wa Chadema zilizofanywa na wafuasi wa uongozi wa sasa wa chama hicho. Ni siasa za whispers na wink wink.- Ndugu siasa zetu hizi siku zote hazina visirani vya kudumu, ndio maana tayari tumeshaanza kusikia kelele za wale waliokimbilia Chaumma wakitaka kurejea Chadema. Haya mambo ya mwanachama fulani kupigwa na mlinzi wa kiongozi mwingine, ni issue za kiusalama, sijui kwanini huyo anayedai alipigwa hakuripoti polisi hiyo issue yake, au kufungua kesi mahakamani ili tuone seriousness yake kwenye hilo.
Sigrada hakupeleka kesi polisi kwa sababu alikuwa bado mwanachama wa Chadema na hakutaka kukiharibia chama chake kwa matumaini kuwa hali itabadilika. Alipoona haibadiliki ndio akaamua kukihama na kujiunga na Chaumma.
Aidha, Mbowe alipigwa Dodoma lakini hakupeleka kesi Mahakamani. Lissu alipigwa Mbeya na pamoja na kuahidi kuwa atamfungulia kesi binafsi polisi mwandamizi aliyempiga hakufanya hivyo. Kwa logic inayotumia kwa Sigrada Mbowe na Lissu hawakupigwa kama walivyodai kwa sababu hwakufungua kesi Mahakani?
Dalili zinaonyesha sio hivyo. Ingekuwa hivyo Heche asingeendelea kuwasemea ovyo wanachama wa Chaumma waliotoka Chadema. Sio hulka yake ya kukiri alipokosea. Sidhani kama Suzan angekubali yamalizwe kimya kimya wakati alidhalilishwa hadharani. Heche angekuwa muungwana angetoa public apology maana sio tu Kiwanga ni mkubwa kwake kiumri lakini pia kuheshimu mchango wake alipokuwa Chadema. Nashangaa kwa vitriol hiyo haielekezi kwa watu kama Msigwa ambao walizunguka nchi nzima kuichafua Chadema. Sitashangaa kama kesho Msigwa akiomba kurudi kundini atapokewa kwa mikono miwili na vigelegele wakati watu kama Suzan ambao hawajazunguka nchi nzima kuchafua Chadema wanaonekana kuwa ni maadui wasio stahili msamaha. Kitu pekee ninachoona ni kuwa wakina Suzan walidiriki kutofautiana kimtazamo na uongozi wa sasa wakati Msigwa alikuwa sehemu ya cabal yao ya kumchimba Mbowe.Sio kulalamika tu na kunyamaza, ndio maana nikakwambia mwanzo, haya mambo private ya watu tuyaache, inawezekana pia hawa wameshamalizana sirini.
Kaka yake Lissu alimshauri awe magnanimous in victory hakumsikia. Alikuwa na kila sababu ya kuwakumbatia aliowashinda kwa sababu alishinda kwa kura chache sana. Hiyo ilioonyesha kuwa aliyemshinda alikuwa na watu wa kutosha wanaomuunga mkono. Hakuna mtu aliyesema kuwa uchaguzi haukuwa wa haki. Dhana ya kuonewa iliibuka baada ya uchaguzi ambapo vitendo vya kuwabeza na kuwadhalilisha vilijitokeza. Umesahau jinsi Lissu alivyomshukia Aida Kenani baada tu ya uchaguzi? naamini alifanya hivyo kwa sababu Aida alisimamia uchaguzi wa mwenyekiti wa Bawacha ambapo mtu ambae Lissu alimfanyia kampeni alishindwa? Utakumbuka pia ni katika uchaguzi huo huo Suzan alipinga uongo uliosambazwa na wafuasi wa Lissu kuwa kura zao wampigie chaguo la Lissu? Yote hayo yanawezekana yamechangia chuki dhidi ya Suzan. Sigrada pia aliwaudhi alipomsifia Mbowe kwa kufanikisha mkutano wa Bawacha uliofanyika mara baada ya uchaguzi mbele ya Mwenyekiti Mpya wa Chadema. Vindictiveness iliyoonyeshwa sio ishara ya uongozi bora. Bahati mbaya chuki ile ile waliyoilea inaweza kuwageukia wao wenyewe baada ya kinachodaiwa kuwa ni kauli ya Lissu ya kukubali majadiliano ya kuelekea kwenye maridhiano kama masharti mepesi yatatekelezwa. Heche nae amewaudhi kwa kudiriki kusema kuwa Halima anaweza kusamehewa. Watu wameanza kunong'ona kuwa huo ni usaliti.- Katikati ya ile mihemko iliyokuwepo kabla na baada ya ule uchaguzi wa ndani, ingekuwa ngumu kuwatuliza watu ambao kila mmoja anajiona ameonewa. Issue ilikuwa ni kusubiri mambo yatulie, vikao vya chama vianze kukaa, hapo ndio pangefuata masuala ya kumaliza tofaiti zao.
Waliwabeza kwanza ndio maana wakaamua kutoka Chadema. Tofauti na mnavyosema, kupata ubunge ilikuwa sehemu tu ya strategy yao. Wao waliamini kuwa kushiriki kwa Chadema katika uchaguzi kungewapa nafasi nzuri zaidi ya kujitangaza na kujitayarisha kwa ajili ya uchaguzi wa 030 na hata ule wa 209. Waliamini kuwa Chadema walikuwa katika nafasi nzuri ya kupata wabunge ( Aida angeshinda bila shaka yeyote) ambao wangeendelea kushikilia miguu ya CCM kwenye moto. Aidha chama kingepata ruzuku kubwa kutokana na kura nyingi ambazo wangezipata hata kama wasingetangazwa kushinda. Na walijua muda uliobaki wa kutekeleza mabadiliko makubwa kabla ya uchaguzi ulikuwa mdogo na usingetosha. Walipoona wenzao sio tu kuwa wamekaza shingo bali walianza kuwa chafua wakaona wawapishe. Sidhani kama walitegemea kupata ushindi mkubwa Chaumma bali walitaka kutumia nafasi hiyo kujitangaza upya na kupata ruzuku zitakazowasaidia katika kujitayarisha kwa ajili ya mwaka 2029 na 2030. Haya yote yalikuwa too complicated kwa watu wengi ambao wanapendelea zaidi sound bites kama " No reforms No elections" bila kuelezwa No Elections itafanikishwa vipi.Bahati mbaya kabla mambo hayajatulia, wengine kwa kiu za kutaka kuwa wabunge wakona hawana muda wa kusubiri, hawa ni watu wazima wenye maamuzi yao, walipoamua kuondoka wakaachwa waondoke, Chadema haina mamlaka ya kuingilia maamuzi binafsi ya wengine.
Heche ni kaimu Mwenyekiti wa Chadema na anatakiwa aonyeshe respect hata kwa wale ambao anatofautiana nao. Mbona haoni taabu kukitaja chama cha CCM? Hiki kiburi ndio kitawa cost Chadema. Ni nchi chache sana ambazo zilifanikiwa kuking'oa chama tawala zilifanya hivyo kwa kutegemea chama kimoja tuu cha upinzani. Mara nyingi ni Muungano wa vyama ( vyote au baadhi) vya upinzani ndio ulifanikisha mageuzi hayo. Tabia inayoonyeshwa na Chadema inafanya vyama vingine visite kushirikiana nacho. Chadema wanasahau kuwa mafanikio makubwa ya Chadema yalipatikana wakati vyama vingi vilikubali kushirikiana chini ya Ukawa. Sio rahisi hilo kutokea tena. Wanashau hilo fundisho at their peril.- Sijui unashangazwa nini na Heche kukataa kutaja jina la kina Kiwangwa, Heche hafanyi kazi ya kutangaza vyama vingine, Heche ni M/Mwenyekiti wa Chadema.
Sawa. Asishangae pia wakikataa kuitetea au kushirikiana na Chadema wakati inapitia wakati mgumu. Pride goes before a fall.Kazi ya Heche ni kuisimamia na kuitetea Chadema, hivyo vyama vingine vijisemee vyenyewe. Heche sio msemaji wao, wala sio kiburi cha Heche kama unavyodai.
Ni kuwa disingenous kukataa mchango wa watu wa mtandao katika kufanikisha mageuzi ya uongozi wa Chadema. Sio sababu pekee lakini mchango wao ulikuwa mkubwa.- Wanaharakati hawajawahi kuwafundisha wajumbe wa kamati kuu Chadema wamchague nani. Wale wajumbe ni watu wanaojielewa miaka yote na ndio maana CCM imeshindwa kabisa kupenyeza watu wao kwenye uongozi wa Chadema kwa miaka yote. Nakataa unapodai wanaharakati ndio sababu ya Chadema kubadilisha uongozi wa chama chao.
Ambayo walisubiri kuianza mpaka wapate baraka za CCM. CCM washaisoma namba ya uongozi wa sasa wa Chadema na kujua kuwa ni maneno mengi lakini waoga wa vitendo. Tuone watafanya nini, jeshi likitangaza siku ya usafi tarehe ile ile ambayo waemkusudia kufanya maandamano au mkutano wa hadhara. Tumeona jinsi walivyo rudi nyuma hivi karibuni walipokatazwa kupandisha bendera ya chama chao hivi karibuni. Chadema sasa hivi sio Chadema ya wakina Husna ambae alisimama kidete kukataa bendera ya chama chake kushushwa Chato.- Chadema hawajarudi nyuma, ni CCM ndio inayotaka kuwarudisha nyuma. Ngoja waanze mikutano yao ya hadhara utapata majibu soon.
Maandamano mangapi yamefanywa chini ya uongozi wa Lissu baada ya kukatazwa na dola? Polisi walikuwa wengi kuwazidi waandamanaji wakati wa Mbowe kwa sababu wafuasi wa Chadema pamoja na mijigambo yao ya mtandaoni hawakujitokeza. Maandamano ya mwisho ndio kabisa. Mnyika alijificha kwa masista ili asikamatwe. Lema alikuja kwa ndege akijua thika kuwa atadakwa akiwasili tu Dar es Salaam. Lissu alilala kwake akijua kuwa kitu cha kwanza polisi watakachofanya ni kuzingira nyumba yake. Ni Mbowe pekee ndie alifanya juhudi za kuwakwepa polisi na kujitokeza peke yake na binti yake. Ingawa maandamano yalikuwa ni ya kupinga utekaji na mauaji, hata ndugu walioathirika hawakujitokeza.- Uongozi wa Lissu haujawahi kupata baraka za polisi kuitisha maandamano, hata uongozi wa Mbowe ulivyoitisha maandamano bado tuliona idadi ya polisi ilikuwa kubwa zaidi ya waandamanaji.
Nitasubiri.Hapa tusubiri kama itatokea siku Lissu akiitisha maandamano ndio tufanye comparison.
Hakuna maandamano yaliyofanyika baada ya ripoti za CAG kuonyesha ubadhirifu mkubwa uliokuwa ukifanyika katika mashirika ya umma. Ripoti za CAG hazikuamsha hisia kama clip za Mange zikionyesha magari ya kifahari yaliopaki katika majumba za matajiri na wanaosemekana kuwa watumishi wa umma. Haikuwa na impact kama kuona vijana wakichezea mabulungutu ya DOLA. Hazikuwa na impact kama foto kopi za kilichodaiwa kuwa malipo yaliyofanya na baadhi ya watu pamoja na pesa zinazodaiwa kuwa kwenye akaunti yao ( zinadaiwa kwa sababu hapakuwa na uthibitisho kuwa tuhuma hizo zilikuwa kweli). Sijui kama zile fujo zingetokea kama Chadema waneshiriki kwenye uchaguzi. Sijui. Ninachoamini ni kuwa vijana wengi walishiriki katika zile fujo kwa sababu zao binafsi na sio kwa sababu Chadema imezuiwa kushiriki katika uchaguzi.- Unataka kusema post za Mange zikionesha utajiri wa nchi, na Chadema kutoruhusiwa kushiriki uchaguzi, hiyo sababu ya kwanza ndio ya kweli?!
Umeithibitisha vipi? Rasilimali za nchi zimekuwa zikichezewa miaka yote, unataka kusema watanzania hawakuwa wakijua hilo mpaka walipoona post za Mange? Nop sikubaliani nawe. Bado naamini kama Chadema ingeruhusiwa kushiriki ule uchaguzi, maandamano yasingekuwepo hata kama rasilimali za nchi zinaibiwa na CCM.
29/10 haikuongozwa na wana siasa na ilisukumwa zaidi na hasira binafsi kuliko mambo ya siasa. Ya 09/12 yalikuwa ya kisiasa zaidi ndio maana hayakuwa na traction. Ingekuwa ya 29/10 yalisukumwa na siasa basi ya 09/12 yangefanikiwa kwa sababu mazingira yalikuwa ni yale yale.- Sioni mazingira yaliyobadilika kutoka kile kilichotokea 29.10 na yale maandamano yaliyoitishwa 09 Dec. Kwasababu lengo kuu la yale maandamano ya 09 Dec ilikuwa ni kutaka uchaguzi urudiwe na CCM ikubali.
Watanzania wote walifeli. Shida yetu kubwa ni ya kutegemea ukombolewe badala ya kujikomboa.Sasa kama CCM bado ndio inaunda serikali, na uchaguzi haukurudiwa, wakati ambapo wanaharakati walikuwa wakihimiza maandamano, ni wazi wanaharakati walifeli kwasababu maandamano hayakufanyika.
Asante.
Asante kwako pia. Hasa kwa jinsi unavyo jadiliana kwa kuheshimiana.
Amandla...