Nimewakumbuka Marehemu Mama na Pacha wangu Japo sikuwahi kuwaona kwa Sura

Nimewakumbuka Marehemu Mama na Pacha wangu Japo sikuwahi kuwaona kwa Sura

Pole bidada!
Huwa tunasema Kuna wanawake wana roho ngumu, ila Kuna wanaume wana roho ngumu pia..,! Au Kuna kitu hakikuwa sawa kwa baba yako, ulijaribu kuuliza tatizo nn mpaka akakutelekeza kwa bibi?
 
Historia ya maisha yako inahuzunisha sana. Umekuwa na bahati mbaya sana. Unawajua ndugu za baba yako na mama? Baba yako aliaga kuwa anaenda wapi? Unadhani alikimbia au pengine alipatwa na bahati mbaya bila nyie kujua?
Asante sana.
Ndugu wa mama niliyekuwa namjua ni bibi tu.
Nilikuwa nikimuona bibi tu.
Bibi hakutaka kunieleza kiurefu kuhusu familia au ukoo wao.

Bibi anasema wakati kaletewa mimi ilikuwa siku ya mazishi.
Na watu walipotawanyika ndipo baba nae akatokomea mpaka leo hii.

Historia inasema mama alikuwa kidato cha tatu, akapata mimba ikabidi bibi amtoe shule na kubaki nae nyumbani.
Bibi hakuwa na uwezo kifedha hivo baba akamchukua mama na kulea mimba.
Alipojifungua alikaa miezi 5 ndipo ikatokea ajali na kuja kutelekezewa mimi pale.

Msiba ulipoisha baba alimwambia bibi kuwa anawasindikiza rafiki zake, ndio ikawa mwisho wa kumuona pale kwake.
Bibi kafariki, baba hajui na hata mimi nimekuwa mkubwa sasa simjui kabisa baba yangu.
 
Pole bidada!
Huwa tunasema Kuna wanawake wana roho ngumu, ila Kuna wanaume wana roho ngumu pia..,! Au Kuna kitu hakikuwa sawa kwa baba yako, ulijaribu kuuliza tatizo nn mpaka akakutelekeza kwa bibi?
Hakukuwa na tatizo.
Na bibi huwa hakupenda kumzungumzia baba kabisa.

Na hata nilipokuwa binti kila nikiuliza kuhusu alipo baba, huwa alikuwa anasema kuwa aliniacha hapo na hajui kuhusu yeye
 
Pole mkuu yote mipango ya mola,alitakalo yeye ndio Huwa,.

Mimi pia tulizaliwa pacha na mwenzangu binti kiziwi Mungu mkubwa wote tupo hai ila tu hatuna mahusiano mazuri kila siku ugomvi,shari,..
Pole sana.
Jaribuni kukaa chini mmalize tofauti zenu
 
Hapana
Haina haja naona.
Sasa hv nimeshakuwa na nina maisha yangu.
Sioni hata ulazima wake sasa.
Kama hujapata mwenza, nakutakia kila la kheri upate mwenza mzuri, atayeelewa hali yako, na awe kama ndiye baba, mama na ndugu yako. Asikunyanyase wala kukufanya ukajuta na kusema ''laiti ningekuwa na ndugu haya nisingenyanyasika''.
 
Hapana
Haina haja naona.
Sasa hv nimeshakuwa na nina maisha yangu.
Sioni hata ulazima wake sasa.
Haitabadirisha uhalisia kuwa ni baba yako.

1. Forgive yourself.
2. Forgive your parents.
3. Forgive others.

Hii husaidia sana kuondoa msongo wa mawazo na Blood Pressure. Na ukimsamehe huyu mzee utabarikiwa zaidi.
 
Unahisi suala la kuondokewa na mke na mtoto halikumuathiri......akiweza kurudi msamehe tu hujui alipitia Hali Gani
Sidhani kama lilimuathiri maana naambiwa alishawahi kwenda kwa bibi kutaka mama akae pale maana yeye hataki kuishi na mtu.
Naona baada ya msiba ndipo akapata nafasi nzuri ya kutumiza malengo yake.

Sidhani kama hata namkumbuka ni miaka mingu mno
 
Kama hujapata mwenza, nakutakia kila la kheri upate mwenza mzuri, atayeelewa hali yako, na awe kama ndiye baba, mama na ndugu yako. Asikunyanyase wala kukufanya ukajuta na kusema ''laiti ningekuwa na ndugu haya nisingenyanyasika''.
Asante sana.
Nashukuru Mungu japo niliishi maisha ambayo sikuyawaza kabla.

Ila kufiwa na mama na kutelekezwa na baba ni jambo gumu sana
 
Back
Top Bottom