Nimewakumbuka Marehemu Mama na Pacha wangu Japo sikuwahi kuwaona kwa Sura

Nimewakumbuka Marehemu Mama na Pacha wangu Japo sikuwahi kuwaona kwa Sura

Sijui kama nitaweza kumsamehe hata kama nikimpata.
Alifanya nikulie kwenye maisha ambayo hayakuwa ndoto yangu.
Pole sana , huwezi jua kwanini ilikua vile na matokeo yakawa haya.
Likuepukalo halikosi heri.
 
Avatar yako imenifanya kushindwa kusoma na kupitia Uzi wote naogopa itanishawishi mabaya.
 
Muda huu nimejikuta ghafla namkumbuka marehemu mama yangu, Mama mapacha Nusratt na Nasra.

Tulizaliwa mapacha na mimi nikiwa Dotto.
Kwa bahati mbaya nasikia mama alipata ajali akiwa na Kulwa (Nasra) wakati wakitoka hospitali ambako Kulwa alikuwa anaugua mafua na homa.

Mama na pacha wangu walisukumwa na gari dogo, Nasra alifia palepale eneo la ajali na mama alifia hospitali masaa machache baada ya kufikishwa hospitali.
Naambiwa nilikuwa na miezi 5 tu.

Baada ya maziko, baba yangu alinipeleka kwa bibi mzaa mama na hakuwahi kurudi tena mpaka leo hii.

Nimekua mkubwa sasa bila kuijua sura halisi ya mama yangu, pacha wangu Nasra wala sura ya baba yangu, zaidi ya kuwaona kwenye picha.

Huenda Nasra asingeugua siku ile, basi tungekuwa tuko familia kamili yaani sisi watoto, baba na mama yetu.

Niliendelea kukua nikijua bibi yangu ndie mama yangu mzazi mpaka pale siku moja aliponiambia ukweli kuhusu mimi, pacha wangu na wazazi wangu.

Nililia sana japo haikubadilisha uhalisia.
Bibi alinilea na kunisomesha kwa juhudi zote.
Aliuza mazao ili niende shule na hatimaye chuo.

Nilifanikiwa kiasi kupata elimu na kujiajiri.
Ila kabla bibi yangu hajafaidi matunda yangu vizuri, Mungu nae akamchukua bibi yangu.

Nimejikuta nakumbuka nilikotoka, nilipokuwa na hapa nilipo.

Mungu aendelee kumrehemu mama yangu, bibi yangu na pacha wangu. Hao ndio ndugu zangu kwani sikuwahi kumjua ndugu yangu yeyote yule.

Baba yangu alinitelekeza hivyo wala sitaki kujua kuhusu yeye.

Nimejikuta nawakumbuka sana.

View: https://youtu.be/cVb7QxyiuR4?si=eoSwWTiW4vt4z_K3

Nyanyuka upambane my dear. Mungu alivyo wa ajabu katika maisha haya haya ukifanikiwa utawajua ndugu wengi tu na hata baba yako. Watakutafuta na kutaka kuwa karibu yako. Lakin usiache kumshukuru Mungu kuwa uko hai na ulipata bibi aliyekupenda. So humu dunian hutakosa watu ambao japo sio ndugu wa kuzaliwa watakuwa ndugu wa kufaana na maisha yataenda. Tumekutana tu kwenye maisha haya katika zama hiz ungeweza kuzaliwa miaka 1775 huko lakin umezaliwa sasa na sisi ndio ndugu zako kwenye safari hii. I one dunia kwa ukubwa wake na uzur wake. Pambana hakuna anaekupenda zaid ya Mungu aliyekuumba. So usimsahau. We ni mtu mkubwa na upo kwasababu maalumu. Yesu anakupenda.
 
Sijui kama nitaweza.
Pole sana Nusrat🥲.
mtafute tu babaako na sio kwa kulazimisha.
Kuonana tu,
Mi ni Baba pia, kwakisa hiki nimegundua kwanini wanangu wanantukana full full.
Ni watu wazima sasa, siwategemei chochote.
Ila nikigusa kitu tu kinawahusu wataporomosha matusi mpk basi.
Nimeelewa ni Bond ya mzazi na mtoto tu kuwa mbali.
Wote wamelelewa na mama, bibi zao.
 
Pole sana Nusrat🥲.
mtafute tu babaako na sio kwa kulazimisha.
Kuonana tu,
Mi ni Baba pia, kwakisa hiki nimegundua kwanini wanangu wanantukana full full.
Ni watu wazima sasa, siwategemei chochote.
Ila nikigusa kitu tu kinawahusu wataporomosha matusi mpk basi.
Nimeelewa ni Bond ya mzazi na mtoto tu kuwa mbali.
Wote wamelelewa na mama, bibi zao.
Asante sana babukijana Ndio, wakati mwingine ni uchungu sana hupelekea hali hio kwa watoto pale wanapokataliwa.
Pole sana ila mimi nilishaapa kuwa sitamtafuta maana alinifanya niishi maisha siyo.
 
Back
Top Bottom