Nimewaza kufanya blogging kama part time, kiuhalisia kwa hapa bongo nitaweza kunufaika kiuchumi?

Nimewaza kufanya blogging kama part time, kiuhalisia kwa hapa bongo nitaweza kunufaika kiuchumi?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kutinga kwenye uwanja, nimekuwa nikicheki interviews za lisaa ama zaidi kwa bloggers waliofanikiwa na kiukweli natamani walau nipate walau hata theluthi ya mafanikio yao hasa napoona kwamba ushindani wa blogs bado ni mdogo hapa kwetu kwenye niche kibao ukiachana na udaku, michezo, siasa, mapenzi, tiba ambako kuna ushindani mkubwa.

Kwa sasa mimi ni fundi seremala na ni kazi naifanya tangu 2013 baada ya kuumaliza mwendo wa safari ya elimu form 4. Ok, turudi kwenye main topic, Blogging nayotaka kuifanya ni safi.

Natilia msisitizo nataka nifanya blogging safi maana nliwahi kufatilia haya mambo kwa kina nikaja kugundua kuna bloggers wanafanya kazi yao kwa mbinu nyeusi, hitaji la msingi kwa blogging huwa ni kupata watembeleaji, sasa wao wanachofanya ni kwamba wanadukua account za facebook alafu hizo account wanaanza kuzitumia ku sambaza picha za uchi zenye link za blogs zao. Watu wakiminya hizo picha wanapelekwa kwenye blog yake, Ukiona account ya rafiki yako inasambaza picha za ajabu jua kwamba ishapigwa.

Sasa tukija kwa upande wangu nataka nifanye kazi inayoeleweka, niwe na blog kama ya ajira, miziki, michezo, n.k. nataka watembeleaji wangu wanapoingia kwenye blog wakute walichokifata.

My plan

Ntaanza blogging 2023,

Ntafanya blogging kwa kitu ambacho nakijua tayari na nakipenda ili hata msomaji ajue kwamba najua nachoandika

Jina la website (domain) ambalo huwa ni kama www.dddd.com ntanunua kwa elf 30, hosting ambayo ndio itashikilia mafaili ya website kama picha, maandishi, n.k nayo ntalipia kwa mwaka nadhani itakuwa laki.

Nimeanza kuandka posts zenye maneno 500, post moja ni kila baada ya siku 2 ama 3. hadi sasa zipo 8 na naendelea, kufikia june mwakanu nataka ziwepo walau 50. Post ndio chakula cha blog, post zinavyozidi kuwa nyingi zinachangia haa kuifanya blog yako iwe kwenye matokeo ya juu pale mtu akisechi google.

Kuhusu kipato naendelea kuchunguza ila nimeona niwe nauza kitabu changu na kuuza vifaa vinavyohusiana na blog, mfano kwa wanaohitaji maelezo zaidi na mifano ya ziada wanaweza kunitumia elf 2 ili niwarushie kitabu kwa whatsapp, Pia katika vitu navyozungumzia kwenye blog endapo mtu hajui kwa kukipata basi naweza kumuuzia na kumtumia hata kwa njia ya basi.

Niliwahi kujaribu bloging kabla ya maamuzi haya, nilifanya kwa majaribio tu niliandika posts kama 4 zenye maneno kama 100 hadi 200 kwa kila post, nikaanza kupata watembeleaji 10 kwa siku, wakaja 50, wakaja 100, wakaja 200 na sasa wapo kwenye 400, kumbuka hapo niliandaa blog ya majaribio tu.... kwa sasa nataka nitengeneze blog kabisa iwe official
 
Blogging nayotaka kuifanya ni safi,

Natilia msisitizo nataka nifanya blogging safi maana nliwahi kufatilia haya mambo kwa kina nikaja kugundua kuna bloggers wanafanya kazi yao kwa mbinu nyeusi, sii ya blogging huwa ni kupata watembeleaji, sasa wao wanachofanya ni kwamba wanadukua account za facebook alafu hizo account wanaanza kuzitumia ku sambaza picha za uchi zenye link za blogs zao, watu wakiminya hizo picha wanapelekwa kwenye blog yake ambayo haina hata cha maana, utaambiwa uminye sehem na ukiminya wao ndio wameshaingiza pesa hapo. Ukiona account ya rafiki yako inasambaza picha za ajabu jua kwamba ishapigwa.

Sasa tukija kwa upande wangu nataka nifanye kazi inayoeleweka, niwe na blog kama ya ajira, miziki, michezo, n.k. nataka watembeleaji wangu wanapoingia kwenye blog wakute walichokifata.

Je mnanishauri vipi wana jamii forums
Anza na utafanikiwa sana. Nasisitiza sana. Cha muhimu tu, uwe na passion na blogging. Ukiwa na passion basi utajikuta kila uchao una content very engaging kwahiyo audience utaipata na before u know it, blog inaanza kukuingiza hela. It takea time ila ukiwa patient, it will pay off. Good Luck
 
Anza na utafanikiwa sana. Nasisitiza sana. Cha muhimu tu, uwe na passion na blogging. Ukiwa na passion basi utajikuta kila uchao una content very engaging kwahiyo audience utaipata na before u know it, blog inaanza kukuingiza hela. It takea time ila uliwa patient, it will pay off. Good Luck
Yes, hapo kwenye kuandika kitu nachokipenda ndio nimetilia mkazo,

Najua inaweza kuwa safari ndefu lakini pindi nikiweza kuzikamilisha post kama 100 hivi ntaanza kupata watembeleaji kadhaa kutoka kwa wale wanaotafuta vitu navyoviandika kwenye blog yangu,

Silaha kuu ni kupata watembeleaji wa google, yani mtu akisechi kitu flani basi kwenye matokeo angalau blog yako iwe kwenye matokeo matatu ya juu.
 
Langu jicho ila kikubwa ni content na watazamaji haimek sense kutengeneza post zisizokuwa na watazamaji pia tupo kuona feilture yako maana hii kazi uvumilivu maana hata demu wako anaweza asiopen link uliyotuma

IM HERE IF YOU NEED ANY TECHNICAL ASSISTANCE
 
Nitakuwa regular reader wako uki post vitu vinavyoni interest. Mfano ukiandika kuhusu sports I won't visit
 
hata demu wako anaweza asiopen link uliyotuma
Content ni kwajili ya watu interested, Ntashangaa mtu blog yake ni ya kunyanyua vyuma then anamtumia link mwanamke ambae hayupo interested.

Na ndio maana source nzuri ya watembeleaji ni google, mtu anasechi kitu kwahio hata akiingia kwenye blog anajua kabisa alichokifata

Sihitaji kumlazimisha mtu kuingia kwenye blog, mtu mwenye uhitaji ndie soko
 
Ndio ujue pia kuset SEO
 
Ndio ujue pia kuset SEO
Competition ya SEO kwa hapa bongo bado ni ndogo na ndio maana hata mimi nimeona nianzie hapa bongo.

Kufanya blogging kwa kiigereza sana sana hizi general niches unaweza kutolewa knockout, unashindana na wataalam wengi wa seo kutoka india, uk, usa, canada, china, n.k yani kwanza huko bloggers wanaenda extra mile kwa kuandika content zenye maneno elf 2, back links za kutosha, grammer imenyooka, links building, speed optimization, internal linking, keyword research iliyoshiba, n.k.

Huko nisubiri tu nisije kupata pressure, naanzia bongo hapa hapa kuna blogs hazina seo ya aina yoyote lakini zipo namba 1 kwenye matokeo ya google, hawa ndio ntaendana nao kwa kuongezea vitu kidogo,
 
Competition ya SEO kwa hapa bongo bado ni ndogo na ndio maana hata mimi nimeona nianzie hapa bongo.

Kufanya blogging kwa kiigereza sana sana hizi general niches unaweza kutolewa knockout, unashindana na wataalam wengi wa seo kutoka india, uk, usa, canada, china, n.k yani kwanza huko bloggers wanaenda extra mile kwa kuandika content zenye maneno elf 2, back links za kutosha, grammer imenyooka, linking social media, internal linking, keyword research iliyoshiba, n.k.

Huko nisubiri tu nisije kupata pressure, naanzia bongo hapa hapa kuna blogs hazina seo ya aina yoyote lakini zipo namba 1 kwenye matokeo ya google,
Naona ninaongea na bwana mdogo just do as you can but kukata tamaa ndio adui.
 
Kwa wabongo ukiandika story za umbeya, uchawi na majungu utafanikiwa
Michezo.
Mapenzi
Tiba
Umbeya

Hizi ni wide niches zina blogs kibao sana. Hata uwe na website kali si rahisi kufika namba moja, hapa unahitaji kazi ya ziada.

Binafsi nimelenga sehemu ambayo hata bloggers ni wachache na haa blogs zilizopo kuna mbinu ya kuzipiku
 
Mafanikio ni bahati na juhudi nirahisi kusikia na kuamini kuwa mtu kafanikiwa bila juhudi kubwa ila ni kawaida kusikia kuwa mtu kafeli japo na mafanikio yake mimi ninauzoefu wa miaka na unachofanya chakukushauri weka malengo sikuzote usimulike tochi miguuni wala kuleeeee milimani piga kati jua tu sio wote watakubali ulichofanya bado kunakuvunjika moyo katika safari yako

All in all mm sipendi kuandika sana ila jaribu sometime kufikiri mara tatu kabla ya kutoa hzo fack sisemi sio fact lahasha ila mdamwingine hazitasaidia kuwa na malengo marefu nje ya unavyofikiri katika blogging at the first moment do as passion yaan kama kitu unachopenda ila ukiingiza tamaa ya oesa kwa haraka na kuanza kuweka pop-ups ndo umetukosa mafanikio hata mwaka yanaweza chukua na zaidi au chini ya hapo kijana
mimi nimejaribu kuongea kwa facts hivyo nakuomba wewe mzoefu ujibu kitaaam kama hutomind
 
Mafanikio ni bahati na juhudi nirahisi kusikia na kuamini kuwa mtu kafanikiwa bila juhudi kubwa ila ni kawaida kusikia kuwa mtu kafeli japo na mafanikio yake mimi ninauzoefu wa miaka na unachofanya chakukushauri weka malengo sikuzote usimulike tochi miguuni wala kuleeeee milimani piga kati jua tu sio wote watakubali ulichofanya bado kunakuvunjika moyo katika safari yako

All in all mm sipendi kuandika sana ila jaribu sometime kufikiri mara tatu kabla ya kutoa hzo fack sisemi sio fact lahasha ila mdamwingine hazitasaidia kuwa na malengo marefu nje ya unavyofikiri katika blogging at the first moment do as passion yaan kama kitu unachopenda ila ukiingiza tamaa ya oesa kwa haraka na kuanza kuweka pop-ups ndo umetukosa mafanikio hata mwaka yanaweza chukua na zaidi au chini ya hapo kijana

Na ndio maana nimesema nafanya blogging safi hizo pop ups nimecheki interviews wengi hawazipendi na zina discourage watembeleaji.

Swala la pop ups niishalifatilia na niliona bloggers wanazikataa, Nilichoamua ni kuingiza kipato kwa kuuza kitabu cha pdf kwa wanaotaka maelezo zaidi kwa shilingi elf 2 na kuuza bidhaa zinazohusishwa na blog kwa ambao hawawezi kuzipata.

Binafsi nina blog tayari niliwahi kuianzisha kwajili ya majaribio niliiacha na kila siku huwa inaingiza watu 100, hio niliifanya kwa majaribio tu bila kuwa serious.
 
nilitengeneza kiblog cha majaribio naona kinaingiza watu 400 kwa siku.

Wote ni kutoka google, wakisechi kwenye google wanaikuta blog yangu.

naamini kwa ushindani mdogo wa blogs za bongo ukijiongeza kidogo tu unakaa nafasi nzuri kwenye matokeo ya google. hapa kama unavyoona watembeleaji wangu hawapungui elf 10 kwa mwezi, na ilikuwa ni majarbio tu.

1671651582730.png
 
nilitengeneza kiblog cha majaribio naona kinaingiza watu 400 kwa siku.

Wote ni kutoka google, wakisechi kwenye google wanaikuta blog yangu.

naamini kwa ushindani mdogo wa blogs za bongo ukijiongeza kidogo tu unakaa nafasi nzuri kwenye matokeo ya google.

View attachment 2453971
Hzo statistics gawanya kwa tatu ndio huenda ikawa idadi ya real visitors maana kunatatizo na statistics za blogger
 
Back
Top Bottom