Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kutinga kwenye uwanja, nimekuwa nikicheki interviews za lisaa ama zaidi kwa bloggers waliofanikiwa na kiukweli natamani walau nipate walau hata theluthi ya mafanikio yao hasa napoona kwamba ushindani wa blogs bado ni mdogo hapa kwetu kwenye niche kibao ukiachana na udaku, michezo, siasa, mapenzi, tiba ambako kuna ushindani mkubwa.
Kwa sasa mimi ni fundi seremala na ni kazi naifanya tangu 2013 baada ya kuumaliza mwendo wa safari ya elimu form 4. Ok, turudi kwenye main topic, Blogging nayotaka kuifanya ni safi.
Natilia msisitizo nataka nifanya blogging safi maana nliwahi kufatilia haya mambo kwa kina nikaja kugundua kuna bloggers wanafanya kazi yao kwa mbinu nyeusi, si ya blogging huwa ni kupata watembeleaji, sasa wao wanachofanya ni kwamba wanadukua account za facebook alafu hizo account wanaanza kuzitumia ku sambaza picha za uchi zenye link za blogs zao.
Watu wakiminya hizo picha wanapelekwa kwenye blog yake ambayo haina hata cha maana, utaambiwa uminye sehem na ukiminya wao ndio wameshaingiza pesa hapo. Ukiona account ya rafiki yako inasambaza picha za ajabu jua kwamba ishapigwa.
Sasa tukija kwa upande wangu nataka nifanye kazi inayoeleweka, niwe na blog kama ya ajira, miziki, michezo, n.k. nataka watembeleaji wangu wanapoingia kwenye blog wakute walichokifata.
My plan
Ntaanza blogging 2023,
Ntafanya blogging kwa kitu ambacho nakijua tayari na nakipenda ili hata msomaji ajue kwamba najua nachoandika
Nimeanza kuandka post moja yenye maneno 500 kila baada ya siku 2 ama 3. hadi sasa zipo 8 na naendelea, kufikia june mwakanu nataka ziwepo walau 50. Post ndio chakula cha blog, post zinavyozidi kuwa nyingi zinachangia haa kuifanya blog yako iwe kwenye matokeo ya juu pale mtu akisechi google.
Kuhusu kipato naendelea kuchunguza ila nimeona niwe nauza kitabu changu na kuuza vifaa vinavyohusiana na blog, mfano kwa wanaohitaji maelezo zaidi na mifano ya ziada wanaweza kunitumia elf 2 ili niwarushie kitabu kwa whatsapp, Pia katika vitu navyozungumzia kwenye blog endapo mtu hajui kwa kukipata basi naweza kumuuzia na kumtumia hata kwa njia ya basi.