Nimewaza kufanya blogging kama part time, kiuhalisia kwa hapa bongo nitaweza kunufaika kiuchumi?

Nimewaza kufanya blogging kama part time, kiuhalisia kwa hapa bongo nitaweza kunufaika kiuchumi?

sasa mkuu wewe umesema posts nyingi hazisaidii seo, mimi nimekuletea mfano wa kukuonyesa jinsi zinavyo saidia seo.... Ingependeza unielimishe kwa mrengo wako ni vipi posts nyingi hazisaidii seo.

Kuniambia tu kwamba mimi ni mbishi haitoshi, Nakuomba unielimishe kwa kunipa details, huu mtandao wa jamii forums naamini huku ni home of great thinkers wanaotoa majibu yaliyoshiba.
mkuu nakuitaji PM tafadhari
 
Yes, hapo kwenye kuandika kitu nachokipenda ndio nimetilia mkazo,

Najua inaweza kuwa safari ndefu lakini pindi nikiweza kuzikamilisha post kama 100 hivi ntaanza kupata watembeleaji kadhaa kutoka kwa wale wanaotafuta vitu navyoviandika kwenye blog yangu,

Silaha kuu ni kupata watembeleaji wa google, yani mtu akisechi kitu flani basi kwenye matokeo angalau blog yako iwe kwenye matokeo matatu ya juu.
Hivi ni teknolojia gani inatumika hapa ili mtu akitumia search engine apate matokeo ya blog fulani.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Hivi ni teknolojia gani inatumika hapa ili mtu akitumia search engine apate matokeo ya blog fulani.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
ushindani unachangia sana mtu akisearch kitu flani google, matokeo yakija zinatokea blogs nyingi, zile za juu kule mwanzo mwanzo hasa 3 bora ndio zitaingiliwa zaidi.

google wana sheria zao za kuifanya blog iwe juu kwenye matokeo, vipo vitu kibao sana kama quality content, kupangilia vizuri headings na sub headings, kujenga utandu wa links za ndani ya websites, back-links, n.k.

mfano nikigusia hapo kwenye back-links ni kwamba kama blog yako imekuwa reffered links zake kupachikwa kwenye blogs ama websites kubwa, google itaipendelea blog yako, mfano blog yako ikiwekwa link yake kama source ya habari flani kwenye websites kama bbc, cnn, n.k. hii ni point inayoifanya blog ipendelewe na google kwa kuongeza uwezekano wa kuwemo kwenye matokeo ya mwanzo kwenye google.
 
Hapo nimeelewa. Nitaitafuta hii elimu ya Blogging maana mm huwa naandika na kuuza mawazo yangu kwa bei ya hasara!

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
blogging sio mchongo nowadays , jaribu kwenda na kasi ya ulimwengu, ila hata sijui nikushauri ufanye nini!
Kweli, blog ilikuwa habari ya mjini enzi hizo hakuna Instagram na kipindi matumizi ya YouTube yako chini hapa bongo, nakumbuka enzi hizo Millard Ayo alikuwa na blog maarufu sana, wengine kina Issa Michuzi, Mange Kimambi n.k ila upepo wa blog ulikuja kuuliwa na Instagram, umbea wote na habari unazipata huko
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kutinga kwenye uwanja, nimekuwa nikicheki interviews za lisaa ama zaidi kwa bloggers waliofanikiwa na kiukweli natamani walau nipate walau hata theluthi ya mafanikio yao hasa napoona kwamba ushindani wa blogs bado ni mdogo hapa kwetu kwenye niche kibao ukiachana na udaku, michezo, siasa, mapenzi, tiba ambako kuna ushindani mkubwa.

Kwa sasa mimi ni fundi seremala na ni kazi naifanya tangu 2013 baada ya kuumaliza mwendo wa safari ya elimu form 4. Ok, turudi kwenye main topic, Blogging nayotaka kuifanya ni safi.

Natilia msisitizo nataka nifanya blogging safi maana nliwahi kufatilia haya mambo kwa kina nikaja kugundua kuna bloggers wanafanya kazi yao kwa mbinu nyeusi, hitaji la msingi kwa blogging huwa ni kupata watembeleaji, sasa wao wanachofanya ni kwamba wanadukua account za facebook alafu hizo account wanaanza kuzitumia ku sambaza picha za uchi zenye link za blogs zao. Watu wakiminya hizo picha wanapelekwa kwenye blog yake, Ukiona account ya rafiki yako inasambaza picha za ajabu jua kwamba ishapigwa.

Sasa tukija kwa upande wangu nataka nifanye kazi inayoeleweka, niwe na blog kama ya ajira, miziki, michezo, n.k. nataka watembeleaji wangu wanapoingia kwenye blog wakute walichokifata.

My plan

Ntaanza blogging 2023,

Ntafanya blogging kwa kitu ambacho nakijua tayari na nakipenda ili hata msomaji ajue kwamba najua nachoandika

Jina la website (domain) ambalo huwa ni kama www.dddd.com ntanunua kwa elf 30, hosting ambayo ndio itashikilia mafaili ya website kama picha, maandishi, n.k nayo ntalipia kwa mwaka nadhani itakuwa laki.

Nimeanza kuandka posts zenye maneno 500, post moja ni kila baada ya siku 2 ama 3. hadi sasa zipo 8 na naendelea, kufikia june mwakanu nataka ziwepo walau 50. Post ndio chakula cha blog, post zinavyozidi kuwa nyingi zinachangia haa kuifanya blog yako iwe kwenye matokeo ya juu pale mtu akisechi google.

Kuhusu kipato naendelea kuchunguza ila nimeona niwe nauza kitabu changu na kuuza vifaa vinavyohusiana na blog, mfano kwa wanaohitaji maelezo zaidi na mifano ya ziada wanaweza kunitumia elf 2 ili niwarushie kitabu kwa whatsapp, Pia katika vitu navyozungumzia kwenye blog endapo mtu hajui kwa kukipata basi naweza kumuuzia na kumtumia hata kwa njia ya basi.

Niliwahi kujaribu bloging kabla ya maamuzi haya, nilifanya kwa majaribio tu niliandika posts kama 4 zenye maneno kama 100 hadi 200 kwa kila post, nikaanza kupata watembeleaji 10 kwa siku, wakaja 50, wakaja 100, wakaja 200 na sasa wapo kwenye 400, kumbuka hapo niliandaa blog ya majaribio tu.... kwa sasa nataka nitengeneze blog kabisa iwe official
Blogs ina fursa sana hasa ukiweza kufanya SEO na kuattract site visitors kwa ajili ya ad revenue. Pia kuweza kuendesha bloga mbalimbali kwa ajili ya commissions ni mojawapo ya advantages
 
Blogs ina fursa sana hasa ukiweza kufanya SEO na kuattract site visitors kwa ajili ya ad revenue. Pia kuweza kuendesha bloga mbalimbali kwa ajili ya commissions ni mojawapo ya advantages
blog ukiifanya huku ukijua unachokifanya basi wala hupati tabu, tatizo wengi tunafanya tukitanguliza pesa in mind kwanza unakuta mtu
- hana genuine content
  • hana mbinu za seo
  • hata topic inayoeleweka
utaona maisha ya blogging ni magumu sana, btw blogging sasa hivi ni old fashion
 
Ni kweli kabisa mkuu, mambo inabidi uwe na passion nayo ili uweze kufika mbali
 
Vipi kuhusu usajili wa blog kwa upande wa TCRA? Ukiwa na blog unapaswa kulipia sh' ngapi?
 
kuwa na post nyingi kunasaidia sana tu..

Blog ikiwa na post nyingi nako kunasaidia, inakua kama duka lenye bidhaa nyingi ambazo hazipo kwenye duka dogo.
Kwanza, Search Engine sio duka mkuu. Kama Search Engine ingekuwa ni duka basi watu wangekuwa wanalipia ili post zao ziwe rank nzuri.

Pili, naomba utofautishe website rank na post rank. Kuwa na post nyingi kunaweza kusaidia website iwe na rank nzuri lakini kuwa na post nyingi hakuwezi kufanya post iwe na rank nzuri kwenye search results. Ili post yako iweze kuwa na rank nzuri kwenye search results, you must optimize it well.
 
I can't wait kuanza rasmi hii ishu, nishaandika Post zangu zaidi ya 90 zenye maneno zaidi ya 800 kila post bado kuzifanyia lundering kwajiri ya kuzipost Pesa ya kuanzia 120,000 Tzs ndio inanichelewesha hadi sasa
 
Back
Top Bottom