Nimewaza kufanya blogging kama part time, kiuhalisia kwa hapa bongo nitaweza kunufaika kiuchumi?

Hzo statistics gawanya kwa tatu ndio huenda ikawa idadi ya real visitors maana kunatatizo na statistics za blogger
Sio mbaya kwa blog niliyofanyia majaribio hasa ukizingatia niliitengeneza fasta fasta tu na kuweka post chache fupi fupi kisha nikaacha,

Kwa sasa nataka nifanye iwe serious kabisa, Nataka nihamie word press na sio blogger niliyofanyia majaribio, nataka niandika maneno angalau 500 kwa post na sio 100 hadi 200 nilipofanya majaribio, nataka ziwepo post za kutosha na sio kama blog ya majaribio hazifiki hata 6, backlinks ntaweka pia hata kwa humu jf, n.k.

Yaani navyoonaga zile interviews za bloggers wa marekani jinsi ushindani wao ulivyo mkubwa halafu nikicheki huku kwetu naonaga kama fursa inanipita.
 
Kama uko creative na una story fupi fupi za kuvutia bora youtube, video za dakika mbili mpaka nne kama zinavutia unaweza kufanikiwa
youtube kwa sasa hali tete, mabando ni ghali mno, hata wasanii maarufu tuliowazoea kuwaona wakipata views milioni kwa masaa kwa sasa wanazitafuta hata kwa wiki
 
Ningekua na uwezo ningekushauri uanze youtube
 
Mkuu na wewe ni blogger
 
Kuna mengi usiyo yafahamu kuhusu Search Engine Optimization (SEO). Kuwa na post nyingi kwenye blogu au tovuti, hakuwezi kufanya posti hizo ziweze kuwa na rank nzuri kwenye search results.
 
Kuna mengi usiyo yafahamu kuhusu Search Engine Optimization (SEO). Kuwa na post nyingi kwenye blogu au tovuti, hakuwezi kufanya posti hizo ziweze kuwa na rank nzuri kwenye search results.
kuwa na post nyingi kunasaidia sana tu..

Blog ikiwa na post nyingi nako kunasaidia, inakua kama duka lenye bidhaa nyingi ambazo hazipo kwenye duka dogo.
 
Nilichokiona kwa NetMaster ni mbishi na asietaka kujifunza anasimamia sana misimamo yake hiko ndio kitakachomfelisha huyu jamaaa
 
Nina blog ila kinacho nichanganya post kutokuonekana kwenye google search
Jaribu kufanya haya nunua Domain name, tumia custom pro blogger themes zilizo na onpage seo, kumbuka kuweka label na search description kila unapopost post mpya, set vizuri sitemap na angalia settings za robot hapo usijekuwa umelock post kuwa indexed jisajili na uweke sitemap kwenye search console na bingwebmaster kila mda ambapo google italeta error kuhusu indexing fix, fanya keyword research unapotengeneza post
Yote yakifeli amia WordPress
 
Dionwillz angalia kilicho pelea hapo nje na domain name
 
Ndugu nimekuongezea traffic ila sipo vizuri kabisa kwenye swala la content wala layout sina hata comment
 
Nilichokiona kwa NetMaster ni mbishi na asietaka kujifunza anasimamia sana misimamo yake hiko ndio kitakachomfelisha huyu jamaaa
sasa mkuu wewe umesema posts nyingi hazisaidii seo, mimi nimekuletea mfano wa kukuonyesa jinsi zinavyo saidia seo.... Ingependeza unielimishe kwa mrengo wako ni vipi posts nyingi hazisaidii seo.

Kuniambia tu kwamba mimi ni mbishi haitoshi, Nakuomba unielimishe kwa kunipa details, huu mtandao wa jamii forums naamini huku ni home of great thinkers wanaotoa majibu yaliyoshiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…