Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Idea hii ungeipeleka Ulaya au ukawasiliana na bright Ideas [emoji362] huenda ukafanikiwa kama idea haijafanyiwa kazi bado duniani
Wazo zuri sana
 
Mimi kama mdau mkubwa upande wa automobile engineering, hii kitu anachotaka kiwe, inawezekana kama wahandisi watarudi kwenye drawing table. Madhala yake yatakuwa mengi hasa upande wa bei. Itakuwa hayanunuliki magari yenye 'state of the art' ya system hiyo na hata huyo mwenye uwezo akiwa nalo akienda sehemu ambayo ni 'utoporoni' mtandao ni wa kusuasua utashindwa kuwasha gari lako.
 
Sheria inakataza mtu asiye na leseni ya udereva kuendesha gari "no matter what"...
Vipi kama babako kupatwa na stroke daraja la 1 au 2 wewe mwanae kwa utundu wako unaweza kuendesha gari na kunusuru maisha ya babako, utaacha kuvunja Sheria hiyo au.....?
 
ni kama wazo la kijinga lakini lina mantiki sana.Kuna magari mengine ukipanda umelewa haliwaki hii
 
Vipi kama babako kupatwa na stroke daraja la 1 au 2 wewe mwanae kwa utundu wako unaweza kuendesha gari na kunusuru maisha ya babako, utaacha kuvunja Sheria hiyo au.....?
Ninarudia tena. Sheria ya nchi inakataza mtu asiye na leseni ya udereva kuendesha gari. Zingatia sana hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…