Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Watu wanamazito jamani
 
Hapo kwenye kinyesi me mwenyewe ilinitokeaga
Nilijisaidia kwenye shamba la jamaa ambaye pale kijijini alikuwa anaogopeka Sana
Basi Kumbe jamaa alikuwepo mle shambani kalala na aliniona
Akaniacha nimalize baada ya dk kadhaa nashangaa jamaa yupo nyuma yangu kashika panga
Akaniambia zoa hayo mavi na mkono
Nilichofanya nikachota kuanzia chini ya udongo kwani udongo ulikuwa mlaini nikaenda kutupa mtoni.
Aisee Kuna watu wanaroho ngumu Sana.
 
You must get over it bro, ila usisahau mafundisho ya mapito yako.

We were on the same boat.

Mpaka sasa am living my life ... bila ya msaada wa ndugu ...

life goes on
 
Tatizo kubwa la wazazi hasa wanaume wa Africa huwa hawaandiki wosia wakiwa hai, hii husababisha mitafaruku mikubwa sana baada ya wao kufariki kama mke ni dhaifu.

Pia utamaduni wa kishenzi wa baadhi ya jamii wa kufanya mali za mtu binafsi ni za ndugu wote au ukoo mzima imechangia kukuza hili tatizo la kugombea mali. Ni wakati sasa wa kutunga sheria inayosema mali za familia ni za mke, mume na watoto wao tu.
 
Trust me yanapita.
Nilifanya maamuzi magumu ya kwenda kusoma course nisiyoitaka ili tu nitafute nafuu.
Na kweli bana ile course nisiyoitaka na kuipenda ndio ikanipa ajira serikalini...!!
Hiyo ajira ikalipa ada ya kusoma ile course niliyoitaka..!!
Na sasa natumikia ile course niliyoitaka.

Nafuu ipo ila ukipambana huku unamuomba Mungu.

#YNWA
 
Watu wanamazito jamani
Acha tu ndugu yangu, na mbaya zaidi unakuta hao wa kujuita ndugu wakiona unaanza kupata unafuu kidogo wanakupiga hata kipapai.

Mwanzoni nilihangaika sana yani mpaka nikajiona nina mikosi tu hii dunia,kumbe kuna mtu kashaapa kwamba nitatanga tanga miaka yote mpaka siku nakufa bila kufanikiwa hata nikishika pesa kiasi gani.

Mbinu ni moja tu,ilikua ni kukata mawasiliano mazima yani wasijue kama niko hai au lah! Pia nikaamua kuachana na masuala ya kuulizia rasilimali za huyo Mshua.

Mpaka leo niko safe,niko kama mafichoni ila nina amani kiasi.
 
Safari yako hii ngumu ndo iliyokufanya pia uchukie suala la kuoa?
 

Pole sana
Huruma binadamu wengi tunayo pia wapo wwbaya
Ulikuwa na uwezo wa kumchukua na nafsi bado inakusuta kama ulikuwa na uwezo wa kumchukua na kuishi nae

Kusaidia watu ni wajibu wetu na pia kama una uwezo kulea pia ni nzuri zaidi
Umgekachukua tu maskini
 
Uko sahihi Kaka, kuna muda inabidi tu tukubaliane na hali,ila mimi suala la ndungu hapana aisee!

I swear to God katika kukua kwangu kwote mpaka sasa sijawahi kuishi kwa ndugu wa aina yoyote yule.

Kitu kinachoniuma mpaka leo ni kuniacha niishi nikiwa kama mtoto wa mtaani katika mji na mkoa ule ambao wamejazana na ndio chimbuko letu.
Kwamba hakuna hata mmoja aliekua na huruma na mimi?
Daaaaah wakuu kuna yime naishiwa mpaka nguvu ya kutyp...[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Mungu ni mwaminifu sana.azidi kukutunza na kukulinda kila siku ndugu yangu.wanadamu si watu wema(sio wote)

Tena bora hata mtu baki kuliko hawa ndugu 🥺🥺
 
Huyo Shangazi yenu aliwekeza wema kwenu na sasa anafaidi wema wake
Hao wengine walipandikiza chuki na sasa wanavuna

Binadamu ukitaka uwe na furaha mwisho lazima usaidie na kuwa mwema kwa watu
Hii itakupa furaha milele
Kuna waliotesa wenzao wakiwa wadogo na hata mkiwa wakubwa bado wanawatafuta kwa shari hao ni wa kuwapiga stop [emoji1630] na kuwapa ukweli

Kwa kweli fanya wema na uwe unawasaidia yatima direct isipite kwa mtu

Kama una uwezo wasaidie sana hata kuwapelekea nguo au unapikisha chakula pilau la nguvu siku ya Ijumaa au jumapili wanafurahi sana

Kama ni Xmas au Eid una waalika wote na kuwapikia
Hicho unakiona kidogo ila kwao ni faraja kubwa sana [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
How old is she? Kama anasoma ukiondoka si unamsimamisha masomo au?

Tho waweza ona ni sahihi ila unasababisha mtoto ashindwe kuform relationship later on atashindwa kuform na kumaintain relationship. Unapelekea emotional growth kukwama Na namna yake ya kuditch uhusiano will be just to up and leave.

Kusoma napenda.
 
BS ndugu yangu kwa kipindi nisingeweza kabisa maana nilikuwa ninapitia magumu sana.ingawa na magumu yote niliyokuwa nikiyapitia niliamini na Mpaka sasa ninaamini katika kutoa Kwa wahitaji..Imani yangu inaniambia nifanyapo hivyo basi namgusa Mungu moja Kwa moja.

Bado maisha hayajakuwa vile natamani yawe lakini naamin hiki kidogo nikipatacho nitagawana nao.

Kinandoto na malengo..nikishayafanikisha japo kidogo nitatafuta msaada Kwa watu wengine ili kufanikisha ndoto yangu yakuwa mama wa watoto wengi waliokosa mapenzi ya mama Na kupoteza matumani ya kupata upendo wa wazazi.
 
Unahuruma sana
 

Magumu uliyopitia wewe umeamua kumpitisha pia mwanao huyu wa kike kwa kumfanya akose upendo wa MAMA! Hivi unajua umemfanya mwanao naye awe 1/2 yatima??

Nakubali umepitia magumu japo kuna wengine wamepitia magumu zaidi, nasikitika kwamba badala ya kuwa mnyenyekevu shauri ya maisha uliyopitia umekuwa na kiburi na kujiona!
 
Uyatima mbaya sana Kaka,tena ni mbaya sanaaaa asikwambie mtu.

Ila licha changamoto mimi nilipenda sana shule,tena sana yani. Mpaka ilifika hatua nikiona watoto wanarudi kutoka shule na mimi niko tu kitaa nauza miwa basi naumia sana so kesho yake lazima niende shule.
Nilikua mtoro sugu.

Kipindi niko O.level walikua wananiita "Man Mawazo",yani muda nilikua najitenga peke yangu nawazaaa,naliiaaa baadae najicheka sana kwasababu hata nikilia niliona haisaidii kitu zaidi ya kupunguza maumivu tu ya kimaisha.

Kitaa wakawa wananiita "Kapipo", kwasababu nilikua nimekondaa ila nimekomaa kama chuma kwasababu ya kazi ngumu.

Daah wakuu acheni tu niishie hapa,ila kaka Liverpool VPN uyatima unatesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…