Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Pole sana mkuu, pole kwa mitihani uliyoipitia na mshukuru Mungu kukupitisha na sasa una shuhudia baraka zake kuendelea kutawala katika maisha yako.

Naiona sababu ya wewe kuchukia “KUOA”
lakini sio wanawake wote wana ubaya, huoni shangazi alkupambania ukiachilia mbali hali yake duni, waweza sema shangazi kwa vile ni dada wa baba yako, na mama zako wadogo je? Si ni wadogo zake mama yako?

Mshukuru Mungu kwa yote.
Halafu mmeshangaa sana yaani shangazi huyu ana moyo mwema hvyoo!mi najuaga ndugu wa mama ndo wanakuwaga na moyo kumbe wapo wenye mioyo mibaaya daahhh!mmeshangaa sana!yaani hukoo waliko wanajuta Leo wanaona ht aibu kwa ubaya wao
 
[emoji3][emoji3][emoji3]muone

Aise Nina huruma sana Kwa watoto ningekuwa hili swala ninauwezo nalo..hakika nisingeruhusu mtoto apitie changamoto kabisa.

Wiki kama mbili nilikutana na mtoto wa kiume(rika la kijana wangu kabisa)usiku Ana fanya biashara ya kuuuza nini Sijui huko aise nilimwaga machozi sana ujasiri sikuwa nao tena Kwa Yule mtoto.

Nikamwambia funga unachokifanya nifuate.nikampeleka sehemu ya kula ale akitakacho..aise mtoto alikuwa na njaa yule [emoji3064][emoji3064][emoji3064]..nilikahoji kanandoto ni katoto ambako kapo kwenye plans zangu.haijalishi ndoto zangu zitawahi ama kuchelewa lakini lazima nikawe mbegu njema moyoni mwake.

Itoshe kusema ninahisia za karibu mno
Wewe ni Mimi aseehh!sina tu uwezo ila natamani sana kuishi na wahitaji mnooo!!
 
Hapo kwenye kinyesi me mwenyewe ilinitokeaga
Nilijisaidia kwenye shamba la jamaa ambaye pale kijijini alikuwa anaogopeka Sana
Basi Kumbe jamaa alikuwepo mle shambani kalala na aliniona
Akaniacha nimalize baada ya dk kadhaa nashangaa jamaa yupo nyuma yangu kashika panga
Akaniambia zoa hayo mavi na mkono
Nilichofanya nikachota kuanzia chini ya udongo kwani udongo ulikuwa mlaini nikaenda kutupa mtoni.
Aisee Kuna watu wanaroho ngumu Sana.
[emoji23][emoji16][emoji16][emoji16]ila watu mnachekesha!
 
Uko sahihi Kaka, kuna muda inabidi tu tukubaliane na hali,ila mimi suala la ndungu hapana aisee!

I swear to God katika kukua kwangu kwote mpaka sasa sijawahi kuishi kwa ndugu wa aina yoyote yule.

Kitu kinachoniuma mpaka leo ni kuniacha niishi nikiwa kama mtoto wa mtaani katika mji na mkoa ule ambao wamejazana na ndio chimbuko letu.
Kwamba hakuna hata mmoja aliekua na huruma na mimi?
Daaaaah wakuu kuna yime naishiwa mpaka nguvu ya kutyp...[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
Pole sana
 
Amen BS

Nilishajaribu kuzungumza na baadhi wa watu wa karibu lakini najikuta nakatishwa tamaa wachache mno walilichukulia positive..

Wengi wanasema lazima uwe na kitu ndipo umfate mtu kutaka kitu..bado safari ni ndefu Nikipiga mahesabu kichwa kinauma..naishia kufanya sehemu ambapo mkono wangu unaishia.

BS naomba unioneshe njia.nishike mkono ikikupendeza..naamini katika hili nahitaji watu zaidi

Pole sana
Ila penye nia pana njia na kama unapenda kufanya kitu ambacho kina kheri basi utafanikiwa vuta subra

Mimi naishi nje ya nchi napambana huku kwa weupe
Na sijui pa kukusaidia na pa kuanzia ila unaweza kuulizia huko lazima njia zipo hata kuanza na kidogo tu
Nimeona baadhi ya sehemu Tz ambapo wanalea watoto yatima ila misaada inatoka kwa wazungu na wanaosimamia ni waswahili ila watoto hawana hali nzuri hivyo ingawa wamewekewa kila kitu ila washenzi wanakula hela za watoto kwa manufaa yao

Wanakera sana maana unaona kabisa watoto wana hali ngumu hata vyombo wanavyolia vimechakaa sana

Hiyo ni sehemu moja niliyokuwa naenda kuwaona

Kwa kuwa uko hapo unaweza kutembelea hata balozi kadhaa labda wanaweza kuwa na njia na misaada ya hivyo au contacts za watu wao au taasisi zao

Kila la kheri na ninatumaini kuna wengine humu wanaweza kusaidia maana kuna kila aina ya watu humu
 
Jana (Ijumaa) nikiwa kazini Kuna saa nilikosa Kazi (zilikua zimeisha). Nikawazaa, ghafla mawazo ya maisha ya UYATIMA niliyopitia yalinijia.

Ni ndefu sanaa we somaa.!

Japo siwezi kuyaandika yotee, maana UYATIMA wangu ulinipitisha kwenye makubwa sanaa..!!

Nilizaliwa kwenye familia ya watoto 3 tukiwa na baba na mama.
Baba alifariki kwa ku palaryze nikiwa mdogo sanaa.

Baba alikuwa ni mfanyabiashara mwenye mali nyingi ila mama alikua ni mama wa nyumbani.

Kwasababu ya kumkosa mumewe, baada ya baba kufariki mama alikuwa anaumwa umwa Sana.

Hii ilisababisha Mali nyingi kuuzwa na bila kusahau nyengine zilidhulumiwa na ndugu.

Ndugu na marafiki wa baba waligawana mali nyingi sanaa tukaachwa na nyumba tu ya kuishi.

Mama alikua anateseka Sana na mawazo ya kumpoteza mpendwa wake, hii ilisababisha kudhoofisha Kinga ya mwili na hatimae malaria kali ilimjia na kumchukua.

Ilikua ni siku ya jumapili nilipoletewa habari kuwa "Mama yako amefariki".
Aisee Ile siku ilikua nomaa, Mimi na mama tulikua na kijiwe chetu..!! Pale nyumbani (Kona ya barazani kwenye ua alilokuwa analipenda).

Aisee nilikaa pale na kulia sanaa, nilikumbuka ule usia wake, vicheko vyake, sura yake, harufu yake, kifupi niliona dunia imefika mwisho.

Wakati huo nikiwa mdogo sanaa (darasa la 4) ila huwezi amini NAKUMBUKA KILA KITU MPAKA LEO.

Nakuonya mwana JF "Usimfanyie mtoto ubaya" kwamaana "Hawezi sahau".
Mimi japo nilifanyiwa ubaya na ndugu tena nikiwa mdogo ila nakumbuka majina, siku, location yaani kila kitu kwa jambo nililyofanyiwa na ndugu.


Siku ya msiba wa baba watu walijaa wengi na waliiba Mali za pale nyumbani na wezi wote nawakumbuka ""wakina Wajomba zangu""

Baba alikua Tajiri hivyo nyumbani kwetu kulijaa ndugu waliokuja kuomba Msaada.

Ila baada ya baba kufa walipungua sana na baada ya mama kufa ndio kabisaa sikuwaona.

Tulianza kulelewa na dada.

Maisha ya ushua yalipotea na kama upepo, tukaanza shida.

Dada majukumu yalimzidi tuka hamishwa kila mtu kwake.

Mimi nikabaki Dar, mdogo angu mkoani na dada angu akabaki nyumbani.

Huko nilikoenda nilienda kwa mshua mmoja hivi taita Dar pale (rafiki wa baba).

Ila huyu "Mkewe hakunipenda kabisa" sababu mpaka leo huwa siijui.
Nilikua sili Sana, nilifanya Sana Kazi na mengine ila sijui kwanini hakunipenda.

Nilikaa pale miaka miwili, mama akaanda staili moja ili niondoke kwake.

Lile zegwe hausi geli alilijua.
Akanitahadharisha.

Nikamuhadithia shangazi
Shangazi alikuja kunichukua fasta.

Shangazi yangu hakua na maisha mazuri ila nilikomaa hivyohivyo.

Nilikomaa sanaa, chakula hakitoshi, Shule kwenda na miguu tena Dar es salaam, halafu mbali sanaa.
Mwaka mzima hununuliwi nguo mpya..!! Unavaa nguo za kushindia hizohizo mpaka mtaa una kukariri.

Ila nilikomaa.

Shangazi yangu hakuwa na room kwa watoto wa kiume, kwahiyo sometimes nilikua nalala kwenye korido na sometimes nje ya nyumba.

Yaani nje kabisa, milango inafungwa mi nafunga net kibarazani nalala.

Hakua ananitesa na nilikua nina amani.

Kwakuwa chakula kilikuwa hakitoshi nilianza kufanya Kazi kwenye nyumba za watu.

Maisha ya zamani ilikua mwenye hela ndio anabomba la maji la Dawasco.

Hivyo mi nilikua nachotea watu maji wananilipa ndoo moja 50.

Hapo nikawa napata nauli ya kwenda Shule (kipindi hicho mwanafunzi nauli 50).

Na nyengine kabla sijala nyumbani nilikua natanguliza kwanza sambusa, hivyo na kile kidogo cha nyumba nakua nashibaa.

Maisha yalienda mara la 7 nikafaulu.

Miaka ile kufaulu la Saba ilikua dili hasaaa.

Shuleni kwetu tulienda secondary Wa3 tu, yaani tulifaulu Wa3 tu..!!!

Mtaa mzima hongera...!!!

Kufika Shule nikaanza kucheza kamali ili nipate pesa ya kujikimu..!!

Nilikua nawala hasa.

200 inazalisha 3000 mpaka 5000.

Bwana eeeh Kuna siku ikapitishwa karatasi waandikwe majina ya wacheza kamali, na Mimi ndani...!!!

Tulipigwa sanaa siku ile, fimbo kama 100 hivi.
Enzi zile tulikua tunapigwa hasaaa.
Unashika chini huku umebongoa, walimu wanapita na fimbo, ukiishika Tako umefutaa.!!!

Tulipigwa sanaa.

Ila Sasa hata nikiacha kucheza nitapata wapi hela ya kujikimu shule..!!
Shangazi ya kunipa hana, hana uwezo wa kunipa nauli, je madaftari na vitabu atanunua?

Dah maisha yaliendelea, tukawa tunacheza nje ya Shule.

Kufika form 2 nikaongoza wastani kwa Shule nzima.

Ikabidi mwalimu wa darasa aniite "wewe una akili sanaa, kwanini unakua mtundu?"

Nikamuhadithia nayopitia nyumbani, huyu mwalimu niliona kabisa machozi yana mlenga.

Tokea siku hiyo alianza kunichukulia tofauti sanaa.

Form 4 nikaongoza kwa kupata Division 1 Kali sanaaa.

Taarifa zikaenea kwa ndugu na jamaaa + mtaani.

Hongera na masifa kama yoteee.

Ila nyumbani hali ilikua tofauti..!!

Binadamu yangu ye alipata 4 Mimi 1.

Mama ake ikawa kila jambo ananipendelea Mimi..!!

Binamu yangu alini mind sanaaa.

Akawa anatanitaka nitoke kwao, hii "Toka kwetu" mwanzo niliiona ya kawaida sanaa ili kufika form 5 ilikolea sanaa.

Kuna siku nilirudi nyumbani nikafungasha nguo na kusepa gheto la masela wapiga misuli.

Shangazi alimind sanaa.

Akaniita tukaongea na kuahidi kila jumapili nikachukue elfu 5 ya matumizi ya wiki.

Yaani kwa wiki utumie elfu 5..!!
Kula mchana, asubuhi, usiku na hela ya pindi mchikichini..!!

Nilikonda hasaa, maana kila siku nashindia miogo ya Shule.
Maana kila siku natakiwa kutumia buku..!!

Maisha yaliendelea taarifa zikamfikia baba mdogo.

Akaniomba niwe naenda kwake kuchukua misaada.

Nilienda kama wiki 4 mfululizo (kila jumamosi).

Nakumbuka Kuna jumamosi nilienda nikamkuta mkewe na baba mdogo hayupo.

Sasa bana Mimi Nina aibu ya kuomba Msaada kwahiyo muda wa kuondoka nikaaga ili niondoke kimya kimya.

Mama mdogo aliniita akanipa maneno makali "Unasababisha sisi tuishi maisha magumu kisa wewe....." aliongea mengi ila mwisho wa siku alinikataza kwenda kwake kuchukua misaada.

Na kama baba mdogo alijua maana hakuwahi kuniuliza lolote juu ya lile jambo.

Nilifika nyumbani siku hiyo nililia sanaa, nilikumbuka maisha ya baba yupo na mama.
Nililia balaaa.

Ghafla mama mdogo (ndugu wa mama) akaniambia niwe naenda kwake.

Huyu nae alinisaidia mara sijui 6 ya 7 nae akanipa dongo "Kwani wengine hawapo" nilibaki mdomo wazi.

Nikarudi gheto nikajisemea "Sitaki tena msaada nitakomaa mpaka nafia humu"

Ile elfu 20 ya mwisho niliyopewa Msaada nikafanya mtaji wa kuuza vitu vidogo vidogo Shule na mitaani.

Nikaacha kwenda mchikichini (tution) NECTA form 6 sikufaulu vizuriiiiii, ila nilipata credit za Degree.

Nilisoma PCB ila nilipenda sanaa mambo ya biashara.
Afya sikuiwaza kabisaa na Wala sikuipenda.

Sasa bana kuomba mkopo na post, post zinatoka chuo UDSM halafu bodi ya mkopo "NO LOAN".

Nani atanisomesha sasa??..!!!!!

Dah nikawazaa, kumbe shangazi yangu anahangaika.

Akanitafutia ufadhili mmoja wa ada.
Chuoni nikawa nalipa 240,000/= ya mambo mengine ya chuo ila ni Diploma.

Nikajisemea "yaani hizi C zangu za PCB naenda kusoma diploma, huku wenye E na D wanaenda degree"
Maisha gani haya...!!!

Nikabeba begi kwenda chuo.

Chuoni sikua na raha Wala amani, nilipenda masomo ya biashara ila nikawa nasomo visivyojulikana na moyo wangu..!!

Nikiwa Diploma 2 mdogo angu akamaliza form 4, akapata ufaulu wa kawaida ila sio wa kwenda advance..!!

Wakumsomesha HAKUNA..!!

UYATIMA nyie, Achana nao kabisaa...!!

Ikabidi nimpe ahadi ya kwamba anisubiri mi mwaka mmoja nimalize Diploma halafu yeye ataingia kwa ada yangu mi nitaishia hapo..!!

Ila kabla ya hapo nikiwa form 4 na 6 nasubiri matokea na post zakuendelea kusoma nilishawahi fanya sehemu tempo.

Kwahiyo lengo langu lilikua ni kumaliza Diploma halafu niende pale kujishikiza, then mdogo angu aingie chuo.

Nikamaliza diploma kufika ile ofisi kuongea na bosi akakubali. Kunipa Kazi.

Nikawa mpiga Kazi pale.

Nilikomaa kuishi maisha magumu hasaa ili tu mdogo angu aingie chuo.

Aisee ni mengi aiseee.

Ile dogo kumaliza Certificate nikamshikiza pale job na kikazi fulani hivi.
Huku Mimi nika apply Kazi serikalini nikapata Mkoani.
Dah hapo ndio ikawa kama nafuu imeanza kuja.

Maisha yalienda, serikalini kazini nikaomba ruhusa ya kwenda Shule kupiga Bachelor nikaunga Masters.

Sikuacha ndoto zangu zife, nilienda kusoma masomo ya biashara.
Ghafla zile ndoto zilizozimwa kisa yatima kakosa ada zikatimia.

Na mwaka huu naingia darasani kusoma PhD yangu..!!!

Na mdogo wangu aliendelea mpaka akapata CPA..!! Na mwaka huu anaingia darasani kusoma Masters.

Mama yetu alikua anatuambia "baba yenu alitaka na kutamani sanaa msome".

Angalau sasa hata tukifa tunaenda kuwaambia wazazi wetu "Tumemaliza yale mlioyatamani kutupa"

Dada yetu yupo na ameolewa na yeye ndio mama yetu.

Huwa tunamlea vizuri ""Japo tunampaga pesa kimya kimya ili shemeji asijue..!!!""

Aisee ni mengi aisee na siwezi kuyaandika yoteee.

Maana pia nilishawahi fukuzwa na shemeji (mke wa kaka - kaka mtoto wa baba mkubwa) bila kujua sababu..!!
Nilikua naendaga kuwasalimia, mkewe sijui akanichoka na kunifukuza ..!!!

Kifupi ndugu walikua wanadhani na hasa wake wa ndugu zangu walikua wanadhani sijui naenda kumaliza hela za waume zao.

Kifupi hakuna aliyenisaidia bila kulalamika, na kunisimanga.
Na wotee waliona Bora kunitimua ili nisiwaletee shida makwao.

Kifupi mpaka leo ndugu huwa siwaelewi.
Huwa wanapiga simu na kiukweli si "save" namba zao.
Na kesho wakipiga Tena na nikiwauliza "nani mwenzangu" huwa wanakata simu na kusema "huyu siku hizi yupo serikalini na kasoma basi anajidai sanaaa"

Na huwa hawaniambii direct ila Wana mwambia dada au shangazi.

Cha ajabu WAMESAHAU YOTEE WALIYOTENDA..!!!

Kifupi sina swaga yoyotee na ndugu YOYOTE.

Siwachukii ila SINA MPANGO NAO KABISAAA.

Ila mdogo angu anamsemo wake "Atavuna aliyepanda kwenye maisha yangu tu, kwani wakati hatuna wazazi na tunateseka walikua wapi"

Kifupi hatuna connection na ndugu wa upande wa mama woteeeeee yaani hata mmoja sijui yuko wapi.

Ila Kwa baba ni shangazi yangu ndio aliyepambana tukafika hapa..!!!
Tupo nae karibu na tunampenda sanaaa.

Baba yangu kwao walizaliwa Wa2 tu.
Yeye na dada ake ambae alitulea.

Nampenda sanaa shangazi yangu na namuheshimu sanaa.

Siwezi kufika Dar bila kumuona Wala kumletea Zawadi ni Mungu wangu aisee hapa duniani.

Ila ndugu wa mama HAPANA KWA KWELI.

Siwachukii ila HATA SIJUI WAKO WAPI NA SINA MPANGO NAO KABISAAA.
Waliamua kunitupa na Mimi nimejitupa mazima.

Dah tuishie hapo.....

YANAYONITAWALA KICHWANI.

1. Natamani kumuuliza yule mama wa mshua, kwanini alipanga kunifanyia lile tukio ili mumewe anifukuze?

2. Natamani kuwauliza wajomba zangu, kwanini mliamua kutudhulumu mali zetu?

3. Natamani kuwauliza mama wadogo, kwanini mliamua kumuacha dada yao (mama yetu) atulee kwa shida wakati wao walikua wanakuja kwake kulia shida?

Kifupi natamani tu nikae na walionifukuza halafu niwahojii kwanini walinifanyia vile.
Yaani tuhojianee weee mpaka moyo ukaridhika.

Natamani nikae na walionipitisha kwenye shida niwahojiiii mpaka niridhike.

KITU NILICHOSHINDWA NI KUWATAFUTA NA KUONGEA NAO.
Najua watakua wanamiliki simu ila hata kutafuta namba zao NIMESHINDWA ..

Na nimepitia mengi siwezi kuyaandika yoteee mengine yanauma na kuumiza.

Tuishie hapa.

Miss you Daddy and Mammy.

UYATIMA ni nyokooooo sanaaaa.
Kaka stori mboni kams inanihusu na ni kop mwenzangu?? Nimepitia yanayofanana na hayo na sasa nipo mahali nasema alhamdullilah,na ndugu wanasema naringa,ila cha muhimu tu umeahau kutokumtendea mabaya yatima kwani huwa ndo chachu ya kujituma na kufikia malengo! Mm ndo namalizia masters now kwa nguvu zangu mwenyewe!
 
Kaka stori mboni kams inanihusu na ni kop mwenzangu?? Nimepitia yanayofanana na hayo na sasa nipo mahali nasema alhamdullilah,na ndugu wanasema naringa,ila cha muhimu tu umeahau kutokumtendea mabaya yatima kwani huwa ndo chachu ya kujituma na kufikia malengo! Mm ndo namalizia masters now kwa nguvu zangu mwenyewe!
Komaaa sanaa mwanangu.
Mungu yupo nae ni BABA WA YATIMA.

See You on Top..!!

#YNWA
 
Amen BS

Nilishajaribu kuzungumza na baadhi wa watu wa karibu lakini najikuta nakatishwa tamaa wachache mno walilichukulia positive..

Wengi wanasema lazima uwe na kitu ndipo umfate mtu kutaka kitu..bado safari ni ndefu Nikipiga mahesabu kichwa kinauma..naishia kufanya sehemu ambapo mkono wangu unaishia.

BS naomba unioneshe njia.nishike mkono ikikupendeza..naamini katika hili nahitaji watu zaidi
Mungu akufanikishe hitaji lako utafanikiwa..Mimi nillimchukua mtoto wa marehemu mpangaji wetu,aliacha watoto wawili wakike na wakiume!alikua std 5 huyu wa kike!baba na mama ake walichana b4 hajafa,alivyokufa wakahama siku moja nkapigiwa simu kua madogo hawaendi shule hakuna wa kuwasomesha daahh!I cried that day!nakumbuka nilikua maeneo ya tabata nililia sana!nkaenda kwao nikamchukua wa kike Niko nae yuko form nilipo yupo na hua namtambulisha kama my first born!!kaka ake alipelekwa kijijii kama ningekua na uwezo ningelea wote ila nimepanga huyu nimhamishe kijijini aje mjini akae kwa mama ake nimsomeshe walau nae afikie kidogo malengo yake !ndugu wamewatelekeza wakati enzi yule kaka yuko hai walikua wanajaa mpk alishindwa kujenga kwa sababu ya kusaidia ndugu zake alivyokufa hakuna ht anaejua watoto wako wapi!Niko na huyu binti mwaka wa saba sijawahi ulizwa hata ameamkaje na nduguze.
Ila mmeahidi huyu wa kike nilie nae n
Ila wa kike naomba Mungu anipambanie afikie malengo yake sina kikubwa maisha yangu ya kuunga unga lakini napambana nae!

Sijwahai ishi kwenye uyatima na sijui nimelelewa na baba boraa kabisaa ktk hii dunia ila naumia kuona yatima au mtoto akinyanyasika!
Nikiendaga orphanage hua nalia sanaa
 
Pole sana. Zamani nilikua najua mashangazi ni watu wa hovyo hawana msaada tofaut na ndugu wa mama. Hakika umeni-prove wrong.
Kwa asilimia kubwa watoto huwa wunakua na bond kubwa na ndugu upande wa mama (wajomba, mama wadogo/wakubwa).
Lakini ikitokea mzazi/wazazi wote hawapo duniani mashangazi (au upande wa baba kwa ujumla) ndio wanakua(ga) na msaada zaidi kwa watoto walioachwa.
 
Pole sana
Ila penye nia pana njia na kama unapenda kufanya kitu ambacho kina kheri basi utafanikiwa vuta subra

Mimi naishi nje ya nchi napambana huku kwa weupe
Na sijui pa kukusaidia na pa kuanzia ila unaweza kuulizia huko lazima njia zipo hata kuanza na kidogo tu
Nimeona baadhi ya sehemu Tz ambapo wanalea watoto yatima ila misaada inatoka kwa wazungu na wanaosimamia ni waswahili ila watoto hawana hali nzuri hivyo ingawa wamewekewa kila kitu ila washenzi wanakula hela za watoto kwa manufaa yao

Wanakera sana maana unaona kabisa watoto wana hali ngumu hata vyombo wanavyolia vimechakaa sana

Hiyo ni sehemu moja niliyokuwa naenda kuwaona

Kwa kuwa uko hapo unaweza kutembelea hata balozi kadhaa labda wanaweza kuwa na njia na misaada ya hivyo au contacts za watu wao au taasisi zao

Kila la kheri na ninatumaini kuna wengine humu wanaweza kusaidia maana kuna kila aina ya watu humu
Hiki unachokisema ni kweli kabisa BS.

Kituo changu kitakuja kuleta mapinduzi makubwa sana na ninauhakika hawa watoto hawatajuta kukaa mikononi mwangu..niamini..

Ninachotaka kukifanya si msukumo wa kupata pesa na kufanya matanuzi bali ni kuwa mbegu na kumbukumbu nzuri Kwa watoto walikata tamaa..trust me nitafanikiwa.hii kitu iko ndani yangu Kwa miaka mingi..nitakwenda kutimiza ndoto za watoto wengi sana.

Asante BS nitayafanyia kazi yote ya muhimu
 
Back
Top Bottom